Je hii ni sawa waungwana?

Nyakwaratony

JF-Expert Member
Dec 21, 2011
573
140
Mamboz! Naombeni ushauri juu ya hili……. Juma na Asha ni wapenzi, Juma anafanya kazi Mkoani Dodoma, Asha anafanya kazi Mkoani Tanga. Sasa kuna rafiki yake ya Asha anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni. Asha amemwambia Juma ambaye ni mpenzi wake kuwa "mwezi ujao nitakuja Dodoma kwenye harusi ya rafiki yangu flani naomba twende wote harusini".

Juma akamjibu Asha mimi sitakwenda kwa sababu sipendi kwenda kwenda kwenye sherehe, vile vile Juma akamuuliza kwani hiyo harusi yafanyika sehemu gani yaan mtaa gani? Asha akamjibu sijajua make kadi ya harusi sijapewa ila nikipewa nitakujulisha.

Sasa Asha anaomba ushauri je ni haki kwa Juma kutomsindikiza Asha harusini kwa kigezo kwamba hapendi kwenda kwenye sherehe? Je ni haki Asha aende kwenye sherehe pekeyake afu arudi mida ya usiku wa manane kama mjuavyo harusi huwa zinachelewa kuisha. Naomba wewe mchangiaji ujiweke katika position ya Asha au ya Juma kisha unishauri.

Asanteni!!!!!!!
 
Wapendwa cjawapata kabisaaaaaaaa!

nyakwaratony nango yawa.hapo juma kuna kitu anajaribu kuficha.labda ana ka kiburudisho hapo dom ataki asha agundue,cha msingi asha aende.afikie pale kwa juma,then amlazimishe waende.tuone itakuaje.
 
Amwambie pole pole atamuelewa yeye mtu wa pwani hakosi lakumhashua mpaka Juma akakubali.
 
asha aende tu dodoma lakn apokelewe na juma na wakae wote mpaka mda asha atapoenda harusini, pia juma amsindikize huko harusini na harusi ikiisha juma lazima aende kumchukua asha na kumrudisha nyumbani! juma akikataa na hili pia basi asha aandike hana chake hapo!
 
asha aende tu dodoma lakn apokelewe na juma na wakae wote mpaka mda asha atapoenda harusini, pia juma amsindikize huko harusini na harusi ikiisha juma lazima aende kumchukua asha na kumrudisha nyumbani! juma akikataa na hili pia basi asha aandike hana chake hapo!
Umesomeka ndugu yangu...... Senkyuuuuuuuuuuu!
 
Back
Top Bottom