Je Kuna kifungu chochote kinaruhusu Spika Makinda afukuzwe?

Mzalendo80

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
2,508
1,338
Wanasheria wa JF naomba muongozo kama kuna sheria inayorushusu Spika Makinda a.k.a Mama Kiroboto kufukuzwa Uspika au kusitishwa kutokana na Tabia yake ya Kupendelea chama au kutetea chama badala ya Maslai ya Taifa letu.

Inakera sana jinsi unavyoangalia TV na kuona Mama Kiroboto akiwa Jeuri na mmbabe kana kwamba Bunge ni lake kumbe ni la watanzania yeye amepewa dhamana ya kulisimamia kwa maslai ya Taifa na Watanzania.

Naona Kuna haja ya kuandamana hadi Bungeni na kumtoa Mama kiroboto kwa nguvu kuwa hatufurahii ujinga au ubabe na ujeuri wake dhidi ya watanzania.

Amechagualiwa kutetea Katiba ya nchi na sio Mafisadi wa chama chake, Inakera na inauma pale mambo muhimu ya taifa yanvyoamuliwa kishogashoga na Wahuni wa CCM kwa maslai ya Chama chao sio Taifa.

Naomba Muongozo wa Sheria washeria wa JF kama kuna kipengele chochote cha kutokuwa na Imani na Spika.

Kwa style hii ya Bunge letu la sasa na majibizano ya waheshimiwa nadhani hatuna haja ya kuwa nalo maana hata sielewi wanaongea kwa ajili ya nani watanzania au vyama vyao na familia zao like today noon sijaelewa kabisa very shame to our MPS

mkuu nakupa big up bunge limekuwa la hovyo yan wa2 utafikili wapo soko mjinga kila mtu makelele na yule mama anayaanzisha makelele cjui ajiamini

Wanatia kichefuchefu,utadhani watoto wa chekechea.Hasa wale wa chama cha wenye magamba.......Eti spika aliposema mswaada wa kutafuta maoni kuhusu uundwaji wa katiba aliposema kwamba utarudishwa kwa wananchi wakaanza kushangilia ccm,ccm,......m.Nilikumbuka hadithi moja ambayo mjomba wangu alinisimulia kwamba kipindi kifupi baada ya kupata uhuru Mwl J.K.N alienda UN kuhudhuria kikao.Alikuwa na msaidizi wake wa karibu (.....),Kwa sababu yule J.K.N alikuwa mjanja na lugha inapanda,alimtumia yule kiongozi kama kiwakilishi cha watanganyika walivyokuwa wajinga na umoja wa mataifa unatakiwa kumsaidia ili kuondoa ujinga katika nchi yake.
Ishu ilikuwa hivi,kabla ya mkutano nyerere alimwambia kwamba,tukiwa kwenye mkutano nikikushika bega we cheka sana.Kweli bwana,walipoingia kwenye mkutano,nyerere akasema kuwa nchi yangu ina wajinga wengi mno mpaka nashindwa hata kupata watu wa kunisaidia,J.K akamshika bega yule nanihii,akacheka sana...Jamaa wa UN wakaelewa kweli nchi hiyo ina vilaza kama hiyo ndio afadhari je walioachwa itakuwaje.Kwa mfano huo niliona ccm hawana akili kwa sababu mswaada wameuunga mkono wao halafu wanashangilia kurudishwa kwa umma kama sio ukosefu wa akili ni nini?

Wabunge wa CCM hawana uchungu na watanzania masikini wanaowakilisha na badala yake wanaendeleza ule ushabiki wao wa kijinga wa Umimi na U-CCM.

kamaumeona bunge anavo nyonga haki usingesema atakamaipo utatoleweje nahao waungahoja watasema tupigekura

mi sitoi comment kuhusu huyu mama...maana nili coment one day nilipigwa ban 3 months ...wakubwa wa humu JF wana mahaba kweli na huyu mama

Wanasheria wa JF naomba muongozo kama kuna sheria inayorushusu Spika Makinda a.k.a Mama Kiroboto kufukuzwa Uspika au kusitishwa kutokana na Tabia yake ya Ku
pendelea chama au kutetea chama badala y
a Maslai ya Taifa letu.

Inakera sana jinsi unavyoangalia TV na kuona Mama Kiroboto akiwa Jeuri na mmbabe kana kwamba Bunge ni lake kumbe ni la watanzania yeye amepewa dhamana ya kulisimamia kwa maslai ya Taifa na Watanzania.

Naona Kuna haja ya kuandamana hadi Bungeni na kumtoa Mama kiroboto kwa nguvu kuwa hatufurahii ujinga au ubabe na ujeuri wake dhidi ya watanzania.

Amechagualiwa kutetea Katiba ya nchi na sio Mafisadi wa chama chake, Inakera na inauma pale mambo muhimu ya taifa yanvyoamuliwa kishogashoga na Wahuni wa CCM kwa maslai ya Chama chao sio Taifa.

Naomba Muongozo wa Sheria washeria wa JF kama kuna kipengele chochote cha kutokuwa na Imani na Spika.

Mkuu nadhani ktk heading neno ''kifingu'' unamaanisha ''kifungu''.Ni hilo tu,napisha nzengo ishambulie jukwaa.

Ipo haja ya kuandaa maandamano nchi nzima kumkataa Spika! hata kama sheria haipo tunaandamana tu mpaka watakapoamua kumbadilisha wenyewe!

She has to go! la sivyo atatuharibia nchi huyu. Matokeo ya anayoyapitisha sasa hivi tutakuja yajutia hapo baadae na watoto wetu watatucheka kama sio kutuchapa viboko kuwa tulikuwa wapi wakati haya yanatendeka?

Nafikiri focus ni kuandamana dodoma jengo la bunge na kudai matakwa yetu kwamba huyu mama afukuzwe na atumtambui kama kiongozi wa bunge. Hivi ndivyo vichekesho vya kikwete siku zote anataka watu wazembe kama yeye. Kuteteana kila siku na kuwanyima haki watanzania. Hivi dodoma cc na kikwete wanafanya nini tena?

Mimi naona sisi watanzania ndo tuna uchungu na nchi na sisi tunao wajibu wa kuilinda nchi yetu..adui wa nchi si lazima atoke nje, hata wa ndani ni ADUI, sasa tumtangaze mama huyu adui namba 4 wa taifa letu baada ya ujinga,maradhi na umasikini

napendekeza nguvu yetu watanzania itumike dhidi ya huyu mama adui wa taifa letu,katu hatuwezi kumlea adui huyu fisadi...peoplessssssssss pooooooo.....

Sina imani na spika Makinda,kwa kuwa ameonekana kukipendelea chama chake cha ccm hata kwa mambo ambayo hayana maslahi kwa umma,,leo wamepitisha sheria inayofanya madc kuwepo kwenye uendeshaji wa mahakama zetu,sote tunajua kuwa dc ni mwakilishi wa rais ambao ni muhimili mmoja,na mahakama ni muhimili mwingine,inawezekanaje dc awepo kwenye muhimili mwingine?hakika historia itamhukumu

Kweli kwa yeyote aliyeangalia madudu ya spika,AG kama hujatokwa na machozi au moyo kukudunda,au kupandwa na hasira basi wewe si mzalendo kweli iliogopesha naunga mkono tuandamane.mpaka bi.kiroto aondoke akaendeshe kipindi chake cha daladalaaa! Hapa pamemshinda

Mmmh! Kiroboto, ila wanafanana. JF balaa kwa kufananisha, Wassira kama ...., Pinda kama ..., kwa kweli

kwa kweli bi kiroboto anakwaza. was so sad for my country today kuona maccm yanaleta siasa kwenye ustawi wa jamii leo.lakini ndo yanakuwa ya kwanza kulalamika yakirudi uraiani!

Kwa kwel huyu mama si kwamba anaharibu bunge tu bali na taifa kwa ujumla kilichobaki ni Kuandamana tu mpaka ang'atuke ndio dawa maana c amekaa ili kuwatetea mafisad.

Wanasheria wa JF naomba muongozo kama kuna sheria inayorushusu Spika Makinda a.k.a Mama Kiroboto kufukuzwa Uspika au kusitishwa kutokana na Tabia yake ya Kupendelea chama au kutetea chama badala ya Maslai ya Taifa letu.

Inakera sana jinsi unavyoangalia TV na kuona Mama Kiroboto akiwa Jeuri na mmbabe kana kwamba Bunge ni lake kumbe ni la watanzania yeye amepewa dhamana ya kulisimamia kwa maslai ya Taifa na Watanzania.

Naona Kuna haja ya kuandamana hadi Bungeni na kumtoa Mama kiroboto kwa nguvu kuwa hatufurahii ujinga au ubabe na ujeuri wake dhidi ya watanzania.

Amechagualiwa kutetea Katiba ya nchi na sio Mafisadi wa chama chake, Inakera na inauma pale mambo muhimu ya taifa yanvyoamuliwa kishogashoga na Wahuni wa CCM kwa maslai ya Chama chao sio Taifa.

Naomba Muongozo wa Sheria washeria wa JF kama kuna kipengele chochote cha kutokuwa na Imani na Spika.

Dawa yake ni hiyo avatar yako. Mara moja tu

Back
Top Bottom