Je, Kuna ulazima mwanamke abadili jina baada ya kuolewa?

...Ni lazima mke akishaolewa kutumia jina ukoo la mumewe? ...vipi huyo mke akiendelea kutumia jina hilo hata baada ya kuachika? ...mume ana mamlaka ya kumnyang'anya mtaliki wake "hatimiliki" ya kuendelea kutumia jina la ukoo (wa mume)?
 
Taabu ni pale jina hilo linapotumiwa vibaya na huyo mtalaka wako. Mi naona hakuna ubaya kuendelea kulitumia.
 
sidhani kama kuna ulazima ukiolewa kubadili jina, nadhani ni maamuzi ya mtu tu!....
 
...ni lazima mke akishaolewa kutumia jina ukoo la mumewe? ...vipi huyo mke akiendelea kutumia jina hilo hata baada ya kuachika? ...mume ana mamlaka ya kumnyang'anya mtaliki wake "hatimiliki" ya kuendelea kutumia jina la ukoo (wa mume)?
ni lazima ameishaingia ukoo wenu!:d
 
kwani hiyo system ilianzia wapi? Ikiwa Ni MRS .......... lazima isomeke ukoo wa MR au siyo wakuu. Kama sio MRS tena kuendelea kulitumia unakosea big time maana sifa hiyo hunaaaaaaaaaa.Ukishaachika unabaki na jina lako la utotoni tu .
 
Hapo umenena lakini hii oa, fukuza kesho bila talaka na mgawano wa mali na mkataba wa kutunza watoto, No ana right ya kuitwa hilo jina.
 
... sasa inakuwaje wale wengine keshaachika bado anatumia Surname ya Ex-husband, anaolewa tena bado tu kang'ang'ania Surname ya Ex- wake, mbaya zaidi hata huyo Mume mpya 'hajali'...
 
... sasa inakuwaje wale wengine keshaachika bado anatumia Surname ya Ex-husband, anaolewa tena bado tu kang'ang'ania Surname ya Ex- wake, mbaya zaidi hata huyo Mume mpya 'hajali'...

Hiyo surname inayong`ang`aniwa ni dili mzee. Ktk biblia sehemu fulani pameandikwa kuwa;itafika kipindi wanawake kadhaa watamwomba mwanaume kuwa watumie jina lake,ila wao watajitunza wenyewe. Kwa hiyo mkuu ndo imeshaanza hiyo.
 
...dah, hebu ninukulie hicho kifungu kipo kitabu gani, ngapi mpaka ngapi... nimejaribu kuperuzi na kudadisi bila mafanikio.

Inakuwaje pale mtaliki wako anapata mafanikio makubwa ya kikazi na maisha simply kwa kutumia ujiko (wa) jina la ukoo wako? halafu ukimgusa jeuri nyiiiiingi! Inauma eeh :)
 
Hakuna lolote hapo ni ukoloni wa kizamani tu huo.
Kuingia kwenye ukoo ndio nini?????
mwache mkeo atumie jina lake kama zamani.

Kwani wamelazimishwa kuchukua jina la mume? Wanawake wengine wanapenda kuitwa Mrs. fulani.
 
Hapana. Akiachika anapaswa kuacha kutumia jina la ukoo la mumewe. Nami niulize, ni sahihi binti anapozaa kabla ya ndoa kumwita mwanaye kwa jina la ukoo la baba yake (yaani baba yake mama mtoto, a.k.a babu yake mtoto)?. Watoto wengi wanaozaliwa nje ya ndoa hutumia surnames za babu zao. Kama mama mtoto anamjua aliyempachika mimba kwa nini asitumie jina la ukoo la mpachika mimba?? Ni tuswali tu lakini, nawasilisha
 
Atatumia surname yangu anapokuwa mke wangu. Anapokuwa si mke wangu hastahili kutumia surname yangu! Full stop!!!
 
Atatumia surname yangu anapokuwa mke wangu. Anapokuwa si mke wangu hastahili kutumia surname yangu! Full stop!!!

Tumeangalia upande mmoja tu wa talaka,je mmoja(hasa mume) ktk ndoa akiitwa mbele ya haki mwenza wake huhitaji haki zingine za kibinadamu,wakati mwingine huendelea kutumia jina la marehemu na vibuzi vingine kupiga madili.Hapo je utafufuka ukataze? Suala hili ni gumu kidogo,kuna wengine hasa wanawake huendelea kutumia majina yao kama anatokea ktk ukoo mnene. kikubwa ni kwamba wacha atumie maadamu hatumii vibaya.Pia asili ya kutengana kwenu ilikuwaje.

Ni wazo tu wakuu.
 
...dah, hebu ninukulie hicho kifungu kipo kitabu gani, ngapi mpaka ngapi... nimejaribu kuperuzi na kudadisi bila mafanikio.

Inakuwaje pale mtaliki wako anapata mafanikio makubwa ya kikazi na maisha simply kwa kutumia ujiko (wa) jina la ukoo wako? halafu ukimgusa jeuri nyiiiiingi! Inauma eeh :)

Mkuu Mbu za siku,ulipotelea wapi na ile 10M? Nitajitahidi nikumbe hicho kifungu ili kwa macho makavu ukisome.
 
Back
Top Bottom