Je, Kikwete anaweza kulivunja Bunge??

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Nini kitatokea ikiwa Rais Kikwete ameridhia mapendekezo ya Maboresho ya Sheria ya kusimamia mchakato wa Katiba Mpya na Serikali yake imeshaandaa marekebisho hayo na tayari kumeripotiwa jaribio la wabubge wa CCM kupinga muafaka wa Kikwete,Serikali na CHADEMA katika kikao hiki cha Bunge?
 
Ninachokliona ni usanii mtupu. Wabunge wanataka kuityumia katiba mpya kama kete ya kisiasa. Wakumbuke kwua katiba mpya ni zaidi ya siasa zao na chadema. Wananchi tunataka katibu mpya, hatujali kama atakayefanikisha ni CCM au Chadema. Tunataka katiba inayolinda maslahi yetu, hivyo wakae chonjo kwa sababu kama wakishindwa kuongoza mchakato wa kutupatia katiba tunayoitaka, tutawaweka pembeni
 
...wakihongwa tena kwa jina la POSHO hawana la kusema. Na ndicho kinachoshinikizwa kwa sasa.
 
Kikwete dhaifu hana uwezo wa kulivunja bunge. Saaizi anajaribu kutafuta namna ambayo watz wataendelea kumuonea huruma pamoja na ulegheleghe wake na ufisadi aliofanya kushirikiana na lowasa na rostamu
 
Nini kitatokea ikiwa Rais Kikwete ameridhia mapendekezo ya Maboresho ya Sheria ya kusimamia mchakato wa Katiba Mpya na Serikali yake imeshaandaa marekebisho hayo na tayari kumeripotiwa jaribio la wabubge wa CCM kupinga muafaka wa Kikwete,Serikali na CHADEMA katika kikao hiki cha Bunge?

Ndio anaweza, JK anazo karata zote Dume na Jike katika mchezo huu, anaweza akalivunjilia mbali Bunge na kuitisha uchaguzi upya na kuwawekea ngumu magamba yote yasipite kwenye uchaguzi mpya ndani ya chama chao na hapo ndipo CCM itafufuka na kuwa mwanakondoo aliyepotea karudi zizini na kwakuwa atakuwa kayamwaga magamba basi na vibaraka wao watashindwa kurudi Bungeni, kwa kufanya hilo naamini CCM bado itashinda Urais lakini itapoteza viti vingi vya ubunge na hasa vya mjini ambako waelewa ni wengi sana kuliko vijijini
 
Maamuzi ya kukubali mapendekezo ya CDM ambayo Rais ameridhia yatahitaji kupigiwa kura.Kwa sababu CCM ni wengi bungeni wakiamua kuyapinga watashinda.Na ikitokea hivyo Rais atakuwa amejivua lawama kwa CDM kwa maana yeye aliyakubali lakini bunge litakuwa limeyakataa<kwa kura>.Ndicho kitakachotokea.FULL STOP!
 
BEATRICE SHELUKINDO kajiaibisha sana na Haeleweki hua anadandia hoja kwa vile kajaariwa kulopoka basi anajiona nae ni prominent MP hapa TZ....hayo marekebisho ya katiba sidhani km ameyasoma zaidi ya kutekwa na hisia za amasaburi za uchama zaidi....JK kaeleweshwa na kaelewa wanaharakati walipinga na baadhi ya vyama vya siasa..sasa yeye anadhani RAIS JK ni wa CCM tu na sio wa jamuhuri ya muungano....Kauli aliyotoa kua wanaweza kumpigia JK kula ya kutokua na IMANI nae hivi anajua impact yake kwa TAIFA kwakua anataka kuurudisha muswada bungeni ili ujadiliwe upya? KAULI YAKE ITAMTOKEA PUANI HUYU MAMA KALEWA SIFA ANA COMPARE ISHU YA JAIRO NA JK
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom