Je huu si wizi wa waziwazi wa mabenki yetu?

Andindile

JF-Expert Member
Mar 18, 2009
304
16
Wakati nasafiri kwenda ng'ambo niliacha kwenye account yangu sh. million 7 katika moja ya benki hapa nchini. Niliishi huko kwa muda wa miaka minne. Baada ya kurejea nilikuta account yangu imefungwa kwa kigezo kuwa nilikaa zaidi ya miezi 6 bila kuihudumia.

Iwapo walifunga account yangu, je pesa zangu hawakuzifanyia biashara yoyote?

Na kama walikuwa wanazifanyia biashara, je faida iliyopatikana si ya dhuruma?

Je naweza kudai riba kutoka benki kwa kutumia pesa yangu kwa kipindi chote hicho ambacho account yangu ilifungwa?


naomba msaada wenu
 
BOT ndio wakupigia kelele hawanap policy nzuri na mojawapo ya policy mbaya ndio hiyo inayowataka mabenki kuangalia kwa ukaribu account zilizoko kwenye category ya domant kitu ambacho mabenki wanasema kinaongeza risk na cost kwao kwahiyo wanacharge pesa nyigni zaidi kwa ajiri hiyo
 
Hebu itaje hiyo benki kwa majina yake kamili, ikiwezekana na tawi kabisa. Si unajua hapa tunamkoma nyani mchana kweupe? au ?
 
Hebu itaje hiyo benki kwa majina yake kamili, ikiwezekana na tawi kabisa. Si unajua hapa tunamkoma nyani mchana kweupe? au ?
yeeep! usifiche uozo mkuu, weka hadharani hao banker wajulikane, ujue wahusika wengine tuko nao humhum, kitawawasha watatoa details.mbona sasa naogopa, unaweza kuacha vijisent kidogo ukatoka incase vijimambo vikakwendea kombo ukarudi bilabila, unajifariji ukitegemea utakuta ka-amount kwenye a/c unakkuta patupu, MAMAAA UTALIA, TUKOMAE NAO TU.
 
Mimi wananimaliza tu kwenye makato unapopokea pesa kutoka nje/pesa za kigeni eg £, $ etc, kwanza wanazikata wakati wa kupokea, baadae wanakukata 1% wakati wa kuchukua, exchange rate yao iko chini, hapo bado sijazungumzia jinsi unavyopoteza muda kwenye foleni, kazi kweli kweli...
 
huduma mbovu za mabenki kama hayo ndio tunataka ziwekwe hadharani, wekeni hadharani details tuwape ukweli
 
Nafikiri karibu mabenki yote TZ wana hii sera. Mimi huwa inanilazimu kutuma pesa kwenye akaunti yangu kila baada ya miezi 5 ili kui-keep active na zikifika wanazikata tena, yaani taabu tupu. Pole sana Andindile.
 
Benk yenyewe NMB tawi la benk house. Lipo kule maeneo ya Posta

Mkuu sijui kama upo sirias au unazusha, maana mimi niliacha kutumia akaunti yangu NMB kwa zaidi ya mwaka mmoja na bado ilikuwa active. Ila salio kidogo halikuwa kubwa kama lako, Vp ulijaribu kuongea na meneja wa tawi?
 
Benk yenyewe NMB tawi la benk house. Lipo kule maeneo ya Posta

Grrrrrrrrrrrrr! Nami nna akaunti pale ina vihela kiduchu na sijaenda kwa muda pale kuviangalia. Si unajua NMB wanavoboa? Foleni kama enzi za sukari ya awamu ya kwanza. Ngoja nikaangalie salio nami nitarusha hewani kama watakuwa wamenitenda ubaya huo
 
Mkuu sijui kama upo sirias au unazusha, maana mimi niliacha kutumia akaunti yangu NMB kwa zaidi ya mwaka mmoja na bado ilikuwa active. Ila salio kidogo halikuwa kubwa kama lako, Vp ulijaribu kuongea na meneja wa tawi?

Niko sirias ndugu. Nilikwenda kwa meneja wa tawi ndiye aliyenipa ujumbe kuwa ninachotakiwa kufanya ni kuleta paspoti saizi mbili na sahihi na kujaza form upya ili kuifufua acount yangu. Hasira zimenishika kiasi kwamba nimefikia uamuzi wa kuifunga account yenyewe, ila kabla sijaifunga nataka kujua kama naweza kupata any kind of compersation kwa benk kuifunga account yangu bila kunitaarifu huku wao kuendelea kuzitumia pesa zangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom