Je kwa hili bwana kabwe si kibaraka?

Bunge la kumi lilipoanza ccm walibadili kanuni ili kamati zile za kudumu ambazo huwa zinakuwa chini ya upinzani zisiende cdm kwa kuwa cdm ni theat kwao!katika kufanikiwa hilo kanuni zilizoiruhusu cdm kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni zilibadilishwa ile zile kamati ziende kwa mamluki.katika hili vibaraka mapesa,mzee wa zege na kabwe walipigiwa kura za vishindo na ccm!je unadhani angekuwa lissu angepigiwa kura na ccm kumbuka kuwa mabere pamoja na mustapha akunay wakati wanagomnea uspika na unaibu uspika hawakupigiwakura na ccm hata moja pia hata cuf waliipigia ccm.je kwa hili zitto si kibaraka wao?naomba mawazo yenu.

Gamba umeona tumekushtukia umeanzisha Uzi Mwingine rudi huku

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/249650-je-kwa-hili-amuoni-kama-zitto-ni-kibaraka-2.html
 
Zitto ni kiongozi lakini pia ni binadamu kama wengine. Yumkini kuna makosa ya kibinadamu ambayo atayafanya kwenye maamuzi ama vitendo. Lakini lazima tukumbuke kuwa Zitto bado ni kijana mdogo na ana mambo mengi ya kujifunza ili kuwa mwanasiasa mahiri siku za usoni. Sio sahihi kila mara kumdhania kuwa ni kibaraka kwa sababu tu misimamo anayochukua inatofautiana na misimamo ya watu wengine. Ukiangalia kwa undani hiyo ni mojawapo ya sifa za kiongozi thabiti. Kwani siyo mara zote watu wengi wanakuwa sahihi na historia inaonyesha kuwa mawazo mengi mapya na ya kimapinduzi huwa yanatokea kwenye akili za watu wachache. Mfano mzuri ni asilimia 80% ya watu waliopinga ujio wa vyama vingi kwa mujibu wa kura ya maoni iliyoendeshwa na serikali wakati ule kabla ya mabadiliko ya katiba na sheria kuruhusu vyama vingi.
 
Hivi ww kweli hamnazo,huyo lissu tangua aingie bungeni hapo kafanya nini?hapo cdm hakuna kichwa kama zitto,huyu jamaa huwa anachosema ndio anachofanya'huyo mbowe mikwara mingi kurudisha shangingi halafu kalifata kimya kimya'mbunge gani wa cdm ambae kakataa posho kwa vitendo kama sio zitto'wewe tatizo udini chadema udini uko wazi kabisa wanataka wachungaji na mapadri tu,

Kajipange upya, hoja za kihisia hapa siyo mahala pake! Kawaida watu wenye kutaka majibu rahisi (wavivu wa kufikiri) ndiyo mara nyingi hukimbilia kwenye ubaguzi wa kidini na ukanda. Umiza kichwa bana, uje na hoja za kimsingi hapa, siyo udini, hakuna anayeombea vita za kidini coz ni hatari kuliko zote, hizi husukumwa na imani, acha mchezo wako wewe.
 
Kwa kweli huna hoja katika hili. Umevuma kama debe kabisa. Kwa staili hii Magamba mnazidi kujizalilisha. Hivi utumbo kama huu unapata wapi mda wa kuuandika? Kila sentensi iko kivyake, hakuna hata kitu kimoja kinachoweza kutiririka na kingine. Pole sana, umeshindwa kabisa kujenga hoja na sasa unahaha.
 
Hivi ww kweli hamnazo,huyo lissu tangua aingie bungeni hapo kafanya nini?hapo cdm hakuna kichwa kama zitto,huyu jamaa huwa anachosema ndio anachofanya'huyo mbowe mikwara mingi kurudisha shangingi halafu kalifata kimya kimya'mbunge gani wa cdm ambae kakataa posho kwa vitendo kama sio zitto'wewe tatizo udini chadema udini uko wazi kabisa wanataka wachungaji na mapadri tu,
Zitto ni kibara wa jk, aliwasalitwenzake pale Udsm wakakamatwa enzi za the late Gervas Mkili. Alikuwa anaatumiwa na Malecela.Zitto ni mtu opportunistic sna na anapenda sna madaraka.
 
hivi ww kweli hamnazo,huyo lissu tangua aingie bungeni hapo kafanya nini?hapo cdm hakuna kichwa kama zitto,huyu jamaa huwa anachosema ndio anachofanya'huyo mbowe mikwara mingi kurudisha shangingi halafu kalifata kimya kimya'mbunge gani wa cdm ambae kakataa posho kwa vitendo kama sio zitto'wewe tatizo udini chadema udini uko wazi kabisa wanataka wachungaji na mapadri tu,

we ngongoseke! Acha ubwege, mtazamo wako usikufanye ujione uko peponi kwa sababu tu 'umesafiri upo ndani ya ndege' yaani kwakuwa zitto alikataa posho ndio kichwa? Unajua ni mambo mangapi ya chini chini anawasaliti wenzake wapinzani? Alishawahi kusema hawezi kumpinga jakaya kwakua ni muislam mwenzake, je hii unaielewa? Jiulize kwanini chadema hawamuhusishi kwenye maamuzi makubwa ya chama wakati yeye ni naibu katibu mkuu.
 
Binafsi sina shaka na uwezo wake bali nnatilia shaka uadilifu wake,ukimwona adui anamsifia sana mpiganaji wako tena mmoja tu!ni hekima kuchunguza,kwani ubora wa askari ndio ubora wa jeshi,tofauti na hapo utakuwa unafurahia mgawanyiko wa jeshi lako.
 
Walakini wa Zitto ni mkubwa kuliko ukweli wake unapoangalia ushiriki wake ndani ya CHADEMA. Rejea mwenendo wake na kauli zake wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom