Je Huu ni Mfumo Mpya wa Demokrasia?

Mzozo wa Mizozo

JF-Expert Member
May 26, 2008
426
12
Hivi karibuni katika Chaguzi mbalimbali za viongozi wa Juu wa nchi [Marais] barani Africa kumekuwa na malalamiko ya kwamba chaguzi hizo hazikuwa za huru na haki na kwamba wale ambao walitangazwa kama Washindi walifanya hayo kwa hila nasi washindi halali. Hapa ni kwamba wale viongozi ambao wapo madarakani wanafanya yote ambayo wanaweza kuhakikisha ya kwamba wanaibna uhuru wa Mwananchi kumchagua kiongozi ambaye atawaongoza

Ukiangalia katika kipindi hiki ambacho Demokrasia ya Kweli ni kati ya vile ambavyo vitachangia katika Siasa Safi na Uongozi Bora, hali kama hii ama niseme Style mpya ambayo wanasiasa wetu wameanza 'kuiaddopt' wakikazana kuunda serikali za Umoja wa Kitaifa [Power Sharing Deals]kwa mtazamo wangu inapoteza maana halisi ya Demokrasia katika Utawala.

Kenya walifanya kitu hicho, Odinga akaishia kuambulia uwaziri mkuu, tukakaa kwa Muda kisha Bob na Morgan Tvg. Kama haitoshi naona Zanzibar nao wameanza kuongea kwamba tuige mfano wa Kenya na Zimbabwe katika harakati za kumaliza mgogoro ambao umekuwa unafukuta visiwani toka 2005 mara baada ya Uchaguzi.

Hapa nakuja na kujiuliza jambo moja, je huu ni mfumo mpya wa Demokrasia ambapo waliopo madarakani wanaiba uhuru wa Wananchi kuchagua viongozi kisha wale viongozi ambao hawajachaguliwa wanajaribu kupata 'Piece of the Pie' kwa kutaka kuwe na Serikali za Umoja wa Kitaifa. Sera za hawa Viongozi huwa zinalenga mabadiliko au zinalenga kuwa na nafasi kati ya Watawala wa Nchi?

Je hii ni Demokrasia ya kweli na kama ndio mwelekeo wake halisi ni upi? Zinatujenga hizi Siasa?

"Should we continue aiming for the moon and hoping to land among stars?"
 
Back
Top Bottom