Je, Mwakyembe kujiuzulu Ubunge?!

kikwete is losing control ya nchi na ya chama.
kikwete anaunda tume ili kubabaisha watu na tume ikitoa jibu anababaisha kutekeleza yaliyogundulika.
akiona nchi imekaa pabaya, anatafuta safari anakwenda nje kwanza, angalau kwa siku mbili tatu anaacha kusikia kelele za epa.
tulichoambiwa kelele za mlango sasa naona zimeanza kuwakosesha wakuu usingizi.
nb; baada ya wiki moja kikwete anaruka kuelekea mkutano wa G8 japan.
 
Ningeendelea kuishikia bango ishu hivyo hivyo. Sio kuanza kuyumba yumba ku second guess maamuzi yako mwenyewe ulipochagua nini ukiweke, na nini usikiweke kwenye ripoti yako.

Huwezi sasa hivi kuja kutishia kujiuzulu, au kuanika vitu ambavyo umesema vina madhara kwa taifa ili tu ku dili na maadui zako. Hatakiwi kuwa na hasira hasira za mkizi kama hizo.

Mara nyingi wenyeviti wa tume za uchunguzi wanachaguliwa watu fulani ambao wanaheshimika sana katika jamii. (Nyalali, Warioba, Bomani...) Hii ni kwa sababu tume ya uchunguzi inatakiwa ifanane fanane na taswira ya mahakama, itende haki. Ndio maana huwa wanachaguliwa watu ambao wana track record ya utauwa fulani hivi, hawana bifu na mtu, hawakasiriki kasiriki, na wametumikia nchi kwa uadilifu na taadhima. Elder Statesmen. Hasira ni nzuri, zinazochukia ufisadi na uzembe na usanii wa Bunge. Lakini sio za mkizi za kutishia kuanika yasiyomo kwenye ripoti.

Inawezekana kinachomsuta ni kwamba yeye kama Mwanasheria anajuta jinsi wataalam wenzie walivyo shtukia blunder alilolifanya la kutompa mtuhumiwa nafasi ya kujieleza. Hata majumbani ukisema "natafuta mtoto gani amevuja glasi, namshuku Juma," utaambiwa umemuuliza Juma? Hicho kitu ni cha asili sana, ndio maana Lowassa akasema kinaitwa natural justice.

Hata mimi ningependa "kufaidi" kusikia hayo mengine, na simpendi huyu Lowassa. Lakini kama hayana uzito wa kuingia kwenye ripoti, basi ni hearsay. Kaa nayo. Udaku.

Mwakyembe asianze kuchemsha.

Na wewe Kuhani usichemshe sasa. Nafikiri waiyomchagua Mwakyembe waliona anafaa kufanya kazi hiyo. Anajua anachosema na sio peke yake lazma ame consult wenzaake wakafikia uamuzi huo.Tuvute subira tutayaona.
 
Harisson pokea zawadi hii ndogo toka kwangu

Zaburi:23
Zaburi:35

hapo ungeweka link iwe rahisi kusoma hizo zaburi, kuliko tuanze tena kupekua bible anyway hiyo zaburi 23 ipo kichwani ngoja nitafute hiyo 35. asante
 
Usimtuhumu mwakyembe hizi habari haziwezi kuwa zipo 100% kama zilivyoletwa hapa JF. tuwe nasubiri na pia maoni yako haya ni krudisha nyuma lengo la kutokomeza ufisadi

Usinishutumu kabla hujasoma mtiririko wa line of discussion. Nilikuwa najibu hypothetical nilipoulizwa "ungekuwa wewe ungefanyaje." Lakini the origina posting was worded extremely carefully:

Mwakyembe ana maana gani kusema- kama kweli amesema - eti kuna mambo hakuyaweka kwenye ripoti....

Mi napinga na udaku unaoletwa jamvini hapa. Kama sijaona nukuu ya alichosema, ni udaku, for all I know. Kwa hiyo siwezi nika bugi stepu na kukurupuka ku accuse mtu bila uhakika na kilichosemwa.
 
Jamanni haya ya dini tuyapeleke kwenye dini na ya siasa yabakie siasa.. tukianza kufanya ya siasa yawe dini tutaenda mbali. Ni ushauri tu. Kutoka kudaiwa kuwa JF ni ya Chadema watakuja watu na kusema ni ya Wakristu n.k ...
 
Mstari umeshachorwa ardhini.. kuna walioanza kuuvuka na kuna wale ambao kamwe hawatouvuka. Na wakiendelea hivi tutakuwa na uchaguzi mdogo kwenye majimbo kadhaa kabla ya Novemba. Sikutaka kuandikia hili (kwa maombi ya Reverend) ili kutoa muda wiki hii wa nadharia niliyokuwa nimeijenga, but now I know ni dhahiri nilichofikiria ndicho.

Nadhani kitafanyika kikao cha wana CCM Bungeni na huko ndiko "puta nikupute" itafanyika
.

Utabiri wa mwalimu utatimia hivi karibuni, nafikiri looser watakuwa watakaoangukia katika kundi la MAFISADI hawa lazima tuwatafutie majina mazuri sana ya kuweza kuwamaliza nguvu kabla ya uchaguzi wa 2010.

Lazima tuanzishe propaganda kali sana za kuweza kuhakikisha hili kundi halisimami kijiji chochote bila kuzomewa.

Kwa mfano ukiwaambia wananchi wa kawaida kule vijijini kuwa Pesa ya EPA ni billioni 133 hawawezi kuelewa vizuri itatakiwa kusema unaweza kujaza malori 133. hapa nagalau wataweza kuelewa kidogo.
 
Tuki balance na aya za Kiislamu itatatua tatizo? Nimshtue Allah's Slave kwenye PM?

bado itakuwa ni masuala ya dini.. dini iende kwenye dini mwenye pambio, tenzi, aya, sura, n.k aende nazo huko tutakimbilia kuimba na kusoma. Siasa ibakie siasa, of course kuna vya kuchomekea ambavyo sidhani ni tatizo.. lakini twende pole pole. NI maoni tu.
 
Jamanni haya ya dini tuyapeleke kwenye dini na ya siasa yabakie siasa.. tukianza kufanya ya siasa yawe dini tutaenda mbali. Ni ushauri tu. Kutoka kudaiwa kuwa JF ni ya Chadema watakuja watu na kusema ni ya Wakristu n.k ...

I agree..... dini ibakie kwenye jukwaa lake muhimu kabisaaaa na makeke yake yote ambayo mimi nimeogopa kabisa kuingia huko kuchangia chochote.
 
Neema Kwa Ndesamburo neema Imefunguliwa

Neema Neema Neema Imefunguliwa

Neema Nakwa Slaa"" Neema Imefunguliwa

Neema Neema Neema Imefunguliwa

Neema Kwa Shujaa "" watanzania"" Neema Imefunguliwa

Neema Neema Neema Imefunguliwa

utukufu Apewe Bwana Yesu Apewe Bwana
[/QUOTE]

Neema kwawapenda amani
Neema imefunuliwa
Neema neema neema imefunuliwa
Neema kwa wabunge shupavu
Neema imefunuliwa
Neema neema neema imefunuliwa
Hallelluya
 
sioni kama kuna mwanga wowote katika bunge hili, samahani nisiwakatishe tamaa lakini naanza kukata tamaa.
 
bado itakuwa ni masuala ya dini.. dini iende kwenye dini mwenye pambio, tenzi, aya, sura, n.k aende nazo huko tutakimbilia kuimba na kusoma. Siasa ibakie siasa, of course kuna vya kuchomekea ambavyo sidhani ni tatizo.. lakini twende pole pole. NI maoni tu.

Mimi na quote whatever is sensible, Shakespeare, Jay-Z, Bob Marley, Fela Kuti, The Bible, The Quran, The Bhagavad Gita, The Vedas, The Dhammapada, Lao Tzu, Tibetan Book Of The Dead, The Tripitaka,Methali za Kiswahili, Quantum Physics, Alfu-Lela-U-Leila you name it.

As long as it is sensible and applicable.

At the same time nazi blast hizo zote hapo juu, as long as they are not sensible.

Kwa nini tujipunguzie wigo wa utajiri wa fasihi?

Ah I know where the problem is, to me dini is fasihi and mythology, equal to Shakespeare, to some.... well not quite.
 
bado itakuwa ni masuala ya dini.. dini iende kwenye dini mwenye pambio, tenzi, aya, sura, n.k aende nazo huko tutakimbilia kuimba na kusoma. Siasa ibakie siasa, of course kuna vya kuchomekea ambavyo sidhani ni tatizo.. lakini twende pole pole. NI maoni tu.

Ndio maana ilibidi uachie pale pale panaposema dini sio mahala pake.

Ulipoanza kusema JF itakuwa ya Wakristo, tayari umeingiza dini.

Kwamba tatizo ni Ukristo umezidi. Ndo nikasema basi na wenzenu waki balance kwa kuchomekea chomekea aya za Kurani, hilo lingetatua tatizo. Mtakuwa mko on par. Nikataka kumshtua Allah's Slave. Based strictly on pure logic.

Kwa hiyo, aidha kuna imbalance ya mapambio ya dini moja au mapambio -yawe ya ki-Budha, ya Kisingasinga, ki Confucionism - yakizidi, sio mahala pake. Hata yakiwa fifte fifte. Nukta.
 
Kuhani hapo juu umesound kama CHRIS TUCKER MWENYEWE!
Yani very artistical yet classic with a decisive message and tone.
 
chitaliko!chitaliko! lowasa na rostam wanakulipa kiasi gani? hivi mshahara wanaokulipa ni mkubwa kuliko unaolipwa na wananchi wa buchosha?
 
Ndio maana ilibidi uachie pale pale panaposema dini sio mahala pake.

Ulipoanza kusema JF itakuwa ya Wakristo, tayari umeingiza dini.

Kwamba tatizo ni Ukristo umezidi. Ndo nikasema basi na wenzenu waki balance kwa kuchomekea chomekea aya za Kurani, hilo lingetatua tatizo. Mtakuwa mko on par. Nikataka kumshtua Allah's Slave. Based strictly on pure logic.

Kwa hiyo, aidha kuna imbalance ya mapambio ya dini moja au mapambio -yawe ya ki-Budha, ya Kisingasinga, ki Confucionism - yakizidi, sio mahala pake. Hata yakiwa fifte fifte. Nukta.

Ndio maana kuna mtu alishauri kuwa majukwaa yote yaunganishwe na jukwaa la siasa, inawezekana alijenga kwenye hii argument yako kuwa kila kitu ni sawa tu as longer as kina balance.. ndio hivyo?
 
Mwanafalsafa wa Kijeruman Arthur Schopenhauer aliyeishi kati ya miaka ya 1788-1860 aliwahi kusema.
"Ukweli Wowote hupitia Ngazi tatu.

Kwanza ngazi ya kukejeliwa.
Pili,ngazi ya Kupingwa na hata ikibidi damu kumwagika .
Tatu, ni Ngazi ya Kukubalika ,kwa kuwa ukweli hujisimamia wenyewe"

Richmond ,Lowassa , na Mafisadi sasa wapo hatua ya ngapi?
 
Back
Top Bottom