Je Karume DAY ina UDINI?

Haya ndio matunda ya Jakaya Kikwete, mbegu alioipandikiza ya udini haitamwacha salama, na wala haitaicha Tanzania salama, mwenye masikio na asikie. mtoa mada yuko sahihi, jibu ni udini mtupu ndio maana hakuna askofu aliealikwa pale.
 
mkuu mavazi yasikuhofishe. tunajua wakristo wakiona kanzu na kofia tu kwa waislam tayari wao hofu huwaingia. hili ni tatizo. usiogope mavazi mkuu hata wewe waweza kwenda dukani na kuchukua kanzu wayo kwani ni vazi tu.
mimi kitu ambacho nakiona kapa ni bora hizi siku za wafu ziunganishwe iwe moja kuliko kupoteza siku kibao za kulijenga taifa letu. au hata ingewezekana zifutwe kabisa.
wenzetu wa Asia wanafanya kazi usiku na mchana kama china na wako mbali sana kiuchumi sisi tunaenda kazini kutimiza tu siku ili kusubiri mwisho wa mwezi na kundika madokezo mengi ya kuiba hela za wananchi. we need a true change.
 
Dah !kwa kweli tunahitaji katiba mpya,ili sheria,haki na mipaka ya uhuru wa mtu na mtu tuijue...kwa fikra na mawazo haya sidhani kama Tanzania ni salama.
 
Km huna ushahidi ucropoke coz cjui yule ni padri au askofu bt alikuwepo akasoma dua au kwa kuwa analafudhi ya znz ukafikiri ni muislam 7bu waislam wamefuata utaratibu wao wa kusoma hitima sasa wewe una DIS nini
 
Haya ndio matunda ya Jakaya Kikwete, mbegu alioipandikiza ya udini haitamwacha salama, na wala haitaicha Tanzania salama, mwenye masikio na asikie. mtoa mada yuko sahihi, jibu ni udini mtupu ndio maana hakuna askofu aliealikwa pale.

Saigon acha kuropoka,pale hakuna udini wote wote,ni viongozi tu wamekwenda kwenye kaburi lake na kumwombea,tena alikuwepo na mwakili kutoka jumuiya ya wakristoa naye alitoa sala zake,sasa tatizo liko wapi....mimi ni mkristo,ila siungi wazo potofu kabisa kama haya,na wewe mleta mada,kama una issue ya maana ni bora kukaa kimya tu,kuliko kupayuka...ooh udini..!
 
Kwa nini haya ya kumbu kumbu za viongozi marehemu yamezuka karibuni ? sikumbuki kama kabla watu waliomboleza au kukumbuka kifo cha Karume. Kwa nini sasa ?

Nikiwaheshimu viongozi wote waliopita lakini naona pia Watanzania wana mambo mengi ambayo yanahitaji wao na viongozi wao kuyashughulikia . Viongozi wote waliopita watakumbukwa kwenye sikukuu ya mashujaa. Kama famili zao wanataka kufanya kumbu kumbu basi hiyo pia ni sawa lakini lisiwe jambo la kitaifa .
 
Mbona hujalalamika wakatoliki walipompora 'baba yetu wa taifa' na kumfanya mtakatifu wao? Hapa hakuna udini?
 
Wana jf hebu toeni mada ambazo kweli zitawapambanua km ni great thinkers wa ukweli, manake kuna pumba zinatolewa mpaka zinatia kichefuchefu. Nilichokigundua hii dhana ya udini tunaipka cc wenyewe na wala c viongozi. NA WW MTOA MADA KAMA UMETUMWA USHINDWE NA ULEGEE, Watanzania hatutagawanyika kwa micng ya udin. Udin pale unatoka wapi? Zile kanzu? Au dua? Ulitaka asikumbukwe kwa kuombewa dua kwa micng ya dini yake? Basi chunguza tena oct. 14 uond mwl anafanyiwa nini afu ndo urudi kuropoka? MODERATOR NAOMBA UNIPE MWONGOZO KWA HILI: KILA MADA IPIGIWE KURA KABLA YA KUWEKA JAVINI ILI KUZIPOTEZEA ZISIZO NA KICHWA WALA MIGUU
 
nacheki station flani ya cameron wanaonesha enzi za utumwa hadi mapinduzi yalivyo tokea, inavutia sikuwahi kuona sura ya karume orignal
 
Nafikiri sio ya kidini japo hawa viongozi wetu wamejaribu kuichukulia hivyo. Nafikiri wajitahidi kuifanya ya kitaifa zaidi kwa kufanya mambo ya kumuenzi kama kufanya mihadhara na mijadala mbalimbali inayojadili mambo aliyoyafanya akiwa hai.
 
Haa haa haaa hii ni kali

Nakubaliana na wewe kabisa huu ni udini wa uwazi, na siyo hili tu watanzania tuna tabia ya udini kila tunachokifanya. Ukipita kwenye maofisi ya public utakuta wafanyakazi wameweka nyimbo za dini kwenye makompyuta yao, wengine wamevaa rozari, wengine wanasalimiana bwana yesu asifiwe, wengine wameweka miti ya krismass wengine wamevaa mabarakashia.

Na kosa kubwa sana ni pale serikali iliporuhusu dini kutoa huduma za elimu na afya kwa wananchi wake baada ya Uhuru. Kwa ufahamu wangu huduma hizi ni haki ya msingi ya binadamu na pia ni majukumu ya msingi ya serikali. Hivyo nilizani havikutakiwa vimilikiwe kidini au kikabila kama kweli Tanzania tulikusudia iwe secular state.

Nasikitika kuona ni too late, kusawazisha sasa hivi maana wengi wamelelewa huko, Udini, dini, udini, dini. Viongozi waliokuwepo wakati wa uhuru wamepoteza fursa ya kututengenezea taifa safi la Tanzania. Kwa ufupi hawakuweka misingi yoyote ya kuzuia udini. maana huwezi kuzuia kitu kwa kutumia mdomo tu ukifa jee watakaozaliwa baada ya wewe kufa nani atawazuia. tafakari.
 
Mimi sioni udini wopwote hapo labda jaribu kufafanua kidogo hapo udini unakujaje?? Kwa watu kwenda makaburini kuomba dua na wala sio kusali??? Mbona sherehe zote za kiislam (idd kubwa na ndogo) na za kikristu (krismas na pasaka) ni sherehe za kitaifa na watu wanakwenda kusali??? Au mleta mada hata hujui maana ya siku ya kitaifa??? Yaani watanzania mshakubali kuingia kwenye mtego wa ccm wa kuangalia kila kitu kwa jicho la udini??? kuweni waangalifu sana waloanzisha hili jambo la udini wana hoja moja tu kututawala siku zote!!!:help:
 
Ingekuwa ni vizuri tukaadhimisha siku ya kuzaliwa kuliko kufa, maana kufa mara nyingi kunaendana na Ibada ya kumwombea marehemu! Sasa sala za kiserikali sijui zikoje, tufuatishe kama ile ya Bungeni?
 
Kwa
sababu, ukimkiri Yesu
kwa kinywa chako ya kuwa ni
Bwana, na kuamini moyoni
mwako ya kuwa Mungu
...alimfufua katika wafu,
utaokoka. Kwa kuwa, kila
atakayeliitia Jina la Bwana
ataokoka. Warumi 10:9,
13.
 
Back
Top Bottom