Muadilifu
Senior Member
- Sep 26, 2007
- 149
- 22
Jina linajieleza. Niliamua kutumia jina hilo ili, kwanza kuuonesha umma kuwa hata katika nchi ambayo imejaa watu corrupt, bado tupo waadilifu wachache, na nimekuwa nikijitahidi siku zote (kwa msaada wa Mungu) kuishi sawa sawa na jina langu. Pili kuleta ladha ya tofauti, maana nimekuwa nikishuhudia majina yanayopendwa sana siku hizi, ni Fisadi(mtoto), Shetani, "mwaga ugali nimwage mboga"..etc. Tanzania yenye uadilifu inawezekana, usisubiri wawepo wengi, anza wewe wengine watafuata.