Je kuna aja ya kuupigia mlima Kilimanjaro na Ngorongoro viingie kwenye maajabu 7 ya dunia?

Kakende

JF-Expert Member
Aug 18, 2012
2,741
1,231
Ndugu zangu kuna aja ya wananchi kuwa waalendo kwa nchi yao katika mambo ya msingi. Kuna nchi ambazo zimefikia hatua ya kwenda kumshitaki jirani yake iwapo anaharibu miundombinu au kukwepa kodi, wanaona kukwepa kodi ni dhambi kubwa. Wenzetu wamefikia hatua hiyo baada ya kuona kabisa kuwa kodi yake inafanya kazi kwa kupata huduma ya maji safi, umeme wa kuaminika, elimu safi na rahisi, na asikii kuna fisadi kaiba pesa za umma.

Hata katika nchi zetu masikini unaweza kuwa mzalendo hata kama huduma hazijawa nzuri sana lakini unaona kabisa kiongozi anafanya kazi kwa uhadirifu bila wizi, ukiwa na matumaini kuwa siku moja mtafika kwenye neema kama za wenzetu.

Mimi najiuliza kama kuna haja ya kupoteza muda wangu wa kutumia internet eti nipige kura Kilimanjaro na Ngorongoro vingie kwenye maajabu saba ya dunia. Hivi katika hali ya ufisadi kama huu ambao nikianza kuutaja nitakesha, watu wanaiba Twiga na kuwasafirisha pamoja kwamba wana shingo ndefu lakini bado polisi na usalama wa taifa hawakuweza kukamata waarifu. Ukiangalia TANAPA, BOT nk wamejaa watoto wa vigogo. Hali ya elimu ni mbaya, kama huna pesa jiandae mwanao afaulu akiwa hajui kusoma

Nasita kupigia kura Kilimanjaro na Serengeti, nina wasiwasi kama watalii wakiongezeka na mimi mwananchi wa kawaida nitafaidika au zitaishia kwa wenye nchi kula kuku, kuendesha magari ya kifahari na kusafiri kila siku kwenda ulaya kutanua. Inawezekana na mimi nikafaidika?
 
Mawazo hasi kama haya ni hatari kwa taifa la kesho, kupigia kura mlima Kilimanjaro faida yake hutoiona leo wala kesho bali kwa vizazi vijavyo. Usipo piga kura huna tofauti na yule ambaye anahujumu taifa hili kwa namna yoyote ile, wewe unakuwa kuwa nyima haki yao watoto wa taifa lijalo hali wao mafisadi wamekuhujumu wewe moja kwa moja.

Tuwe wazalendo na kupenda nchi yetu kama tunataka Tanzania bora miaka ijayo. Mabadiliko hayaji kama mvua, huja kwa namna na kunyata tokana na juhudi za wananchi wenyewe!
 
Mawazo hasi kama haya ni hatari kwa taifa la kesho, kupigia kura mlima Kilimanjaro faida yake hutoiona leo wala kesho bali kwa vizazi vijavyo. Usipo piga kura huna tofauti na yule ambaye anahujumu taifa hili kwa namna yoyote ile, wewe unakuwa kuwa nyima haki yao watoto wa taifa lijalo hali wao mafisadi wamekuhujumu wewe moja kwa moja.

Tuwe wazalendo na kupenda nchi yetu kama tunataka Tanzania bora miaka ijayo. Mabadiliko hayaji kama mvua, huja kwa namna na kunyata tokana na juhudi za wananchi wenyewe!

Bado nina wasiwasi, nitapiga kura ufisadi ukiisha
 
mimi nafikiri hiyo soo maajabu...ingekuwa vema kabisa tungeachana na ml.kilimanjaro...hivi unajua kwamba tanzania ndo nchi ya kwanza duniani ambayo watoto wanafaulu mtihani darasa la saba wakati hawajui kusoma wala kuandika....?
mimi naona hili ndo ajabu kubwa la dunia....!,na tungelitangaza hili.....
 
haina maana yoyote,kwani ni hata vikishinda ni sawa na kuzidi kuwatunishia wajanja wachache mifuko yao,wakiwa wanawashawishi wa2,hadi unawaonea huruma!eti onyesha uzalendo wako kwa taifa lako!kwenye ulaji unaonekana *****,hawajanishawishi kamwe,kulima tulime wote kwenye mavuno unaambiwa una wivu wa kike!
 
Hukuna sababu, maajabu ni maajabu tu haihitaji kura ili yawe maajabu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Watanzania wana mawazo hasi sana mkuu jaribu hata kuipenda nchi yako
Maendeleo yanaanza na wewe kuipenda nchi yako sasa kama wewe usipoipenda na kuanza kuponda vitu kama hivi unaonekana una akili
Ila yule anayeiba ndio anaonekana mbaya
Kuifikia nchi kama south africa achilia mbali marekani ni mwaka 3000
 
Back
Top Bottom