Je huu ni wakati muafaka wa kujadili korosho???

MtazamoWangu

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
313
7
kuna wakati nahisi kama hii nchi haina vipaumbele na viongozi wetu wapo kiubinafsi zaidi, kwanini mienendo yetu au shughuli zetu haziendani na wakati tuliokuwa nao?
inafika hatua sasa inakuwa ni kama kuna usaniii kwenye uendeshaji wa nchi hii na kufanya wananchi wajinga na wasionauwezo wa kuhoji maslahi yao katika nchi hii, kundi moja la watu ndio linaamua nini kifanyike na nini kisifanyike....
hivi korosho inaliingizia Taifa kiasi gani cha mapato? nakubali kwamba ni zao muhimu sana kwa upande wa eneo la nchi yetu, lakni je huu ni wakati muafaka kwa kujadili suala la korosho....?? kikao cha bunge cha wakati huu ni kifupi sana na ni wakati muafaka kwa watunga sheria wetu kujadili mambo muhimu yanayoikabili nchi hii, tuna mambo ambayo yanaeelekea hata kuliingiza taifa hili pabaya, suala la umeme wa mgawo,suala la utekelezaji wa maazimio ya bunge juu ya richmond,hili kutokana na uendeshwaji wake sasa limekuwa ni jambo la hatari sana katika mustakabari wa nchi yetu, kwanini halimalizwi maramoja?? tunamlinda nani bora zaidi kuliko amani ya nchi yetu,
suala la madini na korosho lipi muhimu? tumeona na kusikia jinsi wananchi wanaoishi karibu na migodi wanavyoathirika, mgawanyo wa mapato yatokanayo na madini yetu hauinufaishi taifa...
je wakati huu wa njaa korosho ni bora zaidi? hata wanaolima korosho hawategemei zao hilo...

Ninachokusudia kusema ni kwamba, kama taifia sasa lazima tuwe na vipaumbele vya taifa, tujadili, tufanye yale tunayoona ni muhimu kwa mustakabali wa nchi yetu, lakini pia tutatue tatizo lililopo mbele yetu, tuache usanii, mficha marazi.........

huu si wakati wa korosho....
 
Mi kama mkazi na pamoja na biashara zangu lakini pia ni mkulima wa mikorosho Rufiji.

Suala la mjadala wa korosho ni muhimu sana hususan kwa kipindi hiki kwani zao hili tunalazimishwa tuviuzie vyama vya ushirika ambavyo vinakuwa havina fedha na hivyo kutukopa.

lazima nasi tuwe huru na kuuza tunapotaka na kwa yoyote mwenye fedha.
 
Mi kama mkazi na pamoja na biashara zangu lakini pia ni mkulima wa mikorosho Rufiji.

Suala la mjadala wa korosho ni muhimu sana hususan kwa kipindi hiki kwani zao hili tunalazimishwa tuviuzie vyama vya ushirika ambavyo vinakuwa havina fedha na hivyo kutukopa.

lazima nasi tuwe huru na kuuza tunapotaka na kwa yoyote mwenye fedha.

suala sio umuhimu wa zao binafsi..lakini muda huu kweli ni muafaka kwa hili...?
 
Back
Top Bottom