Je hili nalo lisemwe na nani?

vukani

JF-Expert Member
Dec 30, 2009
245
165

Ni siku ya Ijumaa niko ofisini kwangu nimekaa nikiendelea na kazi zangu kama kawaida mara napata mgeni. Mgeni huyu ni rafiki yangu Farida mwenyeji wa kule Arusha niliyesoma nae kidato cha tano kule Morogoro, ingawa baadae mimi nilihamia shule ya binafsi hapa jijini Dar es salaam na kumuacha rafiki yangu kule Morogoro akiendelea na kidato cha sita.

Ni takribani miaka mitatu imepita bila kuonana na rafiki yangu huyu kwani kwa mara ya mwisho tulikutana pale baraza la mitihani mwenge wakati tulipofuatilia result slip zetu.

Ilikuwa ni furaha isiyo kifani kukutana na rafiki yangu huyu ambaye wanafunzi wenzetu walikuwa wakituita pacha wakidai eti tunafanana. Tangu wakati huo tulipoachana pale baraza la mitihani hatukuwahi kuonana wala kuwasiliana.

Nilimuuliza Farida kwamba yuko wapi na anafanya nini? Simulizi zake ndio zilizo nifanya nipate mada ya kuweka humu leo. Ukweli ni kwamba jambo ninalotaka kuzungumzia si geni sana kwa wasomaji wa jamii forum, kwani ni jambo ambalo lipo sana, labda tu niseme kuwa siku za hivi karibuni limezidi kukua tena kwa kasi ya ajabu. Nimeona kama tusipolisemea sisi wanawake, hali inaweza kuwa mbaya sana hapo baadae.

Baada ya kumaliza kidato cha sita Farida hakupata alama nzuri za kumuwezesha kujiunga na chuo kikuu, lakini hata hivyo aliamua kujiunga na chuo cha Kimoja maarufu hapa jijini (Naomba nisikitaje) ili kusoma masomo ya biashara na masoko.
Chuoni hapo Farida alikutana na unyanyasaji mkubwa wa kijinsia, ambao ni vigumu mtu kuamini ukisimuliwa. Vinara wakubwa wa unyanyasaji huo wa kijinsia ni walimu, kwani wakimtaka mwanafunzi hawatarajii kukataliwa na kama mwanafunzi akimkataa mwalimu atarajie kufeli katika somo la mwalimu huyo.

Farida anabainisha kuwa kuna ushirikiano mkubwa miongoni mwa walimu katika kuwafelisha wanafunzi jeuri wasiokubali kutoa penzi kwa walimu hawa wakware, na cha kushangaza hata walimu wa kike ambao ndio wangekuwa msaada kwao lakini hali haiko hivyo nao wanashirikiana na walimu wa kiume kuwakandamiza wanafunzi wa kike.

Ingawa amefanikiwa kumaliza na kufaulu lakini haikuwa rahisi sana kwani ilimlazimu kurudia masomo mawili zaidi ya mara mbili ili kuweza kufaulu. Naamini wote mtakubaliana na mimi kuwa unyanyasaji wa kijinsia upo sana, na sio tu kwenye Elimu bali pia kwenye ajira kuanzia serikalini hadi kwenye sekta binafsi kote huko hapafai kumechafuka ile mbaya.

Swala hili limekuwa ni gumu kushughulikiwa kisheria kutokana na matukio mengi ya namna hii kutoripotiwa katika vyombo vya dola kutokana na kwanza Polisi wetu kutoyapa uzito unaostahili matukio ya namna hiyo na pia waaathirika kuona aibu kuripoti juu ya udhalilishwaji wanaofanyiwa kwa kuhofia swala hilo kuripotiwa kwenye vyombo vya habari na hivyo kuogopa kuchekwa na jamii. Tatizo lingine ni mazingira ya kupatikana kwa ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani wahusika kutokana na vitendo hivyo kufanywa kwa usiri mkubwa.

Inapotokea mwalimu anamfanyia mwanafunzi wake vitendo vya unyanyasaji kijinsia au kumbaka, inakuwa ni vigumu kwa mwanafunzi kutoa taarifa kwa sababu anamuona mwalimu kama ndiye ameshikilia mustakabali wake wa maisha kielimu.

Kusema ukweli athari ni kubwa sana kuliko tunavyofikiria kwa sababu wanafunzi wengi wa kike wanaathirika kwa kupata ukimwi, au maradhi mengine ya zinaa au kupata ujauzito na kuachishwa shule, na matokeo yake wanafunzi hawa huumia ndani kwa ndani na kupata matatizo mengi ya kiakili.

Hata wakuu wa shule au vyuo vyenye unyanyasaji huu wa kijinsia wakiulizwa mara nyingi hukanusha vikali kuwepo kwa tatizo hilo katika shule zao au vyuo vyao, zote hizo zikiwa ni juhudi za makusudi kulinda umaarufu wa shule au chuo husika.

Hebu muulize mwanamke yeyote wakiwemo wale ambao wanashikilia nafasi za juu serikalini kuhusu jambo hili, kama hutashangazwa na kile utakachosikia kutoka kwao, utakuta kama hawakukutana na udhalilishwaji wa kijinsia walipokuwa shule ya msingi, sekondari au chuoni basi itakuwa ni katika ajira, kote huko hapafai, hali ni mbaya kweli kweli. Sasa sijui na hili gonjwa la ukimwi, tutapona kweli?

Nilipoamua kujiajiri niliangalia mambo mengi na hili likiwemo, ingawa mimi haikunitokea kwa kiwango cha Farida.

Ukweli ni kwamba kuna aina nyingi za unyanyasaji wa kijinsia lakini nitaelezea aina tatu za unyanyasaji wa kijinsia ambao ndio ulioshika kasi hapa nchini.

Aina ya kwanza ni unyanyasaji wa mwanamke kuombwa rushwa ya ngono. Hapa mwanamke analazimika kumkubali mwanaume ili apate haki yake. Kwa maana kwamba mwanaume ananufaika kwa kumpata mwanamke ili amsaidie kupata huduma fulani ambayo ni haki yake.
Aina ya pili ni ile ya kumnyima raha mwanamke kwa kumnyanyasa mara kwa mara au hata kumpa adhabu isiyostahili kwa kosa dogo , kwa sababu tu alimkataa mhusika kimapenzi.
Aina hii hutokea sana mashuleni na vyuoni, na hii inawaathiri sana wanafunzi wa kike kisaikolojia, kwa sababu uwezo wao kimasomo unashuka na wakati mwingine kushindwa kuendelea na masomo.

Aina ya tatu ni ile ya kumtomasatomasa, kumbusu, kushika sehemu za siri au hata kumfanyia mwanamke vitendo vya kimapenzi bila ridhaa yake. Vitendo vya namna hii mara nyingi vinafanyika kama utani, hasa huko maofisini.
Mara nyingi mwanamke anayefanyiwa vitendo vya namna hii asipoonesha kukerwa ndivyo mhusika atakavyoendelea kumfanyia vitendo vya udhalilishaji zaidi, ambapo kuna uwezekano mkubwa wa kumfedhehesha ndani ya jamii .

Unaweza kushangaa kuona kwamba miongoni mwa waathirika wa unyanyasaji wa aina hii ni wake za watu ambao wameshindwa kujistahi kwa kutoweka mipaka ya utani. Unyanyasaji wa aina hii unaweza kuepukwa kabisa kama sio kukomeshwa kabisa iwapo tutaweka mipaka ya utani.
Kujistahi ni jambo la heshima sana na mwanamke yeyote anayeweka msimamo wake wazi kwa kumkemea mwanaume yeyote anayejaribu kumfanyia vitendo vya udhalilishaji wa aina hii, bila kujali kuwa ni mwalimu wake au mkubwa wake kikazi, anakuwa anajijengea heshima kubwa.

inaonekana rafikiyo hakuwa mzuri darasani na si kusingizia unyanyasaji wa waalimu.
 
Hata mimi nakubaliana nawe mkuu,vitu hivi vinavyafanyika vyuoni na makazini lakini watu wanavifumbia macho kama hawavioni.Wa kulaumiwa sana ni wanawake wenyewe,kuna sheria ya makosa ya kijinsia iliyorekebishwa mwaka 1998(SOSPA),ile sheria imelalia upande wa wanawake zaidi,maana inamuumiza hata mwanaume anaemkonyeza mwanamke bila ridhaa yake,nilitegemea baada ya ile sheria kupitishwa hayo mambo yangeisha.Lakini wanawake,sijui wana nini,Wanafanyiwa mambo ya aibu kila kukicha na hawaripoti.
 
kaka VUKANI,
Nafurahi sana leo umeeleweka mkuu.
Maximum respect to you.
 
Back
Top Bottom