Elections 2010 Je kama Upinzani ukishinda?

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Mimi najiuliza kama kweli Upinzani ukishinda je CCM watakuwa tayari kuachia madaraka??Au ndo kutumbukiza nchi katika vurugu je Upinzani unaweza kuongoza nchi??Je Kwa nini unadhani Jakaya Kikwete hatakiwi kupewa kipindi kingine??Je Dr.Slaa unadhani anaweza kumshinda JK?Je unadhani kura zitakazopigwa zitakuwa salama??wakati Kamanda wa kikosi cha operation Kamanda Tossi ametamka wazi kila yeyote yule akimaliza kupiga kura siku hiyo atawanyike eneo lakupigia kura!!Je hao watakao baki watamdu kuthibiti hayo maboksi ya kura zetu je hawahongeki au takukuru watawekwa kudhibiti hali??Mimi nawewe hatujui ila unaweza kuweka mawazo yako hapa.
 
Hadi hapo watakaposhinda (kwa mwaka huu kushinda wapinzani haiwezekani). Namaanisha hawawezi. Kuweza kunahitaji maandalizi sio bla bla.
 
wakishinda mwaka huu wataibiwa au hata kuporwa ushindi... ila wakishinda 2015 mambo yanaweza kuwa mengine

I'm no psychologist but surely misplaced optimism can lead to a state of delusion
 
ndoto za ali nacha, hakuna uwezekano wa kushinda hata siku moja

si kwa mwaka 2010 wala 2015 na wala si 2020
 
Upinzani kushida kwa kura wanaweza kushinda lakini Lewis Makame hayuko tayari kuwatangangaza kama wameshida ni CCM mpaka kiyama au mpaka pale watanzania watakapo mka kwenye usingizi mzito. kwa kifupi kwa tume hii ya makada wa CCM yakina Makame ni muhali kushinda.
 
Kushinda uchaguzi (Urais) itawawia ugumu japo maajabu hutokea...kuongoza nchi hawataweza coz nashawishika kuamini CCM watapata wabunge wengi kutokana na maandalizi waliyofanya na kusimamisha mgombea kila jimbo hivyo kusumbua bunge kwa kutounga mkono hoja/miswada ya serikali ya upinzani...JK amejitahidi kuisimamia ilani ya CCM na utekelezaji wake unaonekana japo kwa maeneo kadhaa yaonekana kuna mapungufu coz watendaji wake wamemwangusha...Dr Slaa kumshinda JK ni ngumu kama ataamua kusimamia sera na ilani ya chama chake ila kama atasimamia kuongelea ufisadi basi anaweza akashinda (baadhi ya maeneo) ila si jambo zuri kuzungumzia ufisadi tu na kusahau kuweka sera na ilani mbele..so kwa mtazamo wa haraka (na maoni yangu binafsi) naona hataweza kumshinda..as for wapiga kura nadhani iko haja watu wakatii maelekezo wanayopewa coz si busara kupiga kura na kubaki unazubaa kituoni coz wagombea na vyama vina wasimamizi wao na pia kuna wakaguzi so wananchi hata wakijazana hapo haitasaidia na watasababisha hofu na hivyo kuwafanya polisi kujiweka tayari kwa lolote..hofu kubwa ni je wasimamizi wananunulika au la?hilo ni la msingi coz kama msimamizi akinunuliwa basi hiyo ni hasara ya chama husika ila nadhani wote watakaowekwa vituoni ni waaminifu na wako committed kwa vyama vyao so kwa hilo ni mtu mwenyewe ataamua kukiuza chama chake au la...
kwa ujumla nadhani ni vema kuanza kujiandaa kwa siku hiyo kwa kuwapa somo mawakala wa vyama vyetu na wananchi kujua wajibu wetu siku hiyo ni upi na haki yetu ni ipi ili kuepusha rabsha zinazoweza kutokea kwani jazba kidogo yaweza kuwapa polisi sababu ya kukuumiza..tuwaambie ndugu na jamaa wajue nini wafanye na nini wasifanye siku hiyo Oktoba 31.

NB:ni mawazo tu so unaweza kupingana nayo(kwa hoja)
 
Si kwamba CCM itaiba kura ila itashinda kihalali kama wapinzani hawataungana.
 
Sina wasi wasi Upinzani mwaka huu utashinda.

1. Wataweza kuwa na wabunge wengi kupita mara zote
2. Kura za uraisi zitakuwa nyingi kwa upinzani kupita miaka yote
3. Wabunge wengi wa CCM kuangushwa
4. Upinzani kupata madiwani wengi na kuweka historia
 
ndoto za ali nacha, hakuna uwezekano wa kushinda hata siku moja

si kwa mwaka 2010 wala 2015 na wala si 2020

acha mambo ya ushehe yahaya hapa bwana kwani ccm ninaniwasitoke!??? kumbuka KANU kenya!! Ubaya unamwisho!!
 
Sina wasi wasi Upinzani mwaka huu utashinda.

1. Wataweza kuwa na wabunge wengi kupita mara zote
2. Kura za uraisi zitakuwa nyingi kwa upinzani kupita miaka yote
3. Wabunge wengi wa CCM kuangushwa
4. Upinzani kupata madiwani wengi na kuweka historia


sasa nnauliza mtashinda mtapata kura nying ? hapa mshaonesha inferiority, ,,eisha nyinyi
 
Back
Top Bottom