Je, kuna Ukihiyo wa Sheria Katika Hukumu Kwamba IPTL Isijadiliwe Bungeni?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,023
18,563
Wengi wetu tumeshangazwa na Hukumu ya Majaji watatu wa Mahakama Kuu, Radhia Sheikh, Richard Mziray and Lugano Mwandambo, kwamba IPTL isijadiliwe Bungeni, na yale ambaye Uongozi wa Bunge umekuwa ukisema juu ya hukumu hiyo. Hii ni baada ya Wanasheria wa IPTL na Pan Africa Power, Joseph Makandege, Gabriel Mnyele na Felician Kay kufikisha pingamizi Mahakama ya Rufaa kwamba IPTL isijadiliwe Bungeni kwa sababu "kazi ya Bunge (mandate) ni kutunga sheria tu" (source IPPMedia)

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel, ametoa tamko kwamba Bunge ni taasisi ya Taifa inayojitegemea na haiwezi kuingiliwa katika utendaji wake na mahakama yeyote ya kisheria!

Haya ni mambo mazito na makubwa sana kisheria. Na inawezekana kabisa aidha Waheshimiwa Majaji au Mkurugenzi wa Mambo ya Bunge wakawa wana ukihiyo wa sheria hapa.

Na ikumbukwe kwamba, huko nyuma tumewasikia Spika na Wenyeviti wa Bunge wakiwazuia wabunge kuchangia Bungeni juu ya jambo ambalo "tayari liko mahakamani". Sasa swali jingine hapa ni kwamba ni kwa nini leo tunaambiwa hakuna Mahakama inayoweza kuzuia Bunge kufanya kazi zake? Je, huu ni udhihirisho kwmba BUnge letu linaendeshwa na upepo wa kisiasa badala ya kisheria?


IPPMedia extracts:

  • The High Court granted the injunction yesterday after being satisfied with arguments in the application by Independent Power Tanzania Limited (IPTL) and its subsidiary, Pan African Power, which was filed under the certificate of urgency No. 51/2014.

  • The application, filed by IPTL counsel Joseph Makandege, Gabriel Mnyele and Felician Kay and heard by a panel of three judges – Radhia Sheikh, Richard Mziray and Lugano Mwandambo, argued that the court should bar the National Assembly from deliberating on the Tegeta Escrow Account report prepared by the Controller and Auditor General's Office since the House's only mandate was lawmaking.

  • John Joel, Director of Parliamentary Affairs in the National Assembly, said the National Assembly was an independent arm of the State just like the Judiciary and its activities cannot be interfered with by any court of law.

  • Singida East legislator Tundu Lissu, a lawyer, said he was "astonished" with the High Court ruling "because it is a decision that interferes with the National Assembly's autonomy and independence".

  • National Assembly Speaker Anne Makinda was emphatic that no one could bar the lawmaking body from performing its constitutional duties, assuring parliamentarians that the eagerly awaited debate on the Tegeta Escrow Account saga would begin today and continue for three consecutive days.

 
hakuna ukihiyo wowote mzee, ila KUNA MAPESA, hiyo ndio picha halisi ya judiciary ya Tanzania, wanapenda sana hela, hivyo hapo wameshakula bilioni kadhaa kwa hiyo hukumu yao tu. majaji na mahakimu walarushwa sana sana. walifumbwa macho hapo.
 
hakuna ukihiyo wowote mzee, ila KUNA MAPESA, hiyo ndio picha halisi ya judiciary ya Tanzania, wanapenda sana hela, hivyo hapo wameshakula bilioni kadhaa kwa hiyo hukumu yao tu. majaji na mahakimu walarushwa sana sana. walifumbwa macho hapo.

Kama ni hivyo nchi yetu imeingiliwa na ugonjwa mbaya wa kufisha, na sasa iko mahututi bin taaban!!!
 
Hivi nyie watu mmeiona hiyo ruling kutoka huko mahakamani? ruling inasema status quo is to be maintained...
 
Nimeamini kuwa RAIS MAGUFULI ni member wa JAMIIFORUMS
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom