Je kama ni wewe unatakiwa kufanya nini hapa??

Utamwacha baba na mama yako. By the way, ndoa si ukumbini, ni kuunganishwa kanisani? Hamjawahi ona mtu anafunga ndoa na mgonjwa mahututi au hata marehemu?
 
Ikitokea katika familia yenu mkabahatika kuoza na sendoff ikafanyika lakini ijumaa ambapo kesho yake Jumamosi ndiyo harusi ukaambiwa mama wa Bwana harusi anaumwa yupo katika koma(ICU) Je kama wanafamilia yawapasa mfanyeje ukizingatia upande wa bibi harusi wao wameisha fanya sendoff!!Kilichokuwa kikisubiriwa ni Harusi!!

Kuahirisha litakuwa ni jambo la busara...

Ila kufunga ndoa kusiahirishwe.... Ila sherehe ndiyo isitishwe...

Sema utafaidika na michango ya wanakamati,(itategemea busara zao) ila utakosa zawadi za wageni waalikwa
 
Kuna siku nilitoa mkasa kama huu hapa..............watu tumefikia mahala pa kuzithamini hizi sherehe bila kujali utu hata chembe........sasa maana ya sherehe ni nini...............mnaitoa wapi furaha ya kushereheka?............kama ni vyakula wagawieni masikini wenye njaa mtapata thawabu mara elfu kuliko ubinafsi mnaouendekeza.......maana kwa kweli huku ni kujiendekeza kulikopitiliza!
 
Aaaah, bwanaeee, hakuna anayefurahia ugonjwa ama kifo, but kwenye hali kama hiyo just one day before harusi, hapa harusi inapigwa kama kawaida, then baada ya hapo tunaendelea na kuuguza. Hata ukiahirisha harusi kama ni ugonjwa ni ugonjwa tu, ama kama mtu kafariki ndo hivyo amekwishaondoka. Kinachotakiwa ni kuwaficha wahusika wasipewe taarifa ya uhalisia. Sasa kama akiendelea kuugua kwa mwezi ama zaidi, mtaahirisha hadi lini wakuu?? Ukichuzingatia gharama zilivyo katika harusi/send off, ni kupiga tu then mengine badaye.
 
Back
Top Bottom