Je kwa hili alaumiwe nani?

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
stude.jpg


Mwalimu Samwel Nyamsangya, wa Shule ya Msingi Saranga iliyopo Kimara Temboni, jijini Dar es Salaam, akiwafundisha wanafunzi 200 wa darasa la pili jana huku wakiwa wameketi chini kutokana na ukosefu wa madawati. Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1,080.

maoni: jE HALI HII IMEENDELEA FOR PAST 4 YEARS, SERIKALI ITAOMBA KURA KWA HALI GANI?
 
Hali kama hiyo iko Dar Es Salaam, ukienda mikoani ndiyo utachoka zaidi, Viongozi wetu kila siku wanaimba uchumi unapaa bila kujua waliobebwa kwenye uchumi huo. Binafsi naamini tatizo la madarasa na madawati halihitaji nguvu za wafadhili ila ni jambo la kuamua na kutekeleza tu lakini viongozi wetu hawalitilii maanani pengine kwa kuamini kuwa jamii ya watu wasiokuwa na elimu ndiyo jamii rahisi kwa kuendeleza utawala wao.
 
Siyo lazima kila kitu kifanywe na serikali.
Vitu kama hivi ni uvivu na kutokuwajibika kwa wazazi na walimu wa shule husika.
Angalia picha hiyo vizuri kwa nyuma utaona kuna madawati yaliyoharibika. Walimu wanapata fedha za matengenezo madogomadogo kwenye fedha za shule lakini wameshindwa kufanya matengenezo madogomadogo kwa madawati mpaka yakaharibika hivyo na kuyarundika.
Wazazi ndo wanatengeneza kamati za shule, wanashindwaje kujua matatizo ya watoto wao na kuisukuma shule iwajibike.
Hapa siyo suala dogo kama hilo unalahumu waziri, katibu mkuu na rais....
 
Yaani, yule mfanyabiashara wa soko la tandale kama sijakosea alikuwa na haki ya kumfokea yule Meya, sasa na sisi wananchi wengine sijui tunaweza kufanya hivyo kwa viongozi wetu jamani, hali ni mbaya sana,, wee temblea tu kijijini kwenu uangalie mambo yalivyo, inasikitisha kweli...watoo wanashindwa kusoma aah naona huruma,,,
 
ni upumbafu wa watz wenyewe tunashindwa kuwajibika sisi wenyewe na pia kuwawajibisha wahusika, hakika ktk EAC tutaolewa.pesa zipo, kwani hafla ya jezi ya ronaldo ikulu si ilifana. kwa nini hatuchukui hatua pesa zetu zielekezwe kwenye mambo muhimu km elimu. waacheni walimu wale mahala pao pa kazi.
 
Back
Top Bottom