Je kuongeza eneo bahari ni kuimeza Zanzibar au kuboresha utaifa na uchumi?

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
Siku hizi sipiti sana JF kutokana na mchezo mchafu wa kuchomoa mada hasa zile zinazomhusu Jakaya Kikwete na watu wake. Leo nimepita na kukuta hili "sanga", kimbembe na hekaheka za kuongezwa kwa eneo bahari. Wazanzibari wanaona kama wanamezwa. Hii ni haki yao. Hakuna anayependa kumezwa hasa ikizingatiwa kuwa ni nchi. Wabara sasa wanaanza kuwabeza kweli kweli. Je tatizo ni nini? Je Zanzibar na Pemba kuwa visiwa ni kumaanisha kumilki bahari yote? Maana hili eneo lililoongezwa halikuwa mali ya Zanzibar bali ukanda wa kimataifa. Sasa kelele na mnakasha vya nini jamani? Kuna haja ya kusoma ili kuepuka kufanya vitu kama majuha.
 
Back
Top Bottom