Je kama ni wewe unatakiwa kufanya nini hapa??

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Ikitokea katika familia yenu mkabahatika kuoza na sendoff ikafanyika lakini ijumaa ambapo kesho yake Jumamosi ndiyo harusi ukaambiwa mama wa Bwana harusi anaumwa yupo katika koma(ICU) Je kama wanafamilia yawapasa mfanyeje ukizingatia upande wa bibi harusi wao wameisha fanya sendoff!!Kilichokuwa kikisubiriwa ni Harusi!!

Nikisa cha kweli aliyesababisha ni mamake Brandina Nyoni na Sasa amefariki sijui kama itafungwa hiyo ndoa na kwaresima hii hiyo mpaka April.....!!!!!
 
Mkuu ugonjwa ni zaidi ya sherehe aise
Kuna watu washafanya kila kitu wanasubiri hivyo na msiba ukatokea ambapo mwanafamilia mmoja akafariki
Kila kitu kilisimama mkuu kupisha msiba
Msiba au ugoonjwa ni kitu kingine
Mama yuko ICU na wewe unaserebuka ukumbini hata nyani watakuona hamnazo aise
 
Harusi huwa inaahirishwa na hii ilitokea kwetu, kakangu alifanya send-off alhamisi, baba yetu akapata ajali ijumaa na kufariki jumamosi alfajiri, hivyo suala la ndo liliahirishwa.
 
n upuuz sherehe unaweza kui reschedule ila c ugonjwa au msiba! Ingekuwa unataka fanya mitihan final thn unatokea msiba unaweza kuendelea na paper thn ukaja kulia mbelen wkt ushajenga future ila harus tena hyo michango menu na bia napeleka msibani.
 
Hajafa sasa (ICU)!
 
Hajafa sasa (ICU)!

Mkuu nikuulize
Samahani kama nitakukwaza
Ni mama yako mzazi wewe bwana harusi ndio yuko ICU anaumwa
Kweli utakuwa na nguvu za kukaa pale mbele unatabasamu na kucheka wakati unajua hali ya mama kule sio nzuri
Sidhani hata hizo nguvu za kusherehekea utakuwa nazo
 
Mkuu ugonjwa ni zaidi ya sherehe aise
Kuna watu washafanya kila kitu wanasubiri hivyo na msiba ukatokea ambapo mwanafamilia mmoja akafariki
Kila kitu kilisimama mkuu kupisha msiba
Msiba au ugoonjwa ni kitu kingine
Mama yuko ICU na wewe unaserebuka ukumbini hata nyani watakuona hamnazo aise
Hapa harusi inapigwa tu
 
Hapa harusi inapigwa tu

So we mzazi yuko ICU anaugulia maumivu wewe unapiga harusi
Duh kuna watu wana roho sana aise
Nini unachokimbilia ambacho hakiwezi kusubiri mzazi arudi kwenye afya yake ni chakula kile au vinywaji au kulala na yule dada (afterall ushalala nae sana so sio mpya kihivyoo)
 
Mkuu nikuulize
Samahani kama nitakukwaza
Ni mama yako mzazi wewe bwana harusi ndio yuko ICU anaumwa
Kweli utakuwa na nguvu za kukaa pale mbele unatabasamu na kucheka wakati unajua hali ya mama kule sio nzuri
Sidhani hata hizo nguvu za kusherehekea utakuwa nazo
Itategemea na mtazamo wangu na mtazamowangu hauwezi kuwakilisha mawzo ya wanajF ukae ukijua.
 
Itategemea na mtazamo wangu na mtazamowangu hauwezi kuwakilisha mawzo ya wanajF ukae ukijua.

Yeah I accept that
Msimamo wangu ni tofauti sana aise
Mkuu hapo nitakuwa nakusemea ila msimamo wangu ni huo hakuna sherehe aise wakati nina mgonjwa yuko ICU
 
Yeah I accept that
Msimamo wangu ni tofauti sana aise
Mkuu hapo nitakuwa nakusemea ila msimamo wangu ni huo hakuna sherehe aise wakati nina mgonjwa yuko ICU
kila mmoja anajua anaamini vipi ndiyo maana wengiwetu wanasema itafanyika kimya kimya!Ila ngoja nikuulize swali hivi ukifanya hiyo harusi kwakuwaelezea watu ndoa hii itakuwa nifupi kwa sababu iliyoko nje ya uwezo wetu kwamba tumepata taarifa Mama mzaa bwana harusi kakimbizwa Hospital hivyo tunasikitika baadhi ya matendo hayatafanyikwa utaratibu uliozoeleka kitakachofanyika ni kula keki na kula nakuleta zawadi na ndo mwisho wa harusi je itakuwaje??
 
Kwani harusi kitu gani ni bora mkashughulika na suala la mama. Hata hiyo sendoff nadhani inatosha kuwatambulisha kuwa mlifanya sherehe ya kuoana
 
Mkuu unaweza ukawa na mtu sehem kimwili tuu ila kimawazo yuko mbali sana
Yaani utakuwa umekaa na Bwana Harusi kimwili tuu ila kimawazo yuko mbali sana
Na harusi for some reason ni so special kwa watu atataka kwa gharama alizoingia awe na kumbukumbu ya tukio zima
Ile kuifanya haraka haraka kwa kuwa kuna tatizo matukio mengine yakarukwa kwa wengine sio fair kabisa
 
Kwani harusi kitu gani ni bora mkashughulika na suala la mama. Hata hiyo sendoff nadhani inatosha kuwatambulisha kuwa mlifanya sherehe ya kuoana
Unamsaidiaje mtu yupo ICU na wala hauruhusiwi kuingia!!
 
nafikiri waweza kwenda funga harusi bila sherehe,kama swala ni siku special bado itakuwa special tuu kwani itakupa kumbukumbu ya kuoa bila sherehe wala honeymoon kwa ajili ya mama aliye mgonjwa.mpe pole mgonjwa
 
Ikitokea katika familia yenu mkabahatika kuoza na sendoff ikafanyika lakini ijumaa ambapo kesho yake Jumamosi ndiyo harusi ukaambiwa mama wa Bwana harusi anaumwa yupo katika koma(ICU) Je kama wanafamilia yawapasa mfanyeje ukizingatia upande wa bibi harusi wao wameisha fanya sendoff!!Kilichokuwa kikisubiriwa ni Harusi!!

Ndio maana mwashauriwa vitu hivi vifanyike wiki moja kabla ya harusi.
 
Back
Top Bottom