Je, mmemwelewa Joseph Butiku?

Kutotaka kumuona au kumsikia mzee Butiku ni matatizo yako binafsi, mzee Butiku hakumualika Idd Amin Dada kuivamia Tanzania ili yeye aratibu vita ya kumuadhibu nduli yule. Humtendei haki mzee Butiku. Matatizo tuliyonayo sasa hivi yamesababishwa na viongozi wenye tamaa na ulafi wanao shindwa kukusanya kodi, wanaoingia mikataba ya hovyo, wanaokumbatia ufisadi, wanaokosa ubunifu na uongozi bora. Hao ndio wanaotakiwa kulaaniwa. Kuvunja miiko ya uongozi ndicho kinacho tugharimu sasa.

Pamoja sana mkuu.

Namshangaa huyo mpumbafu kwa kumshambulia Mzee Butiku kuhusiana na vita ya Kagera. Angekuwa yeye ndiye kiongozi na nchi imevamiwa sijui angechukua hatua gani!? Hana akili kabisa. After all, Butiku alikuwa nani wakati huo wa vita? Sijui hiyo historia ameokota wapi! Ndiyo tatizo la JF uhuru uliomwagwa unaruhusu hata mabwege kuchangia mawazo yao ya kibwege.
 
Mimi siwezi kusema ni msomi aliyebobea ktk maswala ya siasa na itikadi, lakini naweza kusema tu kwamba Watanzania bado kabisa tunashindwa kufikiri matatizo tulokuwa nayo yametokana na sababu zipi badala yake tunataka njia rahisi sana na nyepesi ili mradi tunakwepa ukweli.

Binafsi sioni sababu ya kuzungumzia tena Azimio la Arusha kwani hili Azimio limeitwa hivyo kutokana na kwamba Chama CCM walifikia makubaliano hayo mjini Arusha kuendesha siasa za Ujamaa na Kujitegemea (itikadi). Kwa ujumla wake hili Azimio hatulihitaji leo hii isipokuwa vipo vifungu ambavyo vinaweza kutumika kulingana na mahitaji ya leo kitaifa na sii kiitikadi.

Hivyo kinachotakiwa leo ni kuzungumzia matatizo tulonayo leo ambayo yanatokana na Azimio la Zanzibar, hili ndio tatizo na sidhani kama dawa yake ni Azimio la Arusha..Mjadala unaotakiwa ni kuhusu Azimio la Zanzibar ambalo lilifanyika mwaka 1991 au 92 baada ya nchi kuingia ktk Ubepari na mabadiliko yake mengi yamehusu viongozi na sii kuacha Ujamaa kwani huo Ujamaa unaozungumziwa sana tuliuacha toka Mwinyi alipoingia madarakani mwaka 1985.

Ni makosa gani yalifanyika baada ya Azimio la Zanzibar ambayo yametuathiri kiuchumi na kupoteza uongozi bora ambao ulikuwa ngao ya nyenzo kubwa ya utawala bora nchini ndio maswali ya kujiuliza badala ya kulizungumzia Azimio la Arusha hali Azimio hilo lilikuwa na maswala mengi ya kiitikadi kuwa ndio dira ya Taifa, wakati leo hii itikadi haiwezi kuwa dira ya Taifa..

Na nasema hivi kwa sababu hata kubinafsisha sii itikadi ya kisiasa hata kidogo,ingawa watu wengi wanachanganya swala hili na Ujamaa.
Leo hii nchi zote duniani zinabinafsisha bila ya kujali itikadi zao kwa sababu lengo ni la kubinafsisha ni serikali kutua mzigo wa kutoa ruzuku ktk mashirika yake na badala yake itakusanya kodi na kiuchumi mara zote hatua hii imeonyesha mafanikio zaidi ya uzalishaji, utekelezaji na ongezeko la pato ktk mfuko wa Taifa.

Kwa hiyo, nadhani tuwe makini sana tunapozungumzia Azimio la Arusha kwa sababu lina maana zaidi ya kiitikadi itakayoijenga nchi yetu, kitu ambacho leo hii chini ya dunia hii ya demokrasia, Utandawazi na soko huria ni swala la kiimani (kifalsafa) nakuna mitazamo tofauti ambayo huwakilishwa na vyama vya kisiasa. Na hatuwezi kujenga dira mpya ya kitaifa kwa kulipitia upya Azimio la Arusha isipokuwa ujenzi wake utatokana na muundo wa Katiba mpya ambayo itawagusa wananchi wote na wenye itikadi tofauti...

Kwa hiyo pengine Mzee wetu Butiku kauliza kwa sababu anajua sii rahisi kuyachukua machache ya Azimio la Arusha ikiwa makosa makubwa yametokana na kuzaliwa kwa Azimio la Zanzibar ambao limedai kufanya marekebisho ya Azimio la Arusha ili kuboresha zaidi hali ya iuchumi nchini, lakini kama utalisoma vizuri Azimio hilo utagundua kwamba ndilo chanzo cha Ufisadi mkubwa wa viongozi wa Taifa (grand Corruption).


Sasa ni vipi tunaweza kuudhibiti Ufisadi hasa wa viongozi wa juu hali Azimio hilo linawaruhusu viongozi wetu kuhodhi mali ali mradi wanaruhusiwa kuwa matajiri kama wanavyodai. Maana ukiwauliza viongozi wetu watakuuliza wewe tena kwani hutaki viongozi wetu wakatajirika?..Na wanafanya hivi makusudi kwa sababu hawana jibu la Ufisadi huu uliotokana na wao wataweza vipi kujibu hali wao ndio mirija!

Kwa hiyo tunapozungumzia Azimio la Arusha na mathlan tunataka kukata mirija, mimi nadhani hatuwezi kutumia njia zile zile za kukataza kofia mbili, kukataza mishahara miwili na pengine kukataza kiongozi kumiliki mali isipokuwa mimi nadhani tuhnachotakiwa ni kutazama hawa viongozi wetu wamefaidika vipi na Azimio la Zanzibar kiasi kwamba wamekuwa Mafisadi wakubwa. Na mbinu zitapatikana kutokana na kutazama fursa hizi zilizotokana na Azimio hili ili kuzidhibiti...

Majibu mengi bila shaka yapo ktk kuundwa kwa katiba Mpya, mimi naamini hoja nyingi za wananchi kikatiba ndizo zitayavuta mazuri ya Azimio la Arusha na kuacha yale ambayo hatuyahitaji. Makosa yetu hayakuwa kuliondoa Azimio la Arusha bali kuundwa kwa Azimio la Zanzibar ambalo liliondoa miiko na maadili ya viongozi wetu. Na hata kama tukiyarudisha, viongozi leo hii ni viziwi, vipofu na wagumu kuelewa dhambi ya Ufisadi ikiwa ina mafanikio kwa maisha na familia zao. Na ndio maana katiba inakataza kutoa wala kupokea rushwa lakini ndio kwanza sote tunasherehekea inapotokea mwanya.

Tukiweza kupunguza madaraka ya rais, kuondoa nafasi ya waziri mkuu na rais mwenyewe kushiriki bunge na kushika kazi zote za waziri mkuu, wabunge wote lazima wawe wakazi wa majimbo wanayogombea, Majaji, na wakuu wa taasisi zote za seriikali wapitishwe na kamati ya bunge, mahakama huru, TAKUKURU huru, wakuu wa mikoa na wilaya wachaguliwe na wananchi, Halmashauri za miji lazima zipate ujuzi wa kuendesha Halmashauri ktk maendeleo na sii kuendesha siasa..Na juu ya yote haya - NO ONE is above the LAW!

Kama tutaweza kusafisha juu nina hakika huku chini itakuwa rahisi zaidi kufuta kabisa Ufisadi na itabakia labda wizi kwa wale wenye asili wa kuiba maana hawa hatuwezi kuwabadilisha lakini muhimu ni lazima tuwe na regulations ambazo zinapiga vita Ufisadi. Iwe haramu kupokea au kutoa rushwa kwa kupambana navyo kivitendo pamoja na kwamba hii itakuwa mtihani mkubwa lakini kama wananchi watawezeshwa kuwashtaki watoza rushwa, taratibu tutakuja kuzoea na kuwa Wazalendo WAUKWELI..

Hatuhilihitaji Azimio la Arusha ila tunahitaji kulitazama Azimio la Zanzibar na kurekebisha makosa mengi yaliyofanywa na CCM chini ya mh.Mwinyi..
 
Back
Top Bottom