Je, kuna ukweli wowote ktk hili!??

Dogo Lao

Member
Nov 2, 2011
94
38
Katika uwanja huu wa mahusiano, mapenzi na marafiki ni mgeni, lakini ktk nyanja nyingine si mgeni kivile, hivyo kabla ya yote niwaombe wadau mnipokee kwani si busara kuingia pahali bila kubisha hodi!
Direct 2 my point:
ninamchumba wangu, Natarajia kumuoa, mimi ni msambaa, yeye ni mchaga wa machame. Kila ninayemwambia suala hili ananiambia kuwa nimeingia choo cha *ke, kwani hawa jamaa wapo ki maslah zaidi kuliko 'real marriage'. Ukishakaa nao kwa mda mrefu kidogo wanakutanguliza mbele ya haki ili wabaki na mali.
Hapa ndipo ninapopata utata, but sina dhamira mbaya juu ya thread hii, only nahitaji masaada wa mawazo hasa kwa mtu mwenye kuielewa vizuri issue hii. Natumaini nimeleweka vizuri.
 
natumaini kabla ya kutaka kumuoa, umemchunguza tabia na unamjua vyema. Hilo ndo la muhimu. Ukifuata maneno ya binadamu utachanganyikiwa!
 
Mimi mwenyewe nilishawahi kusikia hiyo kitu lakini siiamini hata kidogo!Jaribu kujiuliza mwenyewe swali dogo tu.Je inawezekana katika hali ya kawaida kabila zima wakawa na tabia zinazofanana?Jaribu pia kuwauliza hao jamaa zako wakuonyeshe mmachame hata mmoja wanaemfahamu ambaye anahistoria ya kuua mume wake ili ujiridhishe.Nakushauri endelea na mchakato mkuu.
 
It is true, kwa upande wa tabia, kwakweli sikuiona kasoro. Nashukuru kwa wazo lako mkuu.
 
Mimi mwenyewe nilishawahi kusikia hiyo kitu lakini siiamini hata kidogo!Jaribu kujiuliza mwenyewe swali dogo tu.Je inawezekana katika hali ya kawaida kabila zima wakawa na tabia zinazofanana?Jaribu pia kuwauliza hao jamaa zako wakuonyeshe mmachame hata mmoja wanaemfahamu ambaye anahistoria ya kuua mume wake ili ujiridhishe.Nakushauri endelea na mchakato mkuu.

thanks mkuu, wazo lako nitalifanyia kazi. Asante sana.
 
Mkuu ebu nikuulize swali inasemekana wasambaaa wanakumywa mnazi sana,vp na wewe ni mtumiaji wa mnazi? Jibu utalopata ndo jibu la swali lako.
 
Kuna jamaa yangu mngoni kaoa mmachame na wanaishi fresh tu na huu ni mwaka wa saba. Ni maelewano yenu tu. Watu wengi wanasema hivyo kuhusu wamechame lakini hayo yalikuwa zamani zaidi. Chukua mtoto weka ndani kama unampenda naye kakupenda.
 
Kuna jamaa yangu mngoni kaoa mmachame na wanaishi fresh tu na huu ni mwaka wa saba.

Thank u mkuu ejogo kwa mfano wako hai juu ya issue hii, mchango wako waweza kuwa msaada kwa wengine pia wenye mawazo kama hayo. Thanx...!
 
Hayo ni maneno tu mkuu jichukulie jiko lako uweke ndani haraka kabla hujawaiwa na wajanja!
 
Hayo yalikuwa ni mambo ya zamani za kale na isitoshe hakuna mwanamke anaependa kuishi bila mume tena kwa kumuua mwenyewe sasa ataona raha gani? Usisikilize ya watu. Kaka songa mbele.
 
Kama unamashaka yoyote yale ni bora uachane nae, tafuta mwanamke ambaye utamuamini kwa kila kitu
asilimia mia. kwa nini kujitia mawazo bure.
 
Ni zamani sana hiyo mambo.

Lakini to be on the safe side fanya hivi
1. Jitahidi sana mtoto wa kiume umpate baadae sana mama akishapungukiwa usichana.
2. Usinunue pick-up mapema..
 
Hope unajua unachokitaka maishan mwako,jiulize huyo uliyempenda ni kwa ajili yako au kwa ajili ya washkaji wako?
Utaishi naye ww au ataishi na washkaji wako?
Ukipata majibu hope utakuwa na maamuzi juu ya huyo binti.
 
Wewe unampenda?
umechunguza tabia zake ukaona zinakufaa?
Kama anakufaa wewe oa.
mimi ninachojua ni hayo ni maneno tu ila kuwa makini maana wanawake wa kichaga ni watafutaji sana na wewe inabidi uige otherwise yatakua si mambo...
 
Ni zamani sana hiyo mambo.

Lakini to be on the safe side fanya hivi
1. Jitahidi sana mtoto wa kiume umpate baadae sana mama akishapungukiwa usichana.
2. Usinunue pick-up mapema..

Dogo lao fikiria hiki kilichoandikwa na Puppy. Ukibisha si tutajiandaa kuchimba kaburi na jeneza. Jiulize kwa nini wachaga wanaume wako tayari kuoa mwanamke mchaka kutoka sehemu yoyote ile lakini sio mmachame. Hao wamachame hawaolewi na wachanga toka maeneo mengine, ni wao kwa wao. Tatizo lao kubwa ni ile tabia yao ya kujisifia ukatili wao hadharani nadhani hiyo ndo inyaowaharibia sana huku kwa kina sisi njomba nchumari njia panda.

Ila twende mbele na kurudi nyuma, watoto wa kimachame Mungu kawapendelea sana uzuri, mweee!
 
Wewe unampenda?
umechunguza tabia zake ukaona zinakufaa?
Kama anakufaa wewe oa.
mimi ninachojua ni hayo ni maneno tu ila kuwa makini maana wanawake wa kichaga ni watafutaji sana na wewe inabidi uige otherwise yatakua si mambo...

Unaona ingawa jamaa kakupa moyo lakini ametanguliza onyo. hiyo sio dalili nzuri. Kuna mtu kakushaur kuachana na huyo manzi tafuta wa kabila lingine ili uondokane na wasiwasi moyoni na kuepuka mawazo ya muda gani nafsi yako itatangulia mbele ya haki, loooh!
 
Hope unajua unachokitaka maishan mwako,jiulize huyo uliyempenda ni kwa ajili yako au kwa ajili ya washkaji wako?
Utaishi naye ww au ataishi na washkaji wako?
Ukipata majibu hope utakuwa na maamuzi juu ya huyo binti.

kwa mfumo huu wa extended family unaweza ukajikuta wewe na mkeo na familia yako mnaishi ktk kisiwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom