Je, Kikwete ni Msafi?

Kitila,

Nakubaliana na wewe hapo juu. Tumwache Lowassa aseme, katika kusema ataropoka na kuwataja wezi wenzake kibao.

JK ananisikitisha sana hasa hili suala la EPA, mimi nilitegemea watu wakamatwe mara moja na pia awape E&Y kazi nyingine ya kuchunguza BOT kuanzia miaka ya 90. Inaelekea tumeibiwa pesa nyingi sana.

Hizo pesa zinatosha kujenga daraja la Kigamboni, kutengeneza reli ya kati, kujenga hata bandari za Tanga na Mtwara.

Kwa kweli hii sasa inasikitisha sana, inaudhi mno. Wananchi tusikubali huu
wizi wa BOT upite hivi hivi, lazima JK alazimishwe kuchukua hatua.
 
miye yangu macho, so far nimeachwa njia panda, nashindwa kuelewa hawa watu hawana hata chembe ya uzalendo na nchi yao? kweli madaraka yanalevya, nilihisi kikwete ni fisadi kabla hajachaguliwa but not to this extent.
 
Kama ulifuatilia mjada uliomuhusisha Ridhiwani kupata kazi IMMA, kuna mchangia alieleza sifa za huyo Ridhiwani, kwa kutumia Vigezo vya Masha, inaonyesha kuwa Rodhiwani hastaili kupata kazi IMMA, ok, na kazi iliyoifanya IMMA kwa kuifungua Deep Green na hapo Badae kuifirisi, ni kitu ambacho hakipo katika sheria,Kwa namna hii kuna logic association katika haya mambo, lazima uwe na upeo wa kufikilia sana hapa

pili

Kwa taarifa yako, Kikwete ajafichua Ufisadi wowote na mwanzo alipoambiwa mambo ya Ufisadi alitoa kauli za kejeli, na pia hajashughulikia Mafisadi wowote zaidi ya kuwakumbatia ili nae wasimfichulie Maovu yake, huo ndo ukweli Kikwete smart hata kidogo

Nina washauri nyie watu wote makini akina Baba H na wengineo.Just ignore the kid .He is just distracting you from the discussion kutunisha pay roll yake .Hebu mwacheni kumjibu tuendelee na kujadili hoja .Msiguse huyu kila mmoja anajua kwamba ana lake jambo si kawaida .This is Kada M katika chupa mpya kama alivyo JK na kundi lake kwa jina la awamu ya nne .
 
hizo guts watu wananzo siku zote hata Mwalimu, alipokuwa rais mkuu, sasa usiseme kuwa zimanza baada ya Lowassauka, lakini tatizo ni ushahidi uko wapi, huwezi kummshambulia rais wa nchi kwa maneno ya kuokoteza, kwa sababu kesho utakapokuwa na ukweli itatuchukua time sana kukuamini, maana umekuwa ukilia wolf! Wolf! na hizi article bila sababu, rais wa jamhuri kama ni fisadi basi ufisadi wake uwekwe wazi, lakini sio maneno ya mtoto wake kuajiriwa na shirika binagfsi la sheria, hilo sio kosa,

kama Lowassa, anazo dataz basi aulizwe aziseme, lakini kabla ya hapo hatuwezi kumvunjia heshima rais wa jamhuri aliyechaguliwa na wananchi wengi kwa mujibu wa katiba, ni wajibu wa Freeman kama upinzani kuuliza kila move ya rais na serikali, lakini sio kazi yake kumsingizia rais ufisadi bila ya ushahidi au ukweli na ninajua hajafanya hivyo, pia ni wajibu wa gazetikuuuliza pia hizo moves za rais na serikali, lakini sio kuulizia uafi wake bila ya kuwa na concrete facts kama ni fisadi, hii gotcha mentality haiwezi utusaidia as a nation, Mtikila huenda mahakamani, wakat mwingine kama ushaidi upo serikali hai-act basi tuingie huko, lini tuache kurusha shutuma bila ukweli.

FMES
Ukitaja majibu ya hoja yako basi we need action sasa hivi juu ya kila tuhuma kwa aliyekuwa implicated.Kuna utawala wa sheria utumie badala ya vitume na hadithi kibao kila kukicha hapo JK atakwua msafi kama unavyo taka tuamini na hatanyooshewa kidole . Kabla hajafanya haya hutakuwa nahoja ya kumtetea Rais wa Nchi yetu . Yeye kama mtu na anayependa madaraka kwa ubinafsi ana nafasi kubwa ya kutumaliza kama anavyo endelea kufanya .Vidole atanyooshewa hadi awe mkweli na kundi lake .
 
Kitila,

Nakubaliana na wewe hapo juu. Tumwache Lowassa aseme, katika kusema ataropoka na kuwataja wezi wenzake kibao.

JK ananisikitisha sana hasa hili suala la EPA, mimi nilitegemea watu wakamatwe mara moja na pia awape E&Y kazi nyingine ya kuchunguza BOT kuanzia miaka ya 90. Inaelekea tumeibiwa pesa nyingi sana.

Hizo pesa zinatosha kujenga daraja la Kigamboni, kutengeneza reli ya kati, kujenga hata bandari za Tanga na Mtwara.

Kwa kweli hii sasa inasikitisha sana, inaudhi mno. Wananchi tusikubali huu
wizi wa BOT upite hivi hivi, lazima JK alazimishwe kuchukua hatua.

Ninavyoona sio kwamba wapinzani wanamnyamazisha Lowasa. Ukiangalia sana wanaojaribu kumnyamazisha Lowasa ni wanaccm wenyewe (hasa security detail ya presidaa mwenyewe). Inaonekana kuwa hili swala kule ikulu wameamua kuwa liishe na Lowasa kwa hiyo kuna kila effort za kutaka mambo yaishe hivihivi.

Uzuri wa Lowasa ni kuwa yeye anataka asafishwe, lakini kumbuka kuwa huwezi kumsafisha Lowasa bila kumchafua mwingine (unakumbuka issue ya Sumaye). Katika hili, naona kuna mtu atachafuka katika juhudi za kumsafisha Lowasa, so far that person ni Kikwete.
 
Nafikiri nimekosa posts za huko nyuma, kwa hiyo huenda sijapata mtiririko kamili wa linaloongelewa kuhusu Lowasa. Je Lowasa anataka asafishwe kuwa yeye hahusiki na tope zile au anataka asizibebe tope zote peke yake bali zigawanywe sawa kwa wengine wote waliohusika. Kama anataka tope zigawanywe sawa, hapo namuunga mkono, ila kama anataka "bangusule" apatikane wa kubebeshwa tope zile ili yeye binafsi awe clean, naona tutafikishana mbali.
 
..Kamati ya Mwakyembe imetoa madai kwamba Lowassa alikuwa akitoe maelekezo kwa Msabaha ambayo yalikuwa yanakiuka maamuzi ya Baraza la Mawaziri.

..Je, Lowassa alikuwa aki-act on his own?

..If not, ni nani alimpa Lowassa go-ahead au baraka za kukiuka maamuzi ya baraza la mawaziri?

..Dr.Mwakyembe alitumia "busara" kutomhoji Waziri Mkuu. Kuna uwezekano Lowassa naye angelia kwamba yeye ni bangusilo tu!!

NB:
..Majuzi Mzee Nalaila Kiula ametoa fumbo: kwamba, Baba akikaa "vibaya" kijana utaendelea kumuangalia, au utaondoka?

..Kitendo cha Kamati kutomhoji Lowassa ni sawa ni kijana aliyeondoka ili asimuone Babaye aliyekaa vibaya.

..Inaweza ikafika mahali ikabainika kwamba Baba amekuwa na tabia na mazoea kukaa "vibaya." At that time itabidi awe confronted.
 
Unajua ni kumfukuza mwenda wazimu tukiwa uchi kutegemea Kikwete, atatue matatizo yetu ya toka uhuru in two years?

Wakuu matatizo yetu tunayajua lakini msitufanye kuwa nyiniy ni wenyeji sana bongo, na wengine ni wageni, eti ni lini bongo tulikuwa better than now kimaisha mpaka kisiasa, au kisheria? Kikwete is doing just great, matatizo yapo lakini anajitahidi kwa uwezo wake, kuna mabaya na pia kuna mazuri mengi yanafanyika, ndio maana mpaka waziri mkuu wa nchi amejiuzulu kwa ripoti ya kamati ya bunge, pole pole tunasogea, Roma haikujengwa kwa siku moja.

Wakuu tunahitaji Constructive Criticism, sio majungu na chuki za binafsi!
 
..Kamati ya Mwakyembe imetoa madai kwamba Lowassa alikuwa akitoe maelekezo kwa Msabaha ambayo yalikuwa yanakiuka maamuzi ya Baraza la Mawaziri.

..Je, Lowassa alikuwa aki-act on his own?

..If not, ni nani alimpa Lowassa go-ahead au baraka za kukiuka maamuzi ya baraza la mawaziri?

..Dr.Mwakyembe alitumia "busara" kutomhoji Waziri Mkuu. Kuna uwezekano Lowassa naye angelia kwamba yeye ni bangusilo tu!!

NB:
..Majuzi Mzee Nalaila Kiula ametoa fumbo: kwamba, Baba akikaa "vibaya" kijana utaendelea kumuangalia, au utaondoka?
..Kitendo cha Kamati kutomhoji Lowassa ni sawa ni kijana aliyeondoka ili asimuone Babaye aliyekaa vibaya.

..Inaweza ikafika mahali ikabainika kwamba Baba amekuwa na tabia na mazoea kukaa "vibaya." At that time itabidi awe confronted.

Mkuu huu usemi unatisha! Mimi nimetafsiri kuwa Lowassa ndiye aliyeondoka ili asiendelee kuona jinsi "baba" alivyokaa vibaya!
 
Kiwete is msafi hata kidogo. Pesa za EPA ndizo zilizomweka madarakani, hana ubavu wa kuwakamata wahusika kwani itabidi ajikamate na yeye pia.

Hamuoni kwamba ni vichekesho na mchezo wa kuigiza?. Wezi wanajulikana lakini hakuna hatua ya maana iliyochukuliwa.
Hata huo uchunguzi kufanyika ni badala ya pressure toka kwa mabalozi wa nje na wahisani, lakini Jakaya na serikali yake walishakataa kwamba hakuna ufisadi kama wapinzani walivyokuwa wakidai.
Mwizi wa kuku akishikwa ni kifo na kama akipona kifo basi polisi watampiga na kumtupa lupango. Lakini hawa wezi hatari wako mitaani na wanabembelezwa kurudisha pesa.

JK ni msanii na ni hatari kuliko Mkapa.
 
Ni nani anayeweza kujitangaza kuwa yeye ni msafi kati yetu humu ndani ya nyumba?
Kama wewe ni msafi kabisa na unajiamini kuwa huna doa hata moja jitokeze...
Nani msafi...Kibali au M7? Nyerere au Obote au Field Marshall Amin Dadaa? Moi ni msafi au Kenyatta? Nani msafi Mkapa au Kikwete?
Je Mbowe ni msafi?Sumaye naye?....mandhani nimetoka kwenye mada?..Hata kidogo.
Humu ndani kuna watu kila aina....tunaweza kuasema kuwa sisi wote ni wasafi kama malaika?

Katika historia ya nchi hii hakuna wakati wowowte ninaoweza kukumbuka ambapo tume iliyoteuliwa na bunge au Rais ikatoa report yake hadharani na kusababisha kizaazaa hadi kujiuzulu kwa PM na baadhi ya mawaziri.Uwazi wa jinsi hii haukuwepo tangu nchi hii kupata uhuru.

Tume inayochunguza BOT imeteuliwa na Jk na matokeo yake yanasubiriwa ingawa kuna mafisadi wamerudisha mapesa.Hata katika historia ya nchi hii sijawahi kusikia mafisadi kurudisha pesa...hii ni mpya kabisa.

Sasa ubaya wa Jk unatokea wapi? Kututeulia tume ya uchunguzi ili kufahamu ukweli ni kutokuwa msafi?

Mimi naona pamoja na nia nzuri ya mwandishi kuna elememnt ya kisiasa ndani ambayo inatupeleka kumdhalilisha Rais wetu.

Je kuna makosa Rais kumteua mtu kuwa Jaji kutoka kampuni anayofanya kazi Ridhwan?Inatakiwa aogope kumteua kwa sababu tu kuna mtoto wake humo?
 
Hoja nyingine bwana, sasa kama baba anamtumia mtoto kufanya uhuni, mtoto asitajwe? Hivi kweli wewe na utimamu wote wa mawazo unaamini kuwa kampuni ya anayofanya kazi mtoto wa Rais na ambayo imehusishwa na ufisadi wa chama tawala inatoa Jaji ni jambo dogo?

Yaani huyo mfichua ufisad na mwajibishaji ndio nani? Aliwafichua lini hao mafisadi na aliwawajibisha lini? Aangalie tu akinyosha kidogo asije kuwa anaonesha kwenye kioo ambacho kinaoonyesha sura yake!

DUH! INAKUJA VILE KUMBE.HAYA MAMBO HAYO.
 
Napenda kukufahamisha kuwa mimi si mamluki, wala sina tatizo wala matatizo, sioni umuhimu wa kumuunganisha JK na mwanae, jee ukifumaniwa wewe ndio kafumaniwa mwanao?

Ni uongo usio na mfano kumhusisha mfichuwa ufisadi na mwajibishaji wa mifisadi kuwa yeye ndie "muhusika mkubwa fisadi", huoni haya, basi hata vibaya?

wewe ni mpuuzi sana, mamluki...huna kichwa wala miguu juu ya hoja hii.... kwani uchafu wa kikwete unaonekana kwenye hilo moja tu lililotajwa?
 
Ni nani anayeweza kujitangaza kuwa yeye ni msafi kati yetu humu ndani ya nyumba?
Kama wewe ni msafi kabisa na unajiamini kuwa huna doa hata moja jitokeze...
Nani msafi...Kibali au M7? Nyerere au Obote au Field Marshall Amin Dadaa? Moi ni msafi au Kenyatta? Nani msafi Mkapa au Kikwete?
Je Mbowe ni msafi?Sumaye naye?....mandhani nimetoka kwenye mada?..Hata kidogo.
Humu ndani kuna watu kila aina....tunaweza kuasema kuwa sisi wote ni wasafi kama malaika?

Katika historia ya nchi hii hakuna wakati wowowte ninaoweza kukumbuka ambapo tume iliyoteuliwa na bunge au Rais ikatoa report yake hadharani na kusababisha kizaazaa hadi kujiuzulu kwa PM na baadhi ya mawaziri.Uwazi wa jinsi hii haukuwepo tangu nchi hii kupata uhuru.

Tume inayochunguza BOT imeteuliwa na Jk na matokeo yake yanasubiriwa ingawa kuna mafisadi wamerudisha mapesa.Hata katika historia ya nchi hii sijawahi kusikia mafisadi kurudisha pesa...hii ni mpya kabisa.

Sasa ubaya wa Jk unatokea wapi? Kututeulia tume ya uchunguzi ili kufahamu ukweli ni kutokuwa msafi?

Mimi naona pamoja na nia nzuri ya mwandishi kuna elememnt ya kisiasa ndani ambayo inatupeleka kumdhalilisha Rais wetu.

Je kuna makosa Rais kumteua mtu kuwa Jaji kutoka kampuni anayofanya kazi Ridhwan?Inatakiwa aogope kumteua kwa sababu tu kuna mtoto wake humo?

Mimi Mr Mtambo ni msafi.
 
Napenda kukufahamisha kuwa mimi si mamluki, wala sina tatizo wala matatizo, sioni umuhimu wa kumuunganisha JK na mwanae, jee ukifumaniwa wewe ndio kafumaniwa mwanao?

Ni uongo usio na mfano kumhusisha mfichuwa ufisadi na mwajibishaji wa mifisadi kuwa yeye ndie "muhusika mkubwa fisadi", huoni haya, basi hata vibaya?

Wewe ni Maluki tena ni Habithi. Usibishe.
 
hizo guts watu wananzo siku zote hata Mwalimu, alipokuwa rais mkuu, sasa usiseme kuwa zimanza baada ya Lowassauka, lakini tatizo ni ushahidi uko wapi, huwezi kummshambulia rais wa nchi kwa maneno ya kuokoteza, kwa sababu kesho utakapokuwa na ukweli itatuchukua time sana kukuamini, maana umekuwa ukilia wolf! Wolf! na hizi article bila sababu, rais wa jamhuri kama ni fisadi basi ufisadi wake uwekwe wazi, lakini sio maneno ya mtoto wake kuajiriwa na shirika binagfsi la sheria, hilo sio kosa,

kama Lowassa, anazo dataz basi aulizwe aziseme, lakini kabla ya hapo hatuwezi kumvunjia heshima rais wa jamhuri aliyechaguliwa na wananchi wengi kwa mujibu wa katiba, ni wajibu wa Freeman kama upinzani kuuliza kila move ya rais na serikali, lakini sio kazi yake kumsingizia rais ufisadi bila ya ushahidi au ukweli na ninajua hajafanya hivyo, pia ni wajibu wa gazetikuuuliza pia hizo moves za rais na serikali, lakini sio kuulizia uafi wake bila ya kuwa na concrete facts kama ni fisadi, hii gotcha mentality haiwezi utusaidia as a nation, Mtikila huenda mahakamani, wakat mwingine kama ushaidi upo serikali hai-act basi tuingie huko, lini tuache kurusha shutuma bila ukweli.

Kikwete yumo kwenye LIST OF SHAME,jina lake limetuliaaa.
Natambua kwa dhati kwamba Fisadi mmoja katika List ile yuko chini 10 bado wanadunda.

Wewe huoni kwamba tuna Home Work ya kutufanya Tisilale mpaka 2010????????

Wakati wa kuanza kumjadiri Rais kama mmoja wa mafisadi ndo huu.

Wewe kama unapinga hoja hii anzisha vita ya kuliondoa jina la Kikwete kwenye LIST OF SHAME.

Viongozi wote wa SISIEMU ikiwa ni pamoja na msuli wote wa chama wameshindwa kujenga hoja ya msingi na kuiweka mbele ya wananchi ili kuliondoa jina la MH Kikwe kwenye LIST OF SHAME. Hii ina maana wananchi tuko huru kumchambua vile tupendevyo pale Trail zote zinukazo ufisadi zimlengapo yeye MH Kikwete.

Wakati wa Rais kuwa Mtukufu naona umekwisha au umejimaliza wenyewe. Kilichobakia sasa ni kuondoa vifungu vya mabaki ya katiba ya Sir Richard Turnbull kwenye katiba yetu ili asiweko mtu ambaye yuko juu ya sheria.
 
Kikwete atavunja taifa la Tanzania vipande vipande kabla ya yeye kukimbilia Marekani kula commission zake toka kwa Sinclair. yaani yeye kaweka pamba masikioni na hasikii kabisa kilio cha wananchi wa Tanzania!

Shame on you Kikwete!
 
Habari ya Rais kuhusishwa na ufisadi haiwezi kuepukika,kama Waziri Mkuu alijiuzuru sababu ya wadogo zake,Raisi je? la kwanza kujiuliza wakati hao mabwana wanapewa uwaziri Raisi alikua hafahamu ufisadi wao? Ikumbukwe toka enzi za Nyerere kuna yaliyosemwa.

Kama hiyo haitoshi baada ya kuwachagua mafisadi na kusaini mikataba mibovu kweli Rais hakujua na kuzuia malipo mpaka kamati ya bunge iundwe au mpaka kina Slaa waseme? Hatusemi Raisi ajiuzulu hilo ni juu yake lakini alipaswa kutuambia kitu watanzania na kitu hicho kituingie masikioni na mioyoni.Kwa kweli jambo na IMMA kuhusishwa na Deep Green na kuwa na uhusiano wa karibu na Rais vina utata,bado kutoka IMMA hiyo hiyo wamechaguliwa waziri ambaye wakati wa sakata la Richmond alikua Naibu Waziri wa Wizara husika,kama hiyo haitoshi amechaguliwa mwingine kuwa Jaji,na bado mtoto wake kaajiliwa hapo,kwa nini Watanzania tusiseme?
 
Mjadala huu ni mkali kweli kweli. Kwa ujumla naona walio upande wa utetezi wanadai ushahidi wa uhakika kwamba Rais Kikwete naye ni fisadi, na wale walio upande mwingine wanadhihirisha jinsi walivyopoteza imani na Rais wetu. Kama ushahidi wa ufisadi wake upo na unatosha, litakuwa ni jambo la usaliti kwa nchi kuunyamazia ilihali tukijua mtu huyu atakuja kutuomba kura tena muda si mrefu ili aendelee kutuongoza.
Ama kwa namna nyingine, endapo mijadala hii inafika masikioni mwa Rais mwenyewe, ni vema aichukulie kwamba hii ni sehemu ya tathmini ya wananchi kuhusu uongozi wake.Basi atege masikio na asikie jinsi watu wake wanavyozidi kupoteza imani naye. Jukumu la kuirejesha imani hiyo ni lake mwenyewe.
Miaka miwili na ushee, watanzania walimwamini Kikwete sana tena sana.
Wengi walikuja kutuomba ridhaa ya kuongoza wakati ule, licha ya kutoaminiwa wengine hawakusikilizwa kabisa.
Kama naye ni fisadi,kosa ni la nani? Mtu mmoja kanambia,kiongozi mbovu ni zao la jamii mbovu, hali kadhalika kiongozi mzuri. kama kauli hiyo ina ukweli, basi tunapotathmini uongozi wa Rais na washirika wake, si vibaya tukaiangalia nchi kwa ujumla inahusikaje. Na taasisi zilizomo katika nchi zinahusikaje.
Niwakumbushe kidogo ilivyokuwa na ilivyo sasa.
hodi..nani wewe..Lipumba...sikufungulii
hodi...nani tena...Mbowe...ishia huko huko
hodi wenyewe...u nani wewe...Mrema...sikutaki
hodii...who are you...Mvungi...sitaki wageni
hodi jamani...jitambulishe...mi Mtikila...ishia huko huko
wenyewe mpo...we nani...Shayo...samahani ondoka
hodi hapa...jina lako nani...Makaidi...jaribu mlango wa pili
hodi hodi...shida gani...mii naitwa Anna, nina..samahani mama ishia huko nje
hodi hodi hodi...nani...Kyala hapa...mnanisumbua Bwana.
MARA;
Hodi jamani wenyewe
nani tena
Mimi Kikwete
Unatokea wapi
CCM
shida gani
Naomba ridhaa
Mnh,umetuletea nini
Maisha boooora kwa kila mmoja wenu
utayaletaje
Kwa ari mpya,nguvu mpya,na kasi mpya
mnh, na nini kingine
ajira milioni moja
enhe
nitaziba mpasuko na nita...
tosha Bwana, ngoja niulize kanisani wanasemaje kuhusu wewe
Hodi usharikani
muumini sema tukusaidie
kaja huyu Kikwete anaomba ridhaa
mpe, kwa maana ni chaguo la Mungu.
BAADAYE KIDOGO
mnh,ebu fungua zawadi ulizotuletea
hapa nina t-shirt L,XL na XXL, chaguo lako tu,na hizi Kofia ni za bure pia na kanga chukueni.
Chukua tu ridhaa hiyo hapo
sasa kwa kuwa ridhaa mmenipa, ngoja nifungue na vifurushi vingine
wamachinga wote tokeni mtaani mnachafua
wadau njooni twende tukague dunia tuvunje rekodi ya Vasco na Marcopolo
kamata huyo zombe
walioko magerezani poleni jamani
wagonjwa jamani poleni kwa kulala chini
uongo Mwanza hamli mapanki
Huu ukame huu jamani majaliwa
...
Hicho kibox kingine nacho fungua basi
Mara kikafunguka, loo moshi mkubwa ukatanda juu ya anga la Tanzania, Ufisadiiiii, ufisadiiii
HIVI HUU NDIO WIMBO USIO RASMI WA TAIFA KWA SASA?

Naam, walikuja kumi tukamfungulia mmoja,kama sasa zawadi zake hatuzipendi, yamkini nasi tuliomfungulia na waliotushawishi tumfungulie kwa pamoja tubebe lawama, tujifunze kusikiliza hodi vizuri. Kosa mara ya kwanza kosa, kurudia kosa ni kosa kubwa sana
 
Back
Top Bottom