Elections 2010 Je mfano huu wa Mwalimu J. K. Nyerere umekuwa mfano halisi?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,347
6,471
Plato, Myunani wa kale, alipendekeza kuwa mafilosofa ndio wanaofaa kuwa watawala wan chi, maana wana sifa mbili muhimu: kwanza, wana uwezo wa kutawala, na pili, hawapendi kutawala. Kwa hiyo, Jamhuri ya Plato itakuwa na sheria ya kuwalazimisha mafilosofa kutawala kwa zamu; na mtu zamu yake ya kutawala ikisha, atafurahi sana kurudiashughuli zake za falsafa ambazo ndizo hasa anazipenda. Lakini nchi zetu hazitawaliwi na mafilosofa wa Plato; watawala wetu ni wanasiasa wa kawaida ambao wanapenda sana kutawala, hata kama hawana uwezo wa kutawala, na ambao wako tayari hata kuhonga ili wachaguliwe kuwa watawala, na wakisha kuchaguliwa hawatoki bila kulazimishwa. Si busara kuwaachia wao wenyewe ndio wawe waamuzi wa lini waache kuwa watawala (Nyerere, 1993, p.8)
Reference
Nyerere, Julius K. (1993). Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania. Harare: Zimbabwe Publishing House

 
Ukiangalia kwa undani Kauli za baba wa taifa zilizo nyingi huwa zinamsema JK tu, jamaa hajakaa pake huyu. Na alishawahi kutamkiwa nadhani kifo cha yule mzee alikisherehekea maana urais angeusikia kwenye bomba tu, he is running on empty
 
Back
Top Bottom