Je kuvutia wawekezaji kuliko nchi nyingine ni swala la kujivunia?

The Analyst

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
464
246
Ndugu wana JF,
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nasikia na kuona viongozi wetu wakisifiwa kwa kujitahidi kuvutia wawekezaji kuliko nchi nyingine hapa Afrika. Swala linalonipa maswali ni hili hapa.... Kama huyo mwekezaji ni mfanyabiashara (ambaye siku zote lengo lake ni kukuza faida inayopatikana katika biashara au uwekezaji wake) anavutiwa na nini katika nchi ili asiende nchi nyingine?
Nimekuwa na hofu sana katika hili kwa kuwa nadhani kuwavutia kunaweza kuletwa na utaratibu mbaya kama nchi kujinyima na kuwaachia zaidi katika kutumia raslimali zilizopo. Kama ndivyo au mwanya huo upo je kuna sababu yoyote kujisifia kuwavutia wawekezaji kwa kiwango zaidi kuliko wenzetu?
 
Amani na utulivu tulio nao kwa kipindi chote tangu uhuru ndiyo sababu pekee inayofanya wawekezaji wavutike kwa wingi Tanzania. Sidhani kama hilo ni la kubezwa na mtu mwenye matashi mema na nchi yake.
 
Back
Top Bottom