Je, mbunge akifungiwa vikao vitatu. Je hahudhurii Kamati kama Kamati ya Matumizi ya Bunge zima?

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,334
988
Nimeanzisha thread nyingine kuhusu kitendo cha Dr. Faustine Ndugulile kutolew nje kwa muda wa siku tatu. Adhabu ile amepewa kwa mujibu wa kanuni ya 73(3) ya Bunge isemayo hivi: {Endapo Mbunge yeyote atatakiwa kuthibitisha ukweli wa maneno aliyoyasema na hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa, amekataa au ameshindwa kutoa uthibitisho huo, Spika anaweza kumsimamisha Mbunge huyo asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi vitano}.

Tumeshajadili hili na threa ile inaendelea kujadili hilo.

Kwenye thread hii ningependa tujadili uelewa ninaouna mimi na nyinyi mnipe reference zenu.

Hadi dakika hii kilichokuwa kimebaki ni BUnge kukaa kama Kamati ya Matumizi kujadili issue za Wizara hii ya Ardhi. Kwa uelewa wangu Kikao cha Kamati yoyote si kikao cha Bunge. Ndiyo maana kuna Kamati zingine huenda kufanyia shughuli zao hata nje ya nchi innapobidi.

Humu tulishajadili sana kwamba ili kiitwa kuwa ni Kikao cha Bunge basi lile rungu laa Bunge linalobebwa na yule askari yaani "mace" lazima liwepo yaani liko conspicuous yaani linaonekana mbele ya kila mmoja. Pia kiti cha Spika kiwe hakiko wazi "sede plena" yaani lazima kiwe kimekaliwa na mtu. Na akikikaliz lazima anakuwa na joho.

Sasa, Bunge linapojigeuza kuwa Kamati basi Kamati hiyo ni sawa na Kamati zingine. SPika anavua lile joho na lile rungu yaani "mace" inafungiwa ndani ya kabati.

Hivyo, hicho kinakuwa si kikacho cha Bunge bali ni kamati tu.

Kwa maana hiyo mbunge yeyote walau ni mwanakamati wa moja ya Kamati za Bunge. Hata asipopenda kujiunga na Kamati zingine basi walau anapaswa kuwa kwenye hii Kamati Bunge linapojigeuza kama Kamati ya Matumizi.

Hivyo Dr. Faustine Ndugulile aliyepewa adhabu ya siku tatu Kanuni haisemi kuwa hatahudhuria Kamati zozote za Bunge. Ninaelewa kutokana na udaktari wake ni mjumbe wa Kamati ya inayohusiana na Afya. Na ikibidi yumo kwenye Kamati zingine zaidi.

Kwa maana hiyo, mwenyekiti wa Kamati yake akiitisha kikao kesho basi Dr. Faustine Ndugulile atahudhuria Kamati hiyo kokote itakakoamua kukutana.

Swali langu ninalotaka mjadili ni kwamba baada ya Professa Anne Tibaijuka kumaliza kuhitimisha hoja za wabunge, kilichofuata ilikuwa ni Kikao cha Kamati ya Matumizi. Job Ndugai akavua joho la Uspika na lile rungu "mace" ikaondolewa ili uanakamati uanze.

Lakini kilichokatiza shughuli hiyo ni umeme kukatika Bungeni na hivyo Kamti ya Matumizi inaahirishwa hadi kesho.

Suala langu ni kwamba ninatofautiana na OSOKONI ambaye mmeshaona ame-comment kwamba Dr. Ndugulile haruhusiwi kuhudhuria kamati ile.

Hii ni timing tu walijua wakija kwenye kupitisha mafungu Dr. Ngugulile angewasumbua sana kwa swala la kigamboni ndio maana Ndugai akaanza kutokwa mapovu!!


Hoja ninayoleta ni kwamba ile kanuni inamkataza kuhudhuria vikao vya Bunge na wala si kamati. Isomeni kikamilifu na mnaonipinga mnipinge kwa msingi wa yaliyoandikwa kwenye Kanuni ile. Hivyo Dr. Ndugulile ana haki ya kuhudhuria Kamati ile kwa mujibu wa Kanuni.

Naomba tunapoelimishana tuchangie kwa kujikita kwa Kanuni zenyewe maana ndipo hapo tunapoweza kuziboresha kama zinatumika vibaya au kama zina mapungufu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom