Je, Matairi yako ni salama? Kama huna Uhakika soma Hapa!

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,967
10,461
Ndugu wanajamii, kuna masuala mengi yanapita bila kuwa na taarifa nayo kutokana na wingi wa majukumu tuliyo nayo. Kuna suala la usalama wa magurudumu ya vyombo vyetu vya moto (magari, pikipiki n.k.) ambayo kila kukicha yanaua ama kusababisha vilema vya maisha kutokana na ubora wake hafifu.

Kuna makala nzuri sana nimeichukua mahali, ya kuangalia usalama wa magurudumu ya gari lako, kama yanakidhi viwango vilivyowekwa na watenngenezaji ama la!
:)
Shusha hiyo attachment na uisome, kwa usalama wa chombo chako. Ni makala muhimu sana kwa wenye magari!
 
Attachments

  • Tire safety.pdf
    667.1 KB · Views: 966
IDIMI thanx for your best education as to how best we should inspect and take care of tyres of our vehicles. I just bought a used vehilcle from Japan. With your education, I inspected the date of manufacture of the tyres and astonished to know that it was 1903, meaning that it was the 19th week of the year 2003 and expired some 4 years ago! In fact, I had a route to Morogoro from Dar es salaam (200 kms) but I cancelled it for 24 hours untill I replace the tyres. THANK YOU VERY MUCH and thumb up JF.
 
Last edited by a moderator:
IDIUMI thanx for your best education as to how best we should inspect and take care of tyres of our vehicles. I just bought a used vehilcle from Japan. With your education, I inspected the date of manufacture of the tyres and astonished to know that it was 1903, meaning that it was the 19th week of the year 2003 and expired some 4 years ago! In fact, I had a route to Morogoro from Dar es salaam (200 kms) but I cancelled it for 24 hours untill I replace the tyres. THANK YOU VERY MUCH and thumb up JF.

Thanks Buddy,
Hio ndio kazi ya JF, kuelimishana.
Huenda ajali nyingi sana za magari yetu zinatokana na ubovu wa namna moja ama nyingine ya gurudumu yetu!
Waelimishe na wengine ili waepuke ajali.
 
mkuu thnkx kwa info but naona kwangu inasumbua kudownload. Naomba ka waweza zip hilo file halafu uliweke hapo nitashukuru sana boc
 
mkuu thnkx kwa info but naona kwangu inasumbua kudownload. Naomba ka waweza zip hilo file halafu uliweke hapo nitashukuru sana boc

Tayari nimeshaazip mtu wangu, we chota tu
 
Attachments

  • Tire safety.zip
    624.2 KB · Views: 154
Idimi ninakushukuru sana kwa elimu hii. Yaani nina tyres zangu za Pireli nilinunua March 2006 mpya na bado natembelea, ni moja tu nillibadilisha kama miezi 5 iliyopita maana ilikatwa na chuma barabarani (same Pireli). So leo hii nikifika tu nafanya zoezi la kukagua na kesho nitakupa jibu. Ndiyo maana ninaipenda JF, you get every experience. Watu hawana ubinafsi. Again,, Big up man! Ndo na print hapa ili niweke kwenye file la magari yangu. Others, do the same. Itasaidia hata ndugu na marafiki zako ambao hawawezi access hii forum yetu, na itasaidia kupunguza majanga ya tyre burst, na impact zake.
 
My appreciation for educating us. I had no idea concerning my car tyres but now I know. I tried to inspect some used cars from Japan, you will be astonished, most of them run with expired tyres. I guess this might have also been the cause to several accidents happening in our lovely country.
 
Ndugu wanajamii, kuna masuala mengi yanapita bila kuwa na taarifa nayo kutokana na wingi wa majukumu tuliyo nayo. Kuna suala la usalama wa magurudumu ya vyombo vyetu vya moto (magari, pikipiki n.k.) ambayo kila kukicha yanaua ama kusababisha vilema vya maisha kutokana na ubora wake hafifu.

Kuna makala nzuri sana nimeichukua mahali, ya kuangalia usalama wa magurudumu ya gari lako, kama yanakidhi viwango vilivyowekwa na watenngenezaji ama la!
:)
Shusha hiyo attachment na uisome, kwa usalama wa chombo chako. Ni makala muhimu sana kwa wenye magari!

Asante sana bwana. Tunaweza kufa hivi hivi kwa kufanya ufundi tunaoujua. Nitafuata maelekezo.
 
Ahsante Idimi, kwa kutuelimisha ili tuwe makini na hii mikweche yetu.
 
Tunashukuru mzee, maana hiyo shule hata wauza ma tyres ukiwauliza zile number zina maana gani huwa hawazijui watakwmbia sema unataka size gani 265/65/R15 au ???? lakini maana yake hawajui. Nafikiri kwa shule hii ujumbe utawafikia tu kwani nikienda kununua tyre itabidi nikague number zote najua lazima watauliza zina maana gani nami nitawaeleza.
 
Ahsante Mkuu. Hii poa sana maana kweli nimeendesha gari for 10 years lakini habari hii ilikuwa kushoto kabisa.

Kwas sababu hii wakuu naomba kuuliza swali. Je ni kitu gani kinadetermine upepo wa tairi zako? Ukienda kwenye upepo unaulizwa unaweka kiasi gani. 25,30,40,etc hapa nawaachia tu waweke kiasi kinachofaa lakini ukweli sijui tairi zangu zinahitaji upepo kiasi gani .

Wakuu naomba shule kidogo hapa.
 
.....Je ni kitu gani kinadetermine upepo wa tairi zako?

Wakuu naomba shule kidogo hapa.

Ukubwa wa magurudumu ya gari lako huwa ndio unaoamua kiasi cha upepo (PSI) ambacho kinatakiwa kujazwa katika magurudumu.
Kama utakuwa imesoma vizuri makala iliyoambatanishwa katika mada hii, kuna maelezo mazuri kabisa ya namna ya kujua kiasi cha upepo cha kujaza katika magurudumu. Ipitie tena makala husika, ina jibu la swali lako
 
Ndugu wanajamii, kuna masuala mengi yanapita bila kuwa na taarifa nayo kutokana na wingi wa majukumu tuliyo nayo. Kuna suala la usalama wa magurudumu ya vyombo vyetu vya moto (magari, pikipiki n.k.) ambayo kila kukicha yanaua ama kusababisha vilema vya maisha kutokana na ubora wake hafifu.

Kuna makala nzuri sana nimeichukua mahali, ya kuangalia usalama wa magurudumu ya gari lako, kama yanakidhi viwango vilivyowekwa na watenngenezaji ama la!
:)
Shusha hiyo attachment na uisome, kwa usalama wa chombo chako. Ni makala muhimu sana kwa wenye magari!

Mkuu Idimi,

Ubarikiwe ndugu yangu, kumbe one can do some checks bila kulazimika kuwapelekea mafundi (wengi wao ni vishoka)!

Cheers
 
Du! eebwanaee
Ahsante sana mkuu kwa elimu hii ya tairi (tyre) maana hata sikujua kamwe kama hizo namba zina maana hiyo.Nikitoka tu kwa ofisi nitakagua ya kwngu nione kama yataniwezesha hata kufika nyumbani maana ni hatari tupu.
Nitaelimisha na wengine labda itasaidia kupunguza ajali zisizo za makusudi
 
<<<<<Nitaelimisha na wengine labda itasaidia kupunguza ajali zisizo za makusudi>>>>>

Ubarikiwe mama!
Na hiki ndicho tunachotakiwa kufanya, kuelimishana ili kuepukana na majanga, badala ya kutoa michango mikubwa na rambi rambi misibani ilhali tulishindwa kuzuia majanga. Kila la kheri.
 
Ndugu wanajamii, kuna masuala mengi yanapita bila kuwa na taarifa nayo kutokana na wingi wa majukumu tuliyo nayo. Kuna suala la usalama wa magurudumu ya vyombo vyetu vya moto (magari, pikipiki n.k.) ambayo kila kukicha yanaua ama kusababisha vilema vya maisha kutokana na ubora wake hafifu.

Kuna makala nzuri sana nimeichukua mahali, ya kuangalia usalama wa magurudumu ya gari lako, kama yanakidhi viwango vilivyowekwa na watenngenezaji ama la!
:)
Shusha hiyo attachment na uisome, kwa usalama wa chombo chako. Ni makala muhimu sana kwa wenye magari!

Mkuu Idimi article yako imeelezea vizuri sana hii mada ambayo niliianzisha february 2009

Mods kwa faida ya wana JF nafikiri hizi thread zingeunganishwa maana zinaongelea kitu kimoja "usalama wa tairi"

Unaweza soma zaidi Tairi-zilizokaa-muda-mrefu-zaweza-kuwa-hatari-kwa-usalama-barabarani
 
Kweli tembea JF ujifunze mengi the tyres on my car were manufactured 16th week of 2003 and to make matters worse i just bought them last November. Ngoja niwabutukie hao watu walioniuzia. This is very dangerous.

Asante ndugu kwa kutufungua macho
 
DUUUH , kwa staili hii naamini gari nyingi bongo zinatembelea rimu.
 
Back
Top Bottom