Je huu ni uungwana jamani?

Habari zenu wote wapendwa...........................

Rafiki wa dada yangu amekuwa akilalamika hivi majuzi kuwa mume wake,
amekosa uungwana/upendo na uvumilivu. Huyu dada pamoja na kuwa anaishi mbali na mume wake kutokana na majukumu ya kazi, lakini amekuwa akiisaidia sana familia kwa kugharamia matumizi yote ya nyumbani kuanzia chakula, matibabu, usafiri na mambo yote muhimu ya kimaisha.

Sasa amekuja kugundua kuwa mume wake anatembea na mwanamke mwingine,na isitoshe huwa anamleta mpaka hapo nyumbani. Mara baada ya huyu dada kugundua hayo aliona ni bora asitishe kupeleka fedha nyumbani, ukichanganya na hasira kidogo aliyokuwa nayo basi ndo hivyo tena. Pamoja na haya yote bado mumewe amekuwa ni mtu wa kumletea dharau sana na maneno yasokuwa na heshma. Lakini kwa jinsi huyu bwana asivyokuwa na haya, anazidi tena kumpigia magoti mkewe ili atume pesa za matumizi hapo nyumbani!

wanajamii,Je huu ni uungwana kweli?

mume anaamini kuwa bado ni siri yake,
na wala mke wake hajui hilo!!!!!!!

bacha hapo kwenye red umeniacha kidogo.........mkewe hajui hilo li-nini?

kama yeye kaka anajua kuwa affair yake bado ni siri, huyu dada hajamtendea haki na kwa vyovyote kureact bila kumjulisha mwenzio kwa nini unareact haisaidii sana sana mke atachukuliwa kama ana kiburi na majigambo kwa kazi yake na kuwa anamnyanyasa mumewe UNLESS amemjulisha kwa nini anareact hivyo anavyoreact.

Halafu mke anavyokatisha matumizi hapo nyumbani hakuna watoto/watu wanaowategemea?? au ndo nao wanakula adhabu kwa kosa wasilolijua??

bacha mshauri dada yako amwambie rafiki yake kuwa ni vema akamjulisha/mwonyesha mumewe kuwa anajua kuwa mumewe anacheat ama sivyo kibao kitamgeukia na yeye aonekane ana makosa.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Hapo chacha.

Off topic: Hujarudi nyumbani mpaka sasa mbona uko via mobile??? Ujue mama anakutafuta

Ntarudi baada ya masaa mawili na nusu.. siuna elewa vitu vingine kuacha nusu ni dhambi. mmmmhhh usimwambie maza niko wapi ntakuambia kitu fidodido mikirudi home mmmhhh
 
Aisee ndugu yangu bacha hii hadithi kakufundisha nani uje utuhadithie....:biggrin1:

:focus:
 
Poleni wanawake wote mnaohudumia family zenu duh, ndio haya sasa unanunua mapochopocho mwenzio anakuja kujitanua hapo,.Wanaume hawana huruma sana wajameni akiamua kukutenda anakutenda haswa
 
Kuhudumia familia kwangu sioni kama ni kosa as long as mama ana kipato kikubwa. Kosa ni kucheat. Maana embu nambie kama una kazi ya maana kama Asha Migiro kweli ela zote utapeleka wapi? Kwenye make ups tu. Lazima utakuwa key provider home ili wanao na mumeo wawe na maisha comfortable.

Haya mambo ya kuwa ela za mke ni za kununulia nguo yamepitwa na wakati. Kwenye maisha ya ndoa hata kama wote mna elimu sawa si hajabu mke kuwa na pesa kuliko mume. Unless you still believe women are of lower post jobs!
 
Sijui tufanyaje hapo maana tukitoa wanaenda kutumia na wengine ilobaki tubane tu au?
 
Wewe utakubali wanao wale kisamvu daily na ela unayo? Maana kumbuka kuna watoto si mume peke yake. Utakubali wanao wasome saint Kanumba na pesa ipo simply because wewe ni mwanamke ela yako ni ya kubana.

As long as you are together pesa yote ni ya kwenu. Sidhani mpaka kufikia kutokuaminiana kiasi hicho kuna haja ya watu kuendelea kuishi pamoja while looking at each other with suspicious eyes and mind.

Sijui tufanyaje hapo maana tukitoa wanaenda kutumia na wengine ilobaki tubane tu au?
 
Wewe utakubali wanao wale kisamvu daily na ela unayo? Maana kumbuka kuna watoto si mume peke yake. Utakubali wanao wasome saint Kanumba na pesa ipo simply because wewe ni mwanamke ela yako ni ya kubana.

As long as you are together pesa yote ni ya kwenu. Sidhani mpaka kufikia kutokuaminiana kiasi hicho kuna haja ya watu kuendelea kuishi pamoja while looking at each other with suspicious eyes and mind.
Nitahakikisha mume kama ana kipato tunakitumia effectively, sitatoa mwanya wa mtu mwingine kula kilaini kihivi, pole inaonekana unanyonywa, hata mie najitoaga tu kwa BF
 
Yaani wife amtafutie pesa ya kula na kuhonga hawara zake! Huyo mwanaume hampendi mkewe anamfanya ATM tu. Huyo mama avunje ukimya,kisipoeleweka a move on amuache jamaa na hawara yake wakajipange Ubungo mataa kwa ajili ya kuanza rasmi kazi ya kuombaomba.
 
huwezi ukajua unaweza ukakuta rafiki wa dada yako huko aliko naye anatembea na mtu wake au boss.
 
Back
Top Bottom