Je, kubisha hodi ni vibaya?

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Shuleni nilifundishwa kuwa kabla ya kuingia ofisi yeyote unatakiwa ubishe hodi, usubiri uambiwe karibu ndipo uingie ndani. Na ukiambiwa karibu na kuingia, unatakiwa usubiri uambiwe 'karibu ukae kwenye kiti'. Lakini kama hujakaribishwa au hujaambiwa ukae, nilifundishwa kwamba nisiingie na wala kukaa kabla ya kuambiwa 'kaa'. Hivi ndivyo ninavyofanya hadi leo hii.

Lakini cha ajabu ni kwamba, ofisini nyingi hapa Tanzania (hasa Dar es Salaam) ukibisha hodi huambiwi 'karibu'. Na kama ikitokea ukaambiwa 'karibu', hutaambiwa 'karibu ukae'.

Siku moja nilienda mahali na nilipofika nikabisha hodi. Hapakuwa na jibu. Nilibisha tena mara kadhaa, lakini hakuna aliyesema 'karibu'. Baadaye niimwona mfanyakazi fulani nikamwuliza kama hapakuwa na huduma yoyote kwenye ofisi ile.

Yeye akanielekeza nifungue tu mlango na kuingia na nilipofanya hivyo nilikuta mhusika akipiga soga na baadhi ya watu. Hata hakuniuliza 'anisaidie nini'. Kisha nikauliza kama mtu niliyemhitaji hayupo, nilipotaja jina lake akasema, 'una shida?' Basi ndipo nikasaidiwa. Naona tabia hii ni ya ajabu sana! Wana JF mnasemaje?
 
Mkuu hii tabia ipo sana ila sasa kuna tofauti kutoka ofisi moja kwenda nyingine ukisema uzoee hii tabia then sehemu nyingine itakuletea tabu. Mimi nakushauri endelea na hii uliyonayo tu manake ndio nzuri kuliko hiyo ya kutokubisha hodi
 
Ni ya ajabu na inatia aibu. Nafikiri ni kufilisika kwa ustaarabu wa maisha Tanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom