Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

Gudboy: hili ni jina la ni wimbo flan wa jamaa Niki wa 2 naupenda sana kwa sababu vitu vingi alivyoimba vinareflect maisha yangu. Mfano pale aliposema gudboy akiwa na kitu moyoni hafichi anasema, hakuna ubaya kama kufanya mabaya mbele ya watoto wanaotuiga leo ili wakafanye mema kesho, kubalehe ni mtihani na wengi wamefail, nani kasema shujaa azaliwi guest, fanya kazi ujenge urafiki na hizi hela, sina chuki za CCM kwenye ubongo wa Lipumba, utajiri wa kwanza ni kuwa na marafiki, simtongozi mwanafunzi kumharibia maisha, usimwache anayekupenda mapenzi yakamfunga jela, wingi wa mashori sio kipimo cha urijali kama mwanaume wa kweli nyumbani wapate ugali, gudboy huamka mapema.

hii ni kati ya mistari katika wimbo huu ambao nauzimia ile mbaya, maana nami ni gudboy mazee
 
i am the firstlady - Y not ninaweza nina confidence nina sifa zote za kuitwa hivyo na ninajitambua kama FL
Sikuipenda siasa ,niliichukia na siku zote niliona wanasiasa wote ni waongo sana promise nyingi utekelezaji hafifu..
napenda fashion so very much -FL
Lakini sasa nataka nijikite kwenye siasa zaidi nijue kuna nini huko mpaka tunadanganyika nijue ni kwanini wazee wanalilia madaraka ,ni kwa nini hawataki kung'atuka ....nataka kumake changes kam FL

Kupitia JF nimeanza kupata kile nachokiitaji
 
Kisoda,ni kifuniko/mfuniko/kizibo wa chupa ya soda.
Nalitumia hili kutokana na kumbu kumbu za shule za awali enzi zile za mwalimu,unatunga viiingi kwenye kijiifito na kamba mfano wa upinde ili upate jifunxa kuhesabu(macalculee flan nyakati hizo).
Pia kama ilivyo matumizi yake ni kuziba/kuzuia kitu kisitoke/mwagika.Kwa maana hiyo kwangu ikitokea nimekereka/kerwa hua na amua kukaa kimya kwa muda nikitafakari kulikoni iwe hivyo,kuepusha kutoa kauli ambayo inaweza kuwa mbaya zaidi upande wa pili ama kwangu pia.
Natumia Kisoda2 ikiwa ni mfuniko tu hata uniudhi vipi nitanyamaza kwanza kisha nikutafutie jibu/neno sahihi la kukupa.
 
Nimeipenda sana hii post,jina nalotumia ni la kwangu la kinyumbani,Msindima maana yake ni Msi-Mchana na ndima ni kazi,kwa hiyo maana halisi ya jina langu ni mchapakazi mchana kutwa,nalipenda sana jina langu.
 
Kimey is my real name. Niliingia JF nikajirejister kwa real name then nikagundua kua wengi humu JF hawatumii real names.. sasa ishu ikaja nataka kubadilisha niweke na mm jina la utani wapi bana ndo hapo nikakundua kua once umeshajiregister ni vigumu kubadili unless utume maombi kwa wahusika na utoe sababu...then nikaamua kuacha kama lilivyo...
 
wa-Swahili husema: ee bwana ee, ile gari (jamaa, pikipiki, etc) imetoka resi, si mchezo! na mimi ninayo tabia kwamba nikishapanga kazi yangu, factor zote zikisema tick, sina simile. huanza kazi kwa 0 to 60 in 2 seconds!! hutoka resi!!
 
tangu1979 kila wakati huwa najaribu kutafuta yaliyo jili kutoka vyanzo mbalimbali vya habari,,hivyo nikajikuta nikitamani kujiita yaliyojili lakini nikakatisha nikaamua kujiita jile79..........
 
Sikonge ni Sikonge. Wilaya moja wapo ya Mkoa wa Tabora. Ni kimji kidogo sana na kimegawanyika katika sehemu mbili. Moja ni ile inaitwa Misheni (kwa wamisionary wa Moravian Church) na nyingine ni Madukani. Hii unayoona karibu ndiyo Misheni na ile ya mbali ni Madukani. Karibuni Sikonge, Wanyamwezi hatuna noma......

 
Back
Top Bottom