Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je madai haya ya Mohamed Said yana ukweli wowote?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mugishagwe, Oct 24, 2006.

 1. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2006
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 347
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Waislam: Hatuna cha kujifunza kutoka kwa Wakatoliki

  Mohamed Said
  IMEBIDI kuandika makala hii kutokana na makala iliyoandikwa na Kaanaeli Kaale yenye kichwa cha habari ‘Kusigana kwa matokeo baina ya shule za Kikatoliki na Kiislamu’ (Mwananchi 17 Oktoba 2006). Makala ilikuwa inaeleza yaliyojadiliwa katika mkutano ulioandaliwa na Shirika la Elimu ya Sheria Tanzania (TANLET) katika moja ya harakati za kumuenzi hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  Katika mkutano huo, ilielezwa kuwa shule za Kikatoliki ndiyo shule bora zinazoshika nafasi ‘kumi bora’ kwa kutoa matokeo mazuri ya mitihani na shule za Kiislam ndiyo ‘zinazoshika mkia’ katika kutoa matokeo mabaya.

  Ama taarifa hizo za shule za Wakatoliki kufanya vyema katika mitihani si habari mpya ni jambo linalotangazwa na vyombo vya habari kila mwaka kwa hiyo linafahamika. Ila kitu cha kushangaza ni kuwa kimezidi nini hii leo hadi ikawa ni muhimu kujadili ufanisi wa shule za Waislam hadharani kisha tukapewa ushauri kuwa Waislamu tujifunze kutoka kwa Wakatoliki ili nasi shule zetu zifanye vyema kama zao ili huu upogo wa elimu kati ya Waislam na Wakristo utoweke?

  Ushauri huu umenitia simanzi kubwa na ndiyo hasa sababu ya kuandika makala hii. Bubu alizungumza kwa uchungu wa mwanaWe ni msemo mashuri. Leo hii sisi Waislam tumekuwa watu wa kusaidiwa na Wakatoliki tuelimike! Waswahili tuna msemo ‘Akutukanae hakuchagulii tusi.’
  Laiti hao wanaotushauri wengeijua tarikh (historia) yetu wasingetamka hayo. Wamishionari wameingia nchi hii wamewakuta babu zetu pwani yote ya Afrika Mashariki na bara kulikokuwa na Uislam wakijua kusoma, kuandika na kuhesabu. Lakini haya tuyaache yanahitaji muda kueleza. Turudi kwenye mada husika.

  Awali ya yote ni kumkejeli hayati Mwalimu Julius Nyerere kwa kuadhimisha kifo chake kwa mkutano wa kuzungumza kubaki nyuma kwa Waislam katika elimu kwa kuwa, kwa kauli yake mwenyewe alisema kuwa upogo katika elimu baina ya Waislam na Wakristo uliorithiwa na serikali yake kutoka kwa Waingereza yeye ameuondosha katika kipindi cha utawala wake.

  Kauli hii aliitoa Novemba 5, 1985 katika hotuba aliyoitoa Ukumbi wa Diamond Jubille akiwaaga Wazee wa Dar es Salaam. Kabla hajastaafu urais, Mwalimu Nyerere alikuwa na haya ya kueleza kuhusu suala la elimu ya Waislam:

  “Waislam wametupa nafasi kupitia sera yetu ya elimu, kurekebisha upogo. Sasa nipo katika hali ya kufurahia kwa kuwa wakati mwingine sielewi kama mbunge mpya, waziri, au katibu mkuu katika wizara zetu za serikali, ni mwislam au mkristo au hana dini labda pale jina lake la kwanza linapotoa utambulisho. Na hata hivyo hiyo siyo njia ya kuaminika kutoa utambulisho wa dini kwa kuwa tuna wakristo wenye majina ya Kiislam, na waislam wenye majina ya Kikristo. Kuvumiliana huku ndiyo sababu; nilichofanya mimi ni kuzungumzia maadili haya kwa niaba yenu.”

  Sasa ikiwa Baba wa Taifa keshawanyanyua Waislam katika elimu na kafurahishwa na kazi yake nzuri, hawa wanaokuja leo na kusema kuwa Waislam wako nyuma wanataka kumshika uongo Mwalimu Nyerere?

  Wanataka hii leo kumsimamisha Baba wa Taifa kizimbani ajibu tuhuma za kuwakandamiza Waislam katika elimu? Kwa hakika si adabu wala ustaarabu kupinga kauli ya Mwalimu Nyerere kuwa hakusema kweli katika tatizo la elimu ya Waislam.

  Je, hawa waliokuja na hoja hii nyeti wanatambua uzito wa kauli zao hasa katika kipindi hiki ambapo Kanisa Katoliki lipo katika mchakato wa kumfanya Mwalimu Nyerere kuwa mtakatifu? Hivi hawasikii nchi nzima inavyomtukuza Mwalimu Nyerere kwa sifa za uadilifu? Majibu wanayo wenyewe. Hili la kwanza.

  Waswahili tuna msemo mwingine “Asiekujua hakuthamini.’ Historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika ni ushahidi wa juhudi za Waislam katika kujitafutia elimu. Wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika tatizo la elimu ya Waislam ndiyo chanzo cha kuanzishwa chama cha upinzani Tanganyika All Muslim National Union (AMNUT) pale akina Ramadhani Mashado Plantan na wenzake walipotoka TANU mwaka 1958, sababu kuu wakihofu Wakristo waliokuwa na elimu kuja kushika madaraka peke yao katika Tanganyika huru na kuwaweka Waislam pembeni.

  Suala hili lilileta mjadala mkubwa katika TANU. Ukipenda unaweza ukarejesha msuguano huu ndani ya TANU nyuma kidogo mwaka huo huo wa 1958 pale Sheikh Suleiman Takadir (aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU Dar es Salaam) alipomkabili Nyerere uso kwa uso na kumtuhumu kwa udini.

  Haya yalitokea baada ya Uchaguzi wa Kura Tatu pale TANU ilipoteua Wakristo kusimama kugombea nafasi za Legislative Council na kuwaweka Waislam wana TANU pembeni. Lakini katika hili palikuwa na sababu maalum za msingi. Hapa si mahali pake kuzieleza. Kipande hiki cha historia kinaogopwa sana na kwa ajili hiyo nami sitokiendeleza.

  Baada ya uhuru kupatikana mwaka 1961 Waislam kwa pumzi ile ile waliyopigania uhuru wakaingia katika harakati za kutafuta elimu. Hawakusubiri wajengewe shule na serikali. Wazee wetu waliitisha mkutano chini ya taasisi zao - Daawat Islamiyya (Mwito kwa Waislam), Jamiatul Islamiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika na Muslim Education Union kujadili nini kifanyike ili Waislam wapate elimu waliyodhulumiwa na wakoloni.

  Mipango ikatayarishwa ya kujenga shule Tanganyika nzima na mwishowe kujenga Chuo Kikuu cha kwanza kwa Waislam katika Afrika ya Mashariki. Huu ndiyo ukweli wa historia ya Waislam.

  Waislam hatuna sifa ya uvivu wala kusubiri misaada kutoka Ulaya. Ufupi wa maneno ni kuwa shule sabini zilijengwa na EAMWS na jiwe la msingi la Chuo Kikuu liliwekwa na Mwalimu Nyerere mwenyewe kwa mkono wake. Sasa la kujiuliza ni kuwa juhudi hizi zote za kutafuta elimu ziliishia wapi na nini sababu yake?
   
 2. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2006
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 347
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ufupi wa mambo ni kuwa Mwalimu Nyerere alipiga marufuku jumuia zote za Kiislam mwaka 1968 na akwaundia Waislam Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata). Historia ya TANU na uhusiano wa Mwalimu Nyerere na Waislam ina majibu ya swali hili.

  Mzee Rashid Mfaume Kawawa yu hai na ni shahidi wa yote yaliyopita katika kipindi kile. Mzee Kawawa anaweza kutoa majibu ya kitendawili hiki. Hili la pili.

  Waswahili tuna msemo mwingine ‘Chokochoko mchokonoe pweza binadamu hutamuweza.’ Imekuwa vyema leo hii, hili tatizo la elimu ya Waislam limesemwa na wasiokuwa Waislam maana laiti tungelisema Waislam tungeambiwa ‘siasa kali’ tunataka kuvuruga ‘amani na utulivu’ kama alivyosakamwa marehemu Profesa Kighoma Abdallah Ali Malima alipoionya serikali kuhusu hujuma dhidi ya Waislam kama alivyoikuta ndani ya Wizara ya Elimu.

  Mwaka 1987 Profesa Malima aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu akiwa Muislam wa kwanza kushika nafasi hiyo. Mawaziri wanane waliopita walikuwa Wakristo. Kulikuwa na malalamiko kutoka kwa Waislam kuwa wizara hiyo imegeuzwa jimbo la Wakristo hasa Wakatoliki, maana ilifika hadi padri (Simon Chiwanga) kuteuliwa na Mwalimu Julius Nyerere kuongoza wizara hiyo.

  Profesa Malima aliposhika wizara hiyo aliona upo umuhimu wa kufanya marekebisho kadhaa ili kurejesha imani ya Waislam katika wizara hiyo. Kulikuwa na tuhuma kuwa Wizara ya Elimu ilikuwa ikiwabagua vijana wa Kiislam kupata nafasi katika vyuo vya elimu ya juu na ilikuwa ikizuia kupanda vyeo kwa Waislam.

  Tatizo hili liliwekwa wazi kwa mara ya kwanza mwaka 1981 na wanafunzi wa Sheikh Malik na ndiyo ikawa sababu ya yeye kufukuzwa nchini.

  Profesa Malima alipoona dhulma ile iliyokuwapo katika wizara ile dhidi ya Waislam, aliwateua Waislam wanne kushika nafasi katika kurugenzi mbalimbali. Halikadhalika Profesa Malima alibadili mtindo uliokuwapo wa kutumia majina badala ya namba katika mitihani.

  Baada ya mabadiliko yale mwaka ule idadi ya wanafunzi Waislam walifaulu kuingia sekondari ilipanda kwa asilimia 40. Profesa Malima akaandika taarifa ya siri kwa Rais Ali Hassan Mwinyi kumtaarifu udini ulioota mizizi Wizara ya Elimu.

  Katika taarifa ile kwa rais Mwinyi, Profesa Malima alieleza kuhusu kudumazwa kwa Waislam kwa makusudi katika mgawo wa elimu. Taarifa hii ilivujishwa kwa vyombo vya habari na kwa Wakristo wengine.

  Katika watu walioipata taarifa hii ni Mwalimu Nyerere akiwa mstaafu lakini akiwa Mwenyekiti wa CCM. Hiki kisa ni kirefu inatosha tu kusema kuwa yaliyomkuta Profesa Malima kwa kutaka kutenda haki hakuna asiyeyajua. Alisimamishwa kizimbani mbele ya Kamati Kuu ya CCM kwa udini na akatolewa Wizara ya Elimu.

  Lakini kabla hatujatoka katika nukta hii ningependa kueleza kuwa katika moja ya sababu kuu iliyofanya serikali ikifungie kitabu kilichoandikwa na Profesa Hamza Mustafa Njozi Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania ni kule kuanika hadharani mbinu zinazotumika nchini kuwanyima Waislam elimu. Profesa Njozi’s aliandika:

  “…Arabia (May, 1985) wrote under the heading "A Closed Door to the Corridors of Power": ‘The majority of pupils in Tanzanian primary schools are Muslim (80 percent), a percentage which dwindles to 15-20 percent in secondary schools, sinking to a mere five percent at University level’. Almost fifteen years later, on 2 February, 1999 the Member of Parliament for Kigamboni Hon. Kitwana Kondo told the parliament that out of every 100 students who sat for the standard seven examination in Dar es Salaam in the year 1998, 71 were Muslim and 29 Christian. But out of every 100 students selected to join government secondary schools only 21 were Muslim while 79 were Christian. The MP wanted to know whether Muslim children were inherently dull (An-Nuur, February 5-11, 1999).

  Yaliyomfika Mzee Kondo nayo yanafahamika. Yapo mengine mengi yaliyofichuliwa katika kitabu hicho yanayohusu mbinu zinazotumiwa katika kuhakikisha Waislam wanabaki nyuma lakini hapa hii leo si mahali pake. Hili la tatu.

  Sasa leo Waislam tunaambiwa tukajifunze mbinu za Wakatoliki ili tuboreshe shule zetu…tukajifunze mbinu gani? Kuhodhi madaraka na nafasi katika Wizara ya Elimu na kujipendelea kwa kuwanyima Wakristo nafasi za elimu ya juu? Hili ni muhali kwa Waislam.

  Hata kama tungekuwa na uwezo nalo Uislam unakataza vyote kudhulumu na halikadhalika kukubali kudhulumiwa. Kwa Waislam elimu ni fardh jambo ambalo ni lazima litekelezwa na kwa kushindwa kufanya hivyo mja huandikiwa dhambi. Hatuhitaji kujifunza kwa yeyote yule kuhusu umuhimu wa elimu. Historia ya Waislam wa Tanganyika inapingana na dhana hiyo.

  Sasa tuzungumze kuhusu matokeo mabaya ya shule za Waislam. Kwangu mimi kwa uzoefu wangu na yale ambayo nayaelewa kuhusu historia ya Waislam wa Tanganyika hili linahitaji uchunguzi zaidi ili tudhihirishe kuwa kweli shule za Waislam zinashika mkia na za Wakatoliki ndiyo zinazotawala ‘kumi bora’ miaka nenda miaka rudi kwa haki au ndiyo hizo hizo mbinu alizotahadharisha marehemu Profesa Malima na Mzee Kondo akahoji katika Bunge na zilizosababisha kitabu cha Profesa Njozi kifungiwe na serikali ya Rais Benjamin William Mkapa?

  Katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Wajerumani walikuwa wakiwakamata Wayahudi Poland na kwingineko Ulaya wakawatoa katika nyumba zao nzuri na kuwarundika katika ghetto. Umati mkubwa wa watu waliokuwa na nafasi na heshima zao katika jamii wakajikuta wanaishi katika sehemu finyu, chafu isiyo na mifereji ya maji taka wala maji safi.

  Wajerumani wakawa wanatuhumu na kuwakashifu Wayahudi kwa uchafu. Katika hali kama hiyo vipi utategemea mtu awe msafi? Huu ndiyo mfano wetu Waislam hii leo.

  Hatuna fursa sawa kama walizonazo Wakristo, shule zetu duni na juu ya hayo bado tunahujumiwa kisha tunalaumiwa kwa kutotoa matokeo mazuri. Hili la nne ambalo ningependa lizingatiwe.

  Kwa taarifa kwa wale wasiojua ni kuwa Organisation of Islamic Conference (OIC) walitaka kujenga Chuo Kikuu Dar es Salaam. Watendaji Wakristo katika Wizara ya Elimu walipiga vita mradi huo na mwisho chuo hicho kikajengwa Mbale, Uganda.

  Darul Iman ya Saud Arabia ilitaka kujenga shule ya ufundi Kibaha na yale yaliyoikuta OIC na wao yaliwafika sawia. Huu ndiyo ukweli wa nchi yetu. Waswahili tunapokabiliwa na mtu mwingi wa mbinu na ghilba tuna msemo maarufu tunautumia kumweleza mtu huyo. Tunasema ‘Kwa nyakanga hakwishi nyimbo.’

  Kichwa kinaniuma kutaka kujua hii agenda ya kudumazwa kwa Waislam katika elimu iliyozuka ghafla bin vuu ni ya nani hasa, yao wenyewe TANLET au wametumwa na mtu? Kama wametumwa, nani huyu kawatuma na kwa maslahi ya nani?

  Agenda hii si ndiyo iliyomfanya Profesa Malima aandamwe na hatimaye kufukuzwa Wizara ya Elimu? Agenda hii si ndiyo iliyomfanya Mwalimu Nyerere amfukuze Tanzania Bara Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na kumrejesha Zanzibar chini ya ulinzi mkali na kuwaweka kizuizini wafuasi wake?

  Agenda hii si ndiyo iliyomfanya Sheikh Hussein Malik afukuzwe nchini na serikali ya Mwalimu Nyerere baada ya wanafunzi wake kupitia taasisi yao ya Waandishi wa Kiislam (Warsha) kuzungumza kuhusu tatizo la elimu ya Waislam? Hii leo kimebadilika nini? Wakati una majibu kwa kila jambo, Waislam tusubiri.
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2006
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 10,021
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Ninachojua kuwa jina la RASHIDI MFAUME KAWAWA haliendei vizuri na waislam Tanzania for obvious reasons
   
 4. K

  Kulikoni JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2006
  Joined: Aug 28, 2006
  Messages: 433
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mugishagwe,

  Sijakiona cha uongo hapo, although hiyo title ilikuwa a bit extreme.. kila jamii inacho cha kujifunza kutoka jamii nyingine. Kwa haraka haraka nadhani waislam, especially wa Tanzania, wanaweza kujifunza hiyo sense of organization iliyo kwa wakatoliki, but in their own way, kama alivyowashauri JK katika speech yake baraza la idi.

  Otherwise the rest of the article ni historical facts. While it is OK to highlight them once in a while, one is better off working to change it for the better.

  Labda swali ni "Je madai haya ya Mohamed Said yana uongo wowote?". Anaeona kuna kipengele cha uongo akiseme na kuleta data zake mbadala, objectiveliy na kistaarabu.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Oct 25, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 32,878
  Likes Received: 1,650
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu kibaya kama kuendelea kurudia uongo mara nyingi hadi ukaanza kuaminika kuwa ni ukweli!! Swali, ni je Waislamu wa Tanzania wamekandamizwa kwa makusudi na serikali yao na hivyo kuwanyima nafasi mbalimbali za uongozi, elimu n.k? Kama ni kweli serikali ya JMT lazima ijibu tuhuma hizi nzito na wale wote ambao walishiriki kwa namna yoyote ile ya ukandamizaji wa raia wa Tanzania wachukuliwe hatua za kisheria!!! Nimechoka kusikia malalamiko haya kuwa mafanikio yangu ni kwa sababu mimi ni mkristu na si kwa sababu nilisoma nikiweza maji kwenye beseni!!! na kwenda tuition n.k!! Nimechoka na kuanza kutembea na hii hisia ya hatia kuwa Wakristu wa Tanzania hawana wanachostahili kwa kazi na jasho lao isipokuwa kile ambacho wamepewa kwa sababu ya kuwakandamiza Waislamu!!!

  Iundwe tume ya Ukweli na Mapatano, iwe na Waislamu watupu, wapewe nafasi huru ya kupitia nyaraka zote muhimu za serikali, wawahoji watu wote wanaodai walinyimwa nafasi yoyote ile kwa sababu ya dini yao, wawahoji wale wote wanaotuhumiwa kukandamiza waislamu, ili ukweli ujulikane!!
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2006
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 12,127
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Dr Who,
  I am curious to know why Kawawa is not esteemed among the Muslims of Tanzania. What are the reasons?
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Oct 25, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 32,878
  Likes Received: 1,650
  Trophy Points: 280
  Jasusi, labda kwa vile yeye ni Muislamu aliyekubali kukandamiza waislamu wenzake na kukubali kukandamizwa na Mwalimu, ambaye amewakandamiza waislamu wote!!
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Oct 25, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 32,878
  Likes Received: 1,650
  Trophy Points: 280
  Huyu naye ni Muislamu jinsi alivyokandamizwa na utawala wa Mwalimu!!!

  Kutoka: Tanzania Daima

  KAZI ya kuandika vitabu kwa ajili ya kuelimisha jamii si kazi ya mzaha, bali ni kazi ambayo inahitaji umakini, usikivu na uelewa mkubwa kwa mhusika.

  “Niliamua kufanya kazi hii katika maisha yangu nikielewa wazi kuwa itakuwa na manufaa makubwa kwa taifa na kizazi kijacho kwa vile nilipata msukumo huu kutoka kwa hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere,” haya ni maneno ya mwasisi na mwandishi mkongwe wa vitabu hapa nchini, Yusuf Halimoja.

  Alizaliwa katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara Machi 19, 1934; na alijiunga na elimu ya msingi katika Shule ya Mbawala iliyoko katika Kijiji cha Namaputa mwaka 1945 na kuhitimu mwaka 1946.

  Anasema kutokana na kuwa na uwezo mkubwa darasani hakuweza kusoma darasa la kwanza, hivyo uongozi wa shule uliamua kumpitisha darasa moja hadi la tatu.

  “Sikuweza kusoma darasa la pili kwa sababu nilikuwa na uwezo mkubwa, hivyo uongozi wa shule ukaamua kunivusha darasa moja, hali hii ilinipa changamoto zaidi ya kufanya vizuri,”anasema Halimoja.

  Baada ya kuhitimu darasa la nne, alichaguliwa kujiunga na Shule ya Central School Lulindi, hiyo ikiwa ni mwaka 1947, hapo alisoma hadi darasa la sita.

  Anasema baada ya kuhitimu elimu hiyo, kiu yake haikuishia hapo, kwani mwaka 1950, alijiunga na Shule ya Sekondari ya Chidya, ambayo ilikuwa chini ya Kanisa la Anglikana.

  “Hii ni shule ya kwanza kujengwa na wakoloni kusini mwa Mto Rufiji, hivyo basi niliendelea na masomo yangu pale, huku nikichemka kwelikweli darasani…tofauti na vijana wa leo,” anasema Halimoja.

  Anasema eneo hilo la Masasi, lilisahaulika kwa kipindi kirefu kuendelezwa kutokana na sera za watawala waliokuwa katika ukanda wa pwani enzi hizo, hali iliyosababisha wanafunzi wengi kwenda kusoma mkoani Tanga.

  Anasema katika kumbukumbu zake zinaonyesha kuwa shule hiyo ilijengwa mwaka 1923 na mwaka 1925 pia ikajengwa Shule ya Sekondari ya Minaki kwa lengo la kupunguza tatizo la wanafunzi kukosa shule.

  “Niliweza kuhitimu vyema darasa la 10 na kufaulu vizuri masomo yangu kama vile Kiswahili, Jiografia, Chemistry, Historia na Kingereza, hali iliyonifanya nipate kiu zaidi ya kuendeelea na masomo pale nilipopata nafasi,” anasema Halimoja.

  Anasema mbali ya kubanwa na masomo, uongozi wa shule zote alizosoma ulikuwa na utaratibu mzuri katika suala zima la michezo, lengo kubwa likiwa kuendeleza vipaji na kudumisha udugu miongoni mwa shule za jirani.

  Anasema mwaka 1954 hadi 55 alisoma katika Shule ya Minaki kwa ajili ya kuchukua masomo ya ualimu kwa miaka mitatu, kazi ambayo anasema ilimsaidia zaidi katika maisha yake.

  “Nilijiunga na Minaki, lakini nilikuwa mtunza muda hodari (Time Keeper), kazi iliyonifanya nichaguliwe kuwa mwanafunzi mwenye nidhamu,… kitendo hicho kilinifanya niwe hadi leo na tabia ya kujali muda,” anasema Halimoja.

  Anasema akiwa Minaki alikuwa bingwa katika masomo ya dini, ambapo mwaka 1953 alikuwa wa kwanza katika somo la Uaskofu katika Wilaya ya Masasi kwa kupata alama 275 kati ya 300.

  “Hili ni daraja la kwanza kupata wakati huo…haikuwa kazi ya mchezo na mwanafunzi aliyenifuatia, jina limenitoka, alipata alama 125 tu, sasa utaona tofauti ilivyo kubwa,” anasema Halimoja.

  Anasema wakati akiwa Minaki walikuwa na gazeti lililokuwa likiitwa Maarifa na yeye aliteuliwa kuliendesha kama kiongozi mkuu na lilipata mafanikio makubwa.

  “Kazi ya uandishi wa habari ilikuwa kwenye damu yangu siku nyingi sana, sasa wakati tuko pale Minaki nakapewa uongozi mkuu wa kusimamia gazeti letu la Maarifa, na hii ilikuwa moja ya kazi nilizokuwa nikililia katika maisha yangu,” anasema Halimoja.

  Anasema wakati huo akiwa Minaki Sekondari walikuwa na wanafuzni wengi ambao leo hii wamekuwa viongozi wakuu wa nchi hii, anawataja kuwa ni pamoja na Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, John Samwel Malicela na Jaji Lewis Makame.

  “Hawa viongozi nilikuwa nao pale Minaki lakini si darasa moja, kwa vile wao walikuwa wametangulia darasa moja tu, kwa kweli wote tuliosoma hapo tumekuwa na mafanikio, ingawa si makubwa sana,” anasema Halimoja.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Oct 25, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 32,878
  Likes Received: 1,650
  Trophy Points: 280
  Anasema akiwa shuleni hapo kwa mara ya kwanza ndiyo aliweza kumuona hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akifika shuleni kwao kama mwalimu wa kawaida.

  "Nilipoonyeshwa na wenzangu kuwa yule ni Nyerere, nilishikwa na butwaa na kuwa na hamu ya kutaka kumsogelea ili aweze kunifundisha walau kidogo, lakini haikuwezekana," anasema Halimoja.

  Anasema kutokana na kushindwa kuonana na Nyerere wakati huo, hakukata tamaa kwani alipohitimu masomo yake walikutana kirahisi Ikulu kutokana na kazi yake nzuri aliyokuwa akiifanya ya kutunga vitabu vya siasa.

  Anasema mwishoni mwa mwaka 1955 alianza kazi ya ualimu rasmi, Middle School Nkomaindo, iliyojengwa mwaka 1876, wilayani Masasi, ikiwa ni shule ya kwanza kufunguliwa na mmoja wa Wazungu wa kikoloni waliokuwa eneo hilo, Mchungaji Edward Steer.

  "Niliendelea na kazi ya ualimu na baada ya muda niliteuliwa na mkuu wa wilaya ya Masasi, enzi hizo, Geofrey Thirtle, kuendesha gazeti la wilaya, lililojulikana kama ‘Masasi ya Leo'," anasema Halimoja.

  "Yule DC siwezi kumsahau kwa mambo makubwa mawili, moja likiwa ni kuhudhuria harusi yangu Agosti 1, 1959 na kuniagizia nguo kutoka Uingereza, kwa kweli hili siwezi kulisahau mpaka leo," anasema Halimoja.

  Anasema aliendelea na kazi ya ualimu hadi Desemba 13, 1961 alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mindu, iliyoko wilayani Tunduma, mkoani Ruvuma, lakini alikaa hadi 1963 aliporudishwa tena Masasi.

  Anasema mwaka uliofuata alikuwa Mtanzania wa kwanza kupelekwa nje na serikali kwa ajili ya kuchukua mafunzo ya uandishi wa vitabu, uchapishaji na usambazaji wa vitabu vya shule za msingi, sekondari na vyuo.

  Anasema mafunzo hayo aliyapata katika Chuo Kikuu cha London, Uingereza hali iliyomsaidia kuandika vitabu vingi vya siasa ambavyo vilitumika kufundishia somo hilo.

  Mwaka uliofuata alirudi nchini na kuteuliwa tena kuwa mkuu wa shule za Lukuledi na Migongo, ambazo ziliunganishwa kutokana na sera za wakati huo za Wizara ya Elimu.

  "Mbali ya kuwa mwalimu mkuu pia nilikuwa mtaalamu wa nyimbo za kwaya, nakumbuka kwaya yetu ilikuwa na waimbaji wanne tu, iliweza kutumbiza wakati wa ujio wa viongozi wa kitaifa, kama vile Nyerere na Aman Abeid Karume walipotembelea shule yetu," anasema Halimoja.

  Mwaka 1968 alihamishiwa katika Shule ya Mandawa, Nachingwea, ambako alikaa kwa miezi sita tu. Anasema baada ya kutangazwa kwa Azimio la Arusha na serikali kutaka wataalamu wa fani mbalimbali, hakusita kuchukua hatua hizo.

  Anasema mwaka huo, aliteuliwa kuwa ofisa wa kwanza (mzawa) katika Wizara ya Elimu kushughulikia masuala ya utamaduni na siasa.

  Anasema yeye ndiye mwasisi wa Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI). Kilianzishwa na Wazungu, kilikuwa na tawi moja tu mkoani Dar es Salaam.

  Anasema wakati huo Wazungu walikuwa na mpango wa kupunguza Waafrika wasizaane sana ili kukitokea matatizo yakiwemo ya vita waweze kushinda kirahisi.
  "Wengi wetu hawakujua, huko kwao wao wapo wengi au wachache, sasa wao walikuwa na lengo la kufanya sisi Waafrika tusiendelee kuzaana ili kukitokea tatizo watushinde kirahisi," anasema Halimoja.

  Anasema mwaka 1970 aliteuliwa kuwa Ofisa Habari na Elimu wa kwanza UMATI, cheo ambacho kilikuwa kikishikiliwa na Wazungu kwa muda mrefu.

  Anasema mwaka 1972 alifanya kazi moja kubwa ya kuanza kufungua matawi ya UMATI katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Dodoma, Shinyanga, Arusha, Tabora, Singida, Kilimanjaro, Tanga na Nzenga.

  "Nikiwa UMATI nilishughulika zaidi na masuala ya elimu, ustawi wa jamii, utamaduni, siasa na elimu ya uraia, haya ndiyo mambo ambayo niliona yanafaa kuyafanya katika jamii yetu ya Kitanzania," anasema Halimoja.

  Anasema mwaka 1970 alipelekwa nchini Iran chini ya uongozi wa UMATI kwa ajili ya kupata masomo juu ya uendeshaji wa vyama ambapo mwishoni mwa mwaka huohuo, alipelekwa tena nchini Ghana kwa ajili ya kupata kozi ya mahusiano mema na watu.

  Baada ya kurejea, Halimoja hakuweza kukaa nchini, kwani alipelekwa nchini Uingereza kwa ajili ya kupata mafunzo ya Utangazaji wa Radio, ambapo alisoma kwa miaka miwili.

  Mwaka 1973 serikali ikamua kumwajiri kama Ofisa Habari wa kwanza katika Wizara ya Elimu na Utamaduni, na kumpeleka moja kwa moja Radio Tanzania kwa ajili ya kuendesha vipindi vya historia na utamduni hadi mwaka 1976.

  "Baada ya hapo niliamua kuacha kazi hiyo na kugeukia kazi ya uandishi wa vitabu, zaidi kwa vile niliona ni jambo la heri kuisaidia jamii na hii ni kutokana na wito wa Mwalimu Nyerere wa kufanya kazi," anasema Halimoja.

  Anasema wakati huo Mwalimu Nyerere hakutaka mzaha kabisa katika suala la elimu, hali iliyochochea yeye kuandika vitabu zaidi vya ujama na siasa.

  Anasema mwaka 1987 alichaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirika la Maendeleo la Elimu Masasi (MEFU) tawi la Dar es Salaam, wadhifa alioushika kwa muda wa miaka miwili mpaka 1999 alipoteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Shirika la Elimu tawi la Dar es Salaam tena.

  Anasema kutokana na kipaji alichojaliwa na Mungu, sasa hivi amekuwa akifundisha shule mbalimbali mkoani Dar es Salaam kwa kujitolea na kuandika makala nyingi katika magazeti mbalimbali kwa lengo la kuendeleza fani yake.

  Anasema kwa sasa anaandaa maonyesha makubwa kuhusu elimu ya uraia, kwa wanafunzi wa shule zote za Mkoa wa Dar es Salaam.

  "Nawaomba wafadhili wajitokeza kunisaidia suala hili muhimu kwani ni la kitaifa, si langu mimi, ni letu sote, kwa vile nalenga zaidi kutoa taaluma kwa ajili ya watoto wetu," anasema Halimoja.

  Anasema hatasahau safari yake ya China mwaka 1986, ambako alikwenda kuhudhuria kozi ya chama cha waandishi wa vitabu wa China na kujionea maonyesho mbalimbali.

  "Niliweza kuona hata mwili wa mwasisi wa taifa hilo, Mao tse Tung, na ukuta mkubwa uliojengwa miaka 300 kabla ya Kristo," anasema.

  Miongoni mwa tuzo alizokwishapata ni pamoja na kuwa mshindi wa kwanza katika shindano la mchezo wa kuigiza lililoandaliwa na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD), mwaka 1964, mshindi wa kwanza tena katika shindano la kutunga insha juu ya maisha ya Rais wa zamani wa Marekani, marehemu John Kenedy.

  Mwaka 1968, mshindi wa kwanza katika kuandika historia kuhusu Chama cha TANU, lililoandaliwa na Maktaba ya Taifa, 1969 pia mshindi wa kwanza katika shindano la kuandika masuala mbalimbali kuhusu historia ya Tanzania, lililoandaliwa na gazeti la Nchi Yetu chini ya Idara ya Habari (MAELEZO); na mwaka 1970 mshindi wa kwanza wa vitabu kwa ajili ya watu wazima.

  Anasema aliamua kutumia falsafa ya Nyerere ya ‘ Nitatumia elimu yangu kwa faida ya wote', ndiyo maana aliamua kuandika vitabu vingi.

  "Nyerere aliamua kutumia elimu kuleta uhuru na kuondoa wakoloni, hivyo lazima tumuenzi," anasema.
   
 10. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2006
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 10,021
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0

  Good question
  To my understanding they viewed him in the same category with Nyerere whom they blame for systematically undermining them ..this also goes to the late Dr OMAR ALI JUMA

  Furthermore they also say that they dont want to be given preferential treatment but rather they want JUSTICE and equal treatment like any other citizen

  ...anyways this is what you get when Politicians get involved with pples religions
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Oct 25, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 32,878
  Likes Received: 1,650
  Trophy Points: 280
  DrWHO,

  Swali langu ni kuwa nataka waislamu waliotaka elimu wakanyimwa, au waliotaka kazi wakakataliwa, au waliostahili kupandishwa vyeo wakanyimwa sababu ya dini zao wajitokeze!! Haya maneno si madogo na hizi tuhuma za ukandamizaji "systematically" si ya kupuuzia!!!
   
 12. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2006
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 10,021
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0

  Mzeee Mwanakijiji

  Swali lako ni zuri japo liko abit vague kwa kwa sababu halilingani directly na statement yangu katika post yangu ya mwisho lakini on Personal level ni kuwa naamini the way Serikali ilivyotaka kulitatua hili tatizo ndio kuna walakini

  Kwa sababu walikataa KU ACKNOWLEDGE kuwa kuna TATIZO na waislam hwakuwa na matatizo na WAKRISTO bali ugomvi wao ulikuwa na Serikali kama ambavyo hii direct quote toka kwenye kitabu cha HAMZA NJOZI page:7

  Social injustice and religious discrimination against Muslims:


  The argument in this book is that the conflict in Tanzania is not between Muslims and Christians but between Muslims and the government. The problem is neither inter-religious nor horizontal but political
  and vertical. In all political regimes, Muslims have repeatedly pointed out, with evidence, that they are being discriminated against. But before examining that evidence it is important to appreciate the magnitude
  and complexity of the problem. Although the problem is political and not religious, yet it seems to me that there is a wide perceptual gulf between how Muslims and Christians look at the problem. This religious
  polarisation has encouraged some people to draw a wrong inference: that the problem lies in the worsening of Christian-Muslim relations. Of course it is perfectly legitimate for intelligent people to come out with different interpretations from the same data. But why should there be a general correspondence between intellectual interpretation and religious affiliation? This shows that we are not dealing with a simple problem.


  UNAWEZA KUKISOMA FREE kwenye hii LINK:

  http://www.igs.net/~kassim/mwembechai/mchai-chap1.pdf  AMINI SUSIAMINI lakini waislam Bongo be it the most fanatic au ma moderates wanaamini kuwa serikali iliwakandamiza SYSTEMATICALLY na haikutaka kumsikiliza mtu mpaka MKAPA alipo kubali kuwa kulikuwa ma mapungufu na aka embark kulisort out kama msomi kwa kuunda kamati maalum ili kuwasikiliza na malalamiko yao..sasa haieleweki utawala uliopita ulishindwa nini katika hili

  http://www.igs.net/~kassim/mwembechai/mchai-chap4.pdf
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Oct 25, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 32,878
  Likes Received: 1,650
  Trophy Points: 280
  Haya nitapitia kijitabu hicho na ushahidi unaotolewa...
   
 14. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2006
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 10,021
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Basi ukimaliza tutapata nafasi ya kudiscuss Issues based on evidene

  Btw Kazi nzuri unayofanya na nadhani ingekuwa vizuri uka expand coverage yako beyond hawa wanasiasa na kuwa Radio Station Kamili

  Actually itakuwa vizuri ukampata hata huo Hamza Njozi au Mohammed Said ukapata undani zaidi au unasemaje?
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Oct 25, 2006
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 32,878
  Likes Received: 1,650
  Trophy Points: 280
  yeah nilikuwa nafikiri hilo la kumpata Njozi baada ya kusoma kijitabu hiki... kama una contacts zake ni PM basi...
   
 16. M

  Mswahili Old Acc JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2006
  Joined: Sep 27, 2006
  Messages: 654
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwanakijji
  Yusuf Halimoja sio muislam ni jina tu kama Tariq Aziz, kuhusu mzee Kawawa hata mdogo wake wa baba mmoja alimfunga kumfurahisha Nyerere.

  Madai ya maonezi unaweza hata kumuuliza Alhaji Abood Jumbe Mwinyi(rais mstaafu wa znz) atakumbia na aliandika kitabu miaka 30 ya dhoruba, na Mwl alikiona na aliombwa majibu hakuwa na majibu, kwa bahati mzee Jumbe yu hai na kawawa tena wote wako London sasa unaweza kupiga simu na kupata maoni yao.

  Ukitaka kujua majina ya walionyimwa elimu kwa uislam wao au kukosa kupandishwa vyeo kwa ajili ni waislam basi wasiliana na Professor Hamza Njozi ambaye ni head wa literature Department-Udsm unaweza kupata contact zake kwenye website ya University of Dar-es-salaam.
  pia unaweza kusoma kitabu cha Mohammed Said ambacho kimechapishwa na Minerva press-London na pia mpigie simu umuhoji yeye yuko Bandari-Tanga.

  Another credible source kuhusu madai haya ya Nyerere kuwahujumu waislam ni Mzee SYKES ambaye naye kwa bahati yuko hai.

  kumbuka akina sykes ndio walikuwa wadhamini wa Nyerere.na wana mchango mkubwa ktk harakati za uhuru.
   
 17. K

  Kimbembe Senior Member

  #17
  Oct 26, 2006
  Joined: May 14, 2006
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mswahili
  Jumbe akaandika kitabu chake kisomwe na Dunia why Mwalimu atakiwe kukujibu ? Hapa kuna walakini .Watu huandika vitabu na kuacha visomwe na sijawahi kusikia mtu unaandika kitabu na unaomba majibu . Jumbe naye kweney mkumbo wa kunyimwa haki yumo? Mbona alikuwa Rais ?na hawa woye unao wataja leo walipata Elimu wapi na chini ya Uongozi wa nani ? Hizo title zao walizo nazo mbona they never denied ama stripped ? Haya madai yana maana gani maana kila uliye mtaja ama ni Msomi wa Kiislam ama kastafu baada ya kuwa na Nyerere .Wengine ni wafanya biashara maarufu hadi sasa .Kuna uongo hapa na unaeneza udini wewe.
   
 18. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2006
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 12,127
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kimbembe,
  Good point. Huyu Jumbe mi nadhani ni mnafiki. Kwanza miaka yote aliyokuwa makamu wa Nyerere hakusema kitu. Baada tu ya kutimuliwa kazi ndipo anaandika kitabu kuwa Nyerere anawabagua waislamu? Kuna wakati huyo huyo Jumbe wenu alikwenda Marekani kwa matibabu. Njiani alipita Libya na Muammar akampa dola $300,000 za kujenga shule Zanzibar. Alipofika hapa akamwomba Balozi Bomani ampeleke dukani akanunue suti. Zilizobaki akaomba wamfungulie account. On the other hand Mwalimu, kabla ya kufariki, alisikitishwa kuona Waislamu pale Butiama wakisali chini ya mti. Alipokuwa Libya alimwomba Muammar msaada kuwajengea msikiti. Fedha zote zilifika na ukifika Butiama leo kauangalie ule msikiti na waulize wale Waislamu juu ya udini wa Mwalimu. Acheni bwana!
   
 19. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2006
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 10,021
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0


  Madai mazito hayo na nadhani ni bora tujadili issues based on evidence mfano hili suala la suti je unazo evidence zozote kuzisapti?

  Kitabu ninachokijua kiliandikwa ni PARTNERSHIP kilichoandikwa na Mzee Jumbe sasa sijui hichi ushakisoma?

  Mzee mwanakijiji nimefuarhishwa sana na upeo wako wa kutaka kujua jambo na naamini baada ya kukisoma hicho kitabu kilichoandikwa na Njozi then tunaweza kujadili yaliosemwa humo lakini constacts zake sina japo mwashili kasema ukicheki web ya UDSM unaweza mpata
   
 20. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2006
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 12,127
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  DrWho,
  I stand by my statement.