je kusamehe ni lazima kurudiana?

dfreym

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
342
87
wadau, habari, kuna maswali kadhaa ambayo ningependa tujadili.........


watu hukoseana katika mahusiano, tena inafikia hatua mpaka kuachana (sababu ya makosa hayo).
kwa mfano makosa kama kufumania, matusi (kutukanwa/kutukana), kudhalilishwa, kusalitiwa na mengine meengi......

kuna baadhi ya kauli ambazo nimekuwa nikizisikia kutoka kwa baadhi ya watu (wadada kwa wakaka),

kuwa ......nimekusamehe lakini siwezi kurudiana na wewe......,

AU ......nimekusamehe lakini moyo umekataa kabisa kukuridhia tena.

nini maana ya msamaha wa kweli?

1. je ni kusahau yaliyopita/yaliyotokea na kuishi kama hakuna kitu kilichotoke (yaani mapenzi moto moto kama hamkukoseana)

2. au kusameheana ila uhusiano uvunjike, (zibaki salamu, na kujuliana hali)

3. vipi kuhusu wale wanao sema kuna makosa ya kusamehe na mengine si ya kusamehe?

4. vipi kuhusu maandiko matakatifu yanasemaje kuhusu suala la msamaha......

karibuni......
 
Mie nitazungumzia maoni yangu tu sitagusa vitabu vitakatifu. Binadamu tuna tabia tofauti unaweza kuona mkosaji mmoja kosa lake ni kubwa sana lakini mpenziwe akawa tayari kumsamehe pindi mkosaji atakapoomba samahani na penzi lao kuendelea. Mkosaji mwingine kosa lake ukilinganisha na huyu wa kwanza linaweza likawa dogo. Aliyekosewa pindi atakapoombwa samahani basi anaweza kabisa kusamehe lakini kutotaka tena kuendelea na mahusiano ya kimapenzi.

Kwa kifupi hakuna formula kwenye swala la kusamehe.
 
Mtu anaweza kukusamehe kabisa frm the heart lakini to protect their feelings and heart anaona anaweza kukuchukua afu ukamfanyia kitu kibaya tena siku zingine so to protect their feelings and emotions anaona bora akuachie..
 
Mie kwa upande wangu nikisha kufumania ntakusamehe lakini ndio kurudiana tena basi.....
 
inategemea na nature na frequency ya kosa lenyewe... all in all, ukimsamehe mtu si lazima mrudiane
 
Kusamehe, kurudiana au kutokurudana ni moyo wa ntu mwenyewe na jinsi alivyotendwa au kukosewa.

Pia kuangalia faida za kurudiana na hasara zake.
 
Back
Top Bottom