Je katiba iliyopo pamoja na viraka vyake mbona serikali ya jk haiifuati?

Maarifa

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
4,568
2,911
Kutokana ma mtafuruku wa Dowans- Waziri Ngereja amabaye ni waziri mhimili alitamka kuwa serikali imeamua kulipa Deni. Kwa tafsiri ni kuwa baraza la mawaziri chini ya mkulu walisharidhia. Halafu Akaja Samuel Sitta na Mwakyembe, Good enough ni wanasheria hao. Wakasema hadharani kinyume. Ina maana walivunja kitu inaitwa 'Collective responsibility' Mie nilikuwa nategea aidha wajiuzulu wenyewe ama walazimishwe kujiuzulu! Lakini Kimya!!! from both sides. Mkulu anahofia kuwaambia wamachi out!! nao wamemtega! haya majamaa ni vipanga, maana wanajua mkulu hana ubavu saa hii kuwaambia wamachi out. Mhh!! je Rais bado anadhani analinda katiba aliyoapa kuwa atailinda?? Usanii. Na a mekaa kimya!! je mbona wanaharakati hawatamka hilo? inaonekana serikali imeshindwa kazi! AU MNASEMAJE GREAT THINKERS!! Nawasilisha. Tulivalie njuga ili tuone mwisho wake. Maana hawa majamaa wanatukoroga. Bado nchi inawatawalika kidemokrasia?
 
Back
Top Bottom