Je huku ni kuwajali wananchi?

Jidu

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
1,232
754
Jana kwenye taarifa ya habari ya channel 10 kuna habari ya kusikitisha juu ya wananchi wa serengeti ambao wanapakana na hifadhi hiyo,Kundi kubwa la tembo limevamia na kuharibu ekari nyingi za mazao yao ambayo walitegemea kuvuna kati ya majuma 2-3 yajao,lakini ndoto hizo zimefutika ghafla baadya ya wanyama hao waharibifu kuteketeza mazo yao.na hakuna juhudi yeyote ya kuwafidia wakazi hao juu ya uharibifu huo.kingine nilichosikia kuwa ikitokea mnyama ameua binadamu basi serikali hutoa kifuta machozi cha Shilingi 20 tu!wapi thamani ya binadamu na mnyama?
 
Ah, hata mimi nashangaa. Mapato yanayopatikana kwenye mbuga huchukuliwa na serikali, sasa kwa nini maafa kama hayo yanapotokea tusigawane keki ya taifa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom