Hii article ipo kwenye Gazeti la Majira 26/11/08
Imetolewa mara ya mwisho: 26.11.2008 0003 EAT
Mwandosya apigiwa chapuo la urais
Habari Zinazoshabihiana
Sigombei 'kumzibia' Mwandosya- Mwang'onda 08.06.2007 [Soma]
Profesa Mwandosya aombwa kusaidia kuunganisha CCM 15.10.2007 [Soma]
Karume: Sifikirii kugombea urais 2010 19.07.2006 [Soma]
Na Rashid Mkwinda, Mbeya
MWENYEKITI wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amemwelezea Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, kuwa ni mtu anayefaa kuwa Rais wa Tanzania kutokana na msimamo na uwezo aliouonesha katika kila wizara aliyoongoza.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika hitimisho la ziara yake Mbeya Vijijini mjini Mbalizi juzi, Profesa Lipumba alisema uwezo aliouonesha Profesa Mwandosya, unatosha kumfanyia tathmini kwamba ni kiongozi anayefaa kuongoza nchi.
"Katika wagombea wa CCM waliojitokeza mwaka 2005, Profesa Mwandosya walau alionesha kuwa na dalili za kuwa kiongozi mzuri ... huyu ndiye angefaa kuwa Rais wa nchi yetu ni mtu makini," alisema Profesa Lipumba.
Profesa Lipumba mwaka 2005 alikuwa mmoja wa wapinzani waliosimama kugombea urais akitumia tikiti ya CUF na kuangushwa na Jakaya Kikwete, ambaye aligombea kwa tikiti ya CCM.
Aidha, Profesa Lipumba alisisitiza kauli yake ya mara kwa mara, kwamba Watanzania hawajalaaniwa na Mwenyezi Mungu, kwani wana ardhi yenye rutuba ambayo inamea kila aina ya mazao na kwamba iwapo nchi ingekuwa na viongozi wanaojali watu wake, hakuna mwananchi ambaye angekufa na njaa.
"Watanzania hatuna laana ya umasikini kutoka kwa Mwenyezi Mungu ... tukiungana na kuimarisha umoja wa kitaifa, tutajikwamua katika lindi la umasikini lililotugubika kwa zaidi ya miaka 40," alisema.
Profesa Lipumba yuko katika ziara ya siku tano mkoani hapa, ambapo amehutubia mikutano ya hadhara katika kata za Mbeya Vijijini, akisisitiza azma yake ya kuwataka wananchi waachane na CCM akidai kuwa kimekuwa kikiwalaghai wananchi kwa ahadi hewa bila utekelezaji yakinifu.
Ujio wa Mwenyekiti huyo wa CUF umetafsiriwa kuwa ni sehemu ya kukipigia debe chama hicho katika ubunge kutokana na kiti hicho kuwa wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Bw. Richard Nyaulawa, kufariki dunia Novemba 9 mwaka huu.