Je mtoto anaweza kuwa chanzo cha kupunguza kasi ya mapenzi kati ya wapendanao?

Prime Dynamics

JF-Expert Member
Dec 30, 2010
551
249
Mtoto ni baraka katika familia husika lakini pia anaweza (mtoto) kuwa chanzo cha kupunguza kasi ya mapenzi kati ya wanandoa. Hali hii huanza baada ya mwanamke kubeba mamba, kwavile mara nyingi huwa na hali ya kuchagua vitu au anachotaka tofauti na mwanzo wa mausiano.
Mtoto akipatikana huja na maitaji yake amabayo yana’ffect energy level ya mwanamke, kamavile kuamka usiku mara kwa mara kumhudumia mtoto, kama vile kumbadilisha ngua nk. Hali kama hii hubadili nguvu za mwanamke ndani ya nyumba na inakua ngumu kua’ttentive kama mwanzo wa mapenzi. Hali huwa mbaya zaidi kama mwanamke hana msichana wa kumsadia kazi za nyumbani. Na pia mtoto huja na financial implications abazo huondoa au kupunguza ile hali ya kwenda kupata chakula cha jioni sehemu (out for dinner) au kuletewa zawadi kama hapo mwanzo wa mausiano.
Mimi nadhani hapo ndio hitilafu ya mapenzi inapoanzia kwa wapendanao.
 
.........inawezekana kuna ukweli ndani yake, mtoto anaweza kufanya mama kuwa busy kiasi kwamba unasahau kwamba kuna mume naye anahitaji huduma. Halafu kuna ule upendo mama anaupata kutoka kwa mtoto......yaani unaona mtoto ndio kila kitu kwako, mawazo yote yanaenda kwa mtoto.
 
Haiwezi kupunguza mapenzi ikiwa na wewe baba utakua jirani na mtoto sometimes unamwambia mama lala tu acha nimbadilishe nepi kama analia unambembeleza mpaka analala unless anataka kunyonya ndio unamwamsha mama yaani ukimsaidia saidia vijikazi vya mtoto wala haiwezi kupunguza mapenzi zaidi mapenzi yataongezeka. Kuna wababa wengine mtoto akikojoa tu utamsikia we mama nanihilu mwanao ashanikojolea bwana njoo umchukue au akilia tu kidogo baba hafanyi jitihada zozote za kumbembeleza mtoto matokeo yake hata kamam anapika anamwita aje achukue mtoto ukifanya hivyo lazima mapenzi yapungue
 
Hasa huyo mume akiwa amefanywa MTOTO - FIRST BORN - NA MKEWE - akija mtoto halisi anajisikia hatendewi haki - anakwenda kutafuta MAMA wa nje badala ya MKEWE

WANANDOA - MAISHA YANAKUWA KAMA YANAVYOPELEKWA - ILA JAMANI WABABA - CHANGE IS NEEDED ..........utoto huo hadi lini???? MTOTO KWENYE FAMILIA ANALELEWA NA WOTE - KUAMKA USIKU ANAPOLIA ETC. SI KUPEANA COMPANY JAMANI????? NDOA SIO JARIBU LA MWANAMKE ILA NI RAHA KWA WOTE

ni mawazo yangu
:angry::angry::angry::angry::angry:
 
Haiwezi kupunguza mapenzi ikiwa na wewe baba utakua jirani na mtoto sometimes unamwambia mama lala tu acha nimbadilishe nepi kama analia unambembeleza mpaka analala unless anataka kunyonya ndio unamwamsha mama yaani ukimsaidia saidia vijikazi vya mtoto wala haiwezi kupunguza mapenzi zaidi mapenzi yataongezeka. Kuna wababa wengine mtoto akikojoa tu utamsikia we mama nanihilu mwanao ashanikojolea bwana njoo umchukue au akilia tu kidogo baba hafanyi jitihada zozote za kumbembeleza mtoto matokeo yake hata kamam anapika anamwita aje achukue mtoto ukifanya hivyo lazima mapenzi yapungue

i:amen:
 
Back
Top Bottom