Je Kijiji hiki ndio asili la jina?

Malunde

JF-Expert Member
Jun 16, 2010
344
88
IMG_8867.JPG IMG_8880.JPG
 
Pia kuna kijiji kipo anga za Iringa huko kinaitwa IBANYA VANU sijui nacho ni asili ya jina

Mgawariziki, nakubaliana na wewe IBANYA VANU nacho kina asili ya jina lake. Najua unafahamu kuwa mimi nauluiza juu ya Tanganyika, niambie kama unajua.
 
Pia kuna kijiji kingine kinaitwa TANGANYIKA MASATI kwa wanatoka Kilombero nakijua...lol kweli bado ni Tanganyika huko
 
Kibantu

TANGA=First/mwanzo
NYIKA= nchi/pori nk

TANGANYIKA=FIRSTCOUNTRY (NCHI YA MWANZO)
 
Oohh Kumbe ndio tafsiri ya Tanganyika!!! Nilifikiri maana yake ni:
TANGA-Angaika
NYIKA-Porini
 
Ukiwa unaenda huko, unapanda Bus pale Ngegezi unapita Matombo mpaka Kunduchi unavuka bahari unatua Makunduchi unaelekea Mchamba wima safari inaendelea .....!
 
Kibantu

TANGA=First/mwanzo
NYIKA= nchi/pori nk

TANGANYIKA=FIRSTCOUNTRY (NCHI YA MWANZO)
Utafiti mzuri wa asili ya hili jina ukifanyika karibu na ziwa Tanganyika, yamkini majibu yaweza patikana. Kuna baadhi ya wenyeji wa maeneo yaliyoko karibu na ziwa hili wanadai Tanga, na Nyika ni majina ya samaki. Aidha ukienda upande wa Congo, ziwa hili huitwa Tanganika. Na tunaposoma maandishi ya akina Henry Stanley waliotembelea maeneo ya hili ziwa kabla ya ukoloni (miaka ya 1800), wanatumia neno Tanganika. Maandishi yao ndio yalitumiwa na wakoloni kuibatiza nchi yetu jina la Tanganyika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom