Je Mrithi wa Regia ilikuwa lazima atoke kasikazini??

Hakuna ulazima wa mtu wa ku replace atoke kusini katikati wala pembeni..list iliyopo tume ifuatwe mbunge mpya atajwe aapishwe akalie kiti aanze kazi haraka..na nyie ofisi za bi kiroboto haraka muandalieni vx lake alikute liko tayari
 
CHADEMA wanaangalia zaidi QUALITY AND NOT QUANTITY. Tulishasema hatumchagui mtu kwa kabila lake wala dini yake na hata anatokea kanda gani. hizo hazina nafasi katika dunia ya werevu. ni mawazo yetu ndo yanauona huo ukaratu but kwangu binafsi naunga mkono ubora wa mtu na si atoka wapi.

Kwahiyo wenye ubora wote wanatoka kaskazini? Jibu hapo!
 
Ulieanzisha mada usome taratibu

Ni Diwani wa kata moja wilayani Karatu

Alishika nafasi ya 26 Viti Maalum Chadema





Marehemu Regia Mtema


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema mwanamke aliyeshika nafasi ya 26 katika majina 102 yaliyopelekwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), mwaka 2010 kwa ajili ya kufanyiwa uteuzi wa ubunge wa viti maalum, ndiye atakayemrithi marehemu Regia Mtema, aliyefariki dunia wiki iliyopita.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, alisema hayo alipotakiwa na NIPASHE kutoa ufafanuzi kuhusu nafasi iliyoachwa wazi baada ya kifo cha marehemu Regia.
Habari zilizopatikana kutoka makao makuu ya Chadema, zinaeleza kuwa mwanamke aliyeshika nafasi ya 26 katika majina 102 yaliyopelekwa Nec, mwaka 2010 kwa ajili ya kufanyiwa uteuzi wa ubunge wa viti maalum, ni Cecilia Daniel Pareso.
Cecilia ni Diwani wa Kata ya Qurus, iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.
Habari nyingine zinaeleza kuwa awali, mwanamke aliyekuwa akishika nafasi ya 26 ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Leticia Mosore, ambaye baadaye alihamia chama cha NCCR-Mageuzi.
Dk. Slaa alisema utaratibu wa kuwapata wabunge wa viti upo wazi kwa mujibu wa sheria na kwamba Chadema hawana mamlaka ya kuongeza wala kupunguza kitu chochote.
Alisema Chadema imeishamuandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda, kumuarifa rasmi kwamba kuna nafasi iliyo wazi, ambapo naye ataiandikia barua Nec kwa ajili ya kufanya uteuzi rasmi.
Dk. Slaa alisema kuwa kama kutakuwa na mabadiliko ya mtu aliyeshika nafasi hiyo ya 26, ikiwamo mtu huyo kupoteza sifa ya kuwa mbunge kwa kuhama chama ama kuonekana na upungufu mwingine ambao unamnyima sifa, Chadema itaiandikia barua Nec ili achukuliwe mtu mwingine aliyeshika nafasi ya 27.
Alisema kama namba 26 na 27 wote hawatakuwa na sifa, Nec itachukua jina litakalofuata namba 28 ili kufanya uteuzi wa kiti hicho.
“Sisi kwa hili tulishalimaliza mwaka 2010 na tunachoweza kufanya kwa Nec ni kuisaidia itakapotaka maelezo yetu juu ya jina linalotakiwa kufanyiwa uteuzi,” alisema Dk. Slaa.
Alisema mwaka 2010 walifanya kazi kubwa na kupata majina 102 ambayo yote yana sifa za kuwa wabunge wa viti maalum na kwamba, Nec ndiyo yenye mamlaka yote ya mwisho na sio Chadema.
Chadema kina wabunge wa viti maalum 25 katika Bunge la 1



 
Siyo ulichosikia, huo ndio utaratibu ulivyo na haujaanza leo, kumbuka hata Geturde Lwakatare aliingia bungeni baada yakifo cha Salome Mbatia, na yeye katika ile orodha jina lake ndio lilikuwa linafuatia.
Kumbe huyu Kakakiiza ni sehemu ya vilaza hapa JF? mbona hakuwahi kuhoji kwa nini mkoa wa Morogoro uwe na wabunge wa viti maalum wawili Regia Mtema na Suzan Kiwanga wakati mkoa wa Lindi hauna hata mbunge mmoja wa viti maalum!!?? huku ni kufikiri kwa kutumia kijambio.
Hata mimi nashangaa sana. Inaonyesha haya yote yanawekwa pembeni linapokuja suala la Chadema. Mtu anapendekeza Uchaguzi uanze upya sijui kwa kutumia sheria na taratibu zipi? Unaposema haraka haraka, mimi sijasikia Chadema wakiongelea hili bali ni Maafisa wa NEC walioongea habari hizi tena sio officially.
 
Kwahiyo wenye ubora wote wanatoka kaskazini? Jibu hapo!
Wewe na Kakakiiza kuna majukwaa yenu maalum mmetengewa humu naomba mtupishe hakuna unaloweza kuchangia hapa, nenda MMU kule utamkuta mwenzio kakakiiza kutwa wao kuongelea ngono, kaanzisha thread hapa halafu yeye kakimbilia jukwaa la MMU pimbi kabis huyu.
 
hii ya kuchagua viongozi kwa ukanda na mikoa ni ujinga. Imesababisha baadhi ya viongozi kuondelea kushikilia madaraka na hata wizara kwa kigezo cha mkoa au kanda..lets focus on quality and not otherwise. Ingekuwa kuwa hivyo hata wamarekani wangekuwa wanapokezana kwa wazungu na weusi. Kama mnavyosema ni zamu ya Zanzibar kuongoza bara hata kama hana uwezo..
 
Nakuunga mkono KK. CDM iajipaka matope chenyewe badala ya kusubiri kipakwe matope na opponents. Walichofanya siyo rahisi kueleweka
Duh Mkuu unanichekesha sana, hivi uelewa wako ndio umeishia hapo? Walichofanya kipi sana hapo kwenye bold? Au umevamia mada tu? Umeambiwa kazi yote sasa hivi inafanywa na NEC sasa kosa la Chadema ni kumweka Cecilia kwenye nafasi ya 26? Majungu tu
 
KK nimesoma thread yako lakini wapaswa kukumbuka kitu kimoja kwamba CHADEMA hawakuchagua wabunge wa viti maalumu kutoka hewani, walikuwa na vigezo vyao walivyotumia, baadhi yake ni Elimu ya muhusika, Mchango wake chamani, Aliyegombea jimboni na kura alizopata(Kwangu mimi hili ni la muhimu sana) na kadhalika.

Hivyo hata dada Regia Mtema hakuchaguliwa ilikubalance ukanda bali ni kutokana na vigezo hivyo! Na kwa mujibu wa sheria Tume ya uchaguzi baada ya kifo yenyewe ndo inahusika na taratibu za viti maalumu.

Mi ningekushauli badala ya kuja na malalamiko muda huu, ungeangalia vigezo vya chama kuhusu wabunge wa viti maalumu wanavyopatikana halafu ungeenda kwenye kanda hizo(ambazo umezitaja na nyinginezo) pindi uchaguzi utakapokaribia ukawahamasishe wananchi na wanachama wa chadema maeneo hayo, wajitokeze kwenye kugombea majimbo na kukijenga chama ili mara uchaguzi unapoisha na kujikuta hawakufanikiwa kupata ubunge(wa kuchaguliwa) wawe na vigezo vya kuupata wa viti maalumu.

Kwa utaratiu huo utakuwa umewasaidia watu wa maeneo hayo, lakini ukingoja kuja na thread zako za kulalamikia kila kitu na kuonyesha ishara ya ukanda hautakuwa unakijenga chama bali ni kukibomoa maana ni chuki tu ndizo zitatawala.
 
karatu? Duu. Hiv mtwara, lindi, pemba, unguja, nk kuna wawakilishi wowote wa viti maalum. Mi binafsi sio haja ya kuwa na wabunge 2 moja wakati kuna sehemu nyingi hakuna hata mbunge. Kama cdm wanataka kujitanua na wanadhamira ya kweli! Sisem mingi nicje nikashambuliwa.


Uongozi au ubingwa katika taaluma havitolewi kama zawadi bali unatakiwa apewe mtu ambaye ana uwezo kwa vigezo vilivyokubalika. Hawa wanaofikiria kimaeneo, bila shaka wangetaka hata uwaziri utolewe kimaeneo. Wanang'ang'ania idadi sawa ya ubunge wa kuteuliwa lakini hawazungumzii uwiano wa wabunge wa kuchaguliwa ambao kimantiki ndio waliouzaa nafasi za ubunge wa kuteuliwa. Hawazungumzii maeneo kama ya vyuo vikuu, mahospitalini na taasisi mbalimbali ambako kuna wataalam wengi wa huko kaskazini. Kama vigezo vimefuatwa kama vilivyowekwa, hakuna sababu ya msingi ya kusema ni lazima mbunge wa kuteuliwa atoke wapi. Na kwa chama makini ni lazima wakati wote kuendesha mambo kwa taratibu zilizokubalika. Anayetaka wabunge wa kuteuliwa wapatikane kwa kuangalia maeneo, anatakiwa aanze na kubadilisha vigezo siyo kuanza kwa kubadilisha majina ya wanaostahili kuteuliwa. Watanzania tutabadilika lini ili tuweze kuishi na kutenda mambo kwa kufuata sheria na kanuni tunazokubaliana? Shame to all who advocate for regionalism to be a deciding factor. Hapa haufanyiki uchaguzi, uchaguzi uliisha mwaka 2010, sasa kinachofanyika ni kufuata utaratibu.
 
Na ili kuweka kumbukumbu sawa, aliyepaswa kurithi nafasi hii ya Regia Mtema ni Leticia Mosole ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa Bawacha lakini baadae akajitoa CHADEMA na kujiunga na NCCR MAGEUZI, kwa hiyo amepoteza sifa ya kuwa mbunge kupitia Chadema kwahiyo anapewa nafasi yule ambaye jina lake linafuatia.
Kufikia hapa nadhani Kakakiiza ungeitendea haki hii thread yako ya kipimbi utoke huko MMU na uje hapa jukwaani na wewe uanze kujibu hoja, sio unaanzisha thread za kifala halafu wewe unakimbilia jukwaa la MMU.
 
mimi ninacho jua, chadema haitoi viti maalum kama njugu yaani kama zawadi au fadhira hapana. chadema tangiapo ilishatoa vigezo vyake ili uwe mbunge wa viti maalum.
1. uwe umegombea na kupata kura za kulidhisha
2. uwe umeenda shule
3. uwe umekisaidia chama(uwe na uchungu na chama) sio leo wanakupa ubunge kesho unauuza kwa ccm. na baada ya uchaguzi wa 2010 kuisha kuna list ya watu 102 ilipelekwa nec. so nec watachagua kutoka hapo. sasa hivi waliishia namba 25. itakayofuata ni namaba 26, 27, 28, 29, 30....
 
Channel TEN

Ingependeza sana kama ungefanya kautafiti kidogo ukajua ni utaratibu gani umetumika, ni option gani zilikuwepo, na opportunity gani zingeweza kutumika. Sishani kama unatutendea haki kwa kusikia tu habari kwenye TV, na kuja na maoni ya moja kwa moja...
 
Nashauri tu thread hii ni ya kuipotezea tu, maana tunaweza kupitwa na topic za maana kwa ufala wa jinga moja tu kama hili. am out of thread now!!
 
Kweli watu huwa wanapenda malumbano yasiyo na sababu..Sasa hapo kisichoeleweka ni nini?Si muende mukamuulize spika taratibu za uchaguzi ni zipi kama hamtaki kuelewa hapa?
 
Mi ninachojua chadema kwa sasa hawahusiki na uteuzi wa Viti maalum.
Uchaguzi ulishafanyika tangu 2010 na list ikapelekwa NEC.
Kwa hiyo kama kuna ulazima wa kuongeza mbunge wa viti maalum NEC ndio wanamtangaza kutoka pale list ilipoishia.

Mfano alipochaguliwa Rebeca Mngodo, yeye aliongezwa tu kutoka list ilipoishia baada ya chadema kupata fursa ya kuongeza nafasi moja ya viti maalum baada ya Saidi Arfi kushinda ubunge jimbo la mpanda kwa tiketi ya chadema.
Kwa hiyo msipotoshe jamvi, kama kuna uteuzi umefanyika sasa basi chadema hawahusiki....nec wanachagua tu kutoka katika list ambayo uchaguzi ulishafanyika tangu 2010 kwa kufuata taratibu zote za uchaguzi.
 
Back
Top Bottom