Je, JK akikupa post serikalini utakubali?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,329
6,447
Ukiwa kama mwana JF ambaye unataka mabadiliko ya kweli kwa watanzania, leo hii JK anakuteua kushika wadhifa fulani serikalini au katika shirika la umma; je utakubali? Kama ndio au hapana, tupe sababu za msingi! Ulimwengu alikwisha wahi mkatalia Mkapa!!
 
Nikipewa post ambayo nna uhakika inaendana na elimu yangu, kiwango changu cha uelewa, uwezo wangu wa kuongoza, uwezo wangu wa kuhimili majukumu NITAIPOKEA ili kuweza kusaidia taifa.

nikifika kati kati nikitakiwa kuchukua maamuzi yasiyo mema kwa taifa nitaacha kazi
 
nitakubali hiyo nafasi kama ninaiweza na pia kabla ya kuanza kazi itabidi niweke wazi mpango wangu wa the assignment execution... when a general calls, you have to respond immediately

CAUTION: USIPOKEE KAZI WITH TOO MUCH EXPECTATIONS BECAUSE ALOT IS EXPECTED FROM YOU AND NOT OTHERWISE
 
No, kwa vile nitakuwa napoteza raslimali muda bure. Hakuna sababu ya mimi kuajiriwa mahali ambapo nina uhakika 100% nitakuwa fired baada ya miezi 2-3...
 
if i will be a supervisor..

1.Nitakuwa mkali kwa wezi wote na sitawaonea haya hata kama ni wakongwe wa chama

2.Nitahakikisah mabadiliko makubwa ya sheria yanafanyika ili yaendana na kasi ya kuleta mabadiliko

3.Watu wote ambao hawana uwezo wa kuleta mabadiliko nitawang'oa,itakuwa siyo serikali ya kulipana fadhila..
 
JK hawezi kunipa Uwaziri kwa sababu mimi simo kwenye Mtandao wala si Fisadi! Tuwaze Uhalisia. Sema 'Kama ningekuwa Waziri wa Tanzania ningefanya nini cha kuisaidia nchi yangu'! At least hili linawezekana. Ten years from now JK hatakuwa madarakani na wewe unaweza bado ukapata bahati ya kuteuliwa kuwa Waziri! my two cent...
 
hivi kwa siku za nyuma kuna mtu aliwahi teuliwa na prezida akakataa? if yes alitoa sababau gani?
sorry for asking
 
Mtu yeyote akiteuliwa na rais kushika madaraka bila shaka atayakubali isipokuwa rais mwenyewe hawezi kumteua mtu yeyote asiyekuwa mwanachama wa CCM kushika madaraka ya uongozi ngazi ya juu ya uongozi wa serikali kutokana na mfumo wa Kijamaa tulokuwa nao..

Toka enzi ya Mwalimu kiongozi yeyote alilazimika kujiunga na chama kwanza ili kupewa wadhifa wa juu serikalini au mashika ya Umma..Hivyo ni swala la kuuliza - Je, rais anaweza kumteua mtu kushika wadhifa serikalini au shirika la Umma hali mtu huyo ni Mpinzani wa siasa za chama CCM?
 
hivi kwa siku za nyuma kuna mtu aliwahi teuliwa na prezida akakataa? if yes alitoa sababau gani?
sorry for asking

Waziri wa maji Mh. Mark Mwandosya aliwahi kuacha kazi akarudi kufundisha baada ya kuletewa mizengwe katika maamuzi yake ambayo aliyaona yalikuwa sahihi. By then alikuwa katibu mkuu wa wizara na JK alikuwa waziri.
 
hivi kwa siku za nyuma kuna mtu aliwahi teuliwa na prezida akakataa? if yes alitoa sababau gani?
sorry for asking

Prof.Issa Shivji alimkatalia Nyerere kuwa waziri (wa nini sijuwi) alimwambia hawezi kuwa karani wake!
 
Mtu yeyote akiteuliwa na rais kushika madaraka bila shaka atayakubali isipokuwa rais mwenyewe hawezi kumteua mtu yeyote asiyekuwa mwanachama wa CCM kushika madaraka ya uongozi ngazi ya juu ya uongozi wa serikali kutokana na mfumo wa Kijamaa tulokuwa nao..

Toka enzi ya Mwalimu kiongozi yeyote alilazimika kujiunga na chama kwanza ili kupewa wadhifa wa juu serikalini au mashika ya Umma..Hivyo ni swala la kuuliza - Je, rais anaweza kumteua mtu kushika wadhifa serikalini au shirika la Umma hali mtu huyo ni Mpinzani wa siasa za chama CCM?

Mkuu wakati tulinao ni wa vyama vingi , na chama kinachoshinda uchaguzi mkuu ndio kinachouunda serikali kwa kuwa hakuna serikali mseto, hivyo kusema lazima awe ccm ndio JK atatmteua ni kweli kwa mantiki hiyo niliyoelezea hapo juu na vinginevyo kama ulivyoelza awali.
 
JK hawezi kunipa Uwaziri kwa sababu mimi simo kwenye Mtandao wala si Fisadi! Tuwaze Uhalisia. Sema 'Kama ningekuwa Waziri wa Tanzania ningefanya nini cha kuisaidia nchi yangu'! At least hili linawezekana. Ten years from now JK hatakuwa madarakani na wewe unaweza bado ukapata bahati ya kuteuliwa kuwa Waziri! my two cent...

Mkuu, naomba radhi in advance.... mbona sijaona hiyo nafasi ya uwaziri kutoka kwa mtoa mada? yeye amesema wadhifa tu, kwani wadhifa ni uwaziri tu jamani??

Nionavyo mimi uwaziri ni cheo kibaya kwani ni cha kisiasa zaidi wakati mie naheshimu zaidi watendaji.... we imagine hata sophia simba naye waziri... KAMA NI UWAZIRI HATA MIMI NINGESEPA
 
Nikipewa post ambayo nna uhakika inaendana na elimu yangu, kiwango changu cha uelewa, uwezo wangu wa kuongoza, uwezo wangu wa kuhimili majukumu NITAIPOKEA ili kuweza kusaidia taifa.

nikifika kati kati nikitakiwa kuchukua maamuzi yasiyo mema kwa taifa nitaacha kazi

Very well said Gaijin kula tano hapo ^^^^^
 
Mkuu wakati tulinao ni wa vyama vingi , na chama kinachoshinda uchaguzi mkuu ndio kinachouunda serikali kwa kuwa hakuna serikali mseto, hivyo kusema lazima awe ccm ndio JK atatmteua ni kweli kwa mantiki hiyo niliyoelezea hapo juu na vinginevyo kama ulivyoelza awali.
Mkuu sijakuelewa hapa maanake najua ktk serikali ya Marekani wapo viongozi walioshika mamlaka wakati wa Bush na wanaendelea kushika mamlaka hayo wakati huu wa Obama..Hapa kwetu wapo viongozi wengi wa mashirika ya Umma na vyombo vya utendaji ambao elimu na ujuzi wao wa kazi (uongozi) hauhusiani kabisa na Uanachama au itikadi ya chama.

Ila ni kweli zipo nafasi za Uongozi serikalini ambazo lazima zichukuliwe na Uongozi uliopo madarakani ili kusimamisha policies za sera zao ktk majimbo waliyoshinda au Kitaifa..Mathlan Kikwete ni rais wa nchi, itokee mkoa wa Kilimanjaro wamechukua Chadema sidhani kama ni busara kuweka mkuu wa mkoa au wilaya kutoka CCM hali ushindi wa kiutawala umepewa Chadema.

Mtumishi wa Umma sii lazima awe mwanachama wa chama tawala ili kufuata sera za chama chake isipokuwa ni elimu yake ndiyo inayompa nafasi ya kushika wadhifa huo...Hapa ndipo tunapotenganisha Siasa na Uongozi, ingawaje ktk madaraka yote ya juu serikalini ni lazima chama kinachotawala kusimamia mamlaka yote yanayoongoza vyombo vya serikali..Sina hakika zaidi na mfumo wa kiutawala lakini hivi ndivyo navyuoona wenzetu wakishiriki ktk Utawala wa nchi zao.
 
if i will be a supervisor..

1.Nitakuwa mkali kwa wezi wote na sitawaonea haya hata kama ni wakongwe wa chama

2.Nitahakikisah mabadiliko makubwa ya sheria yanafanyika ili yaendana na kasi ya kuleta mabadiliko

3.Watu wote ambao hawana uwezo wa kuleta mabadiliko nitawang'oa,itakuwa siyo serikali ya kulipana fadhila..

You are very naive and you will be frustrated to such an extent that you will commit suicide! Wewe umeteuliwa na Jakaya katika wadhifa fulani, umeikuta system yake inafanya mambo yake , Je wewe utawafukuzaje kazi watu ambao system ya Jakaya inawakubali? Mathlani leo Gembe umeteuliwa kuwa waziri wa Kazi na umegundua kuwa Mkurugenzi mkuu wa NSSF ni mla rushwa kiasi kwamba anaogopa hata kuweka fedha benki anachimbia nyumbani kwake, Je wewe una nguvu za kumuondoa mwizi huyu toka kwenye nafasi yake? Hapo hapo ukumbuke kuwa NSSF ni mfadhili mkuu wa chama Tawala ambacho aliyekuteua ni mwenyekiti wake!!.
Ukikubali uteuzi wa Kikwete maana yake umekubali mfumo wa utendaji wa serikali yake; kuwatumikia mafisadi na si wananchi!!
 
Hapana siwezi kukubali nafasi hiyo. Sababu yangu ya msingi ni kama ifuatavyo:-

Asilimia kubwa ya viongozi walio madarakani ni wachafu, wananuka rushwa, wizi, uzembe, uvivu nk. Na hao ndiyo watu nitakaopaswa kushirikiana nao kila siku katika utendaji wangu wa kazi. Itaniwia vigumu sana kufanya kazi na watu kama hao kwani sina huruka na tabia kama hizo. Nitawachukia watu hao, nitaichukia kazi yangu na kujichukia mimi mwenyewe.

Na kumbuka ukifuatana na genge la wezi na wewe utaishia kuwa mwizi.
 
This is not even a question.

Utaratibu wa kupeana kazi based on subjectivity SHOULD BE DISCOURAGED FORTHWITH. Kazi za umma zinabidi zipewe watu based on competitive merits and procedure, and thats it.
 
Wengi wanafiki tu.Wewe leo hii mfano uteuliwe ubunge,halafu upewe wizara utachomoa?Wengi wapiga kelele JF kwavile wako nje ya system,lakini wakikatiwa ulaji ndiyo hao watakuwa wakwanza kuifisadi nchi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom