Je hii ni sahihi? Naomba msaada!

brownuli

Member
May 21, 2008
7
0
Kwa muda mrefu tangu nakua nimekuwa niksikia watu wengi wanapozungumza kiswahili hupenda kuweka neno "ga" mwisho wa neno..mfano Alikwenda wao husema "Alikwendaga" sasa hapo nimekuwa nikijiuliza je ni kiswahili sahihi au la? na swali langu lingine ni hili.. hivi nikifika dukani na ninapotaka kuulizia kitu ipi ni lugha sahihi kati ya hizi, mfano 1. bei gani?? au 2. kiasi gani? naomba msaada jamani.
 
....ga, ni ya wasukuma wew. si kiswahili sahihi

bei gani? au kiasi gani?
Jibu

bei gani? = hiki kiswahili sahihi.
kiasi gani? = maanake ni kuwa unauliza ununua kiasi gani cha bidhaa, na si kuwa unauliza bei. mfano: sukari kiasi gani?= kilo ngapi?, kopo ngapi, vibaba vingapi n.k

Nadhani umeelewa ndg yangu msukuma.
 
"Alikwendaga" ni kosa la kisarufi lililozoeleka. Usahihi ni "alikuwa akienda". Huu ni wakati uliopita katika hali isiyodhihirika. Uulizapo "bei gani?", unapenda kufahamu inauzwa kwa kiasi gani cha fedha, na uulizapo "kiasi gani?", unapenda kufahamu ina ujazo au uzito gani.
 
Bei gani ni sahihi zaidi, na hii ndiyo anayopaswa kuuliza mnunuzi au mlipaji, lakini kiasi gani ni sahihi pia ikiwa itaulizwa na muuzaji au mtoa huduma, mfano "umenipa kiasi gani (cha pesa)?

Mara nyingine utamsikia muuzaji anamuliza mnunuzi, hasa makonda wa daladala, "umenipa bei gani"?, wakati walipaswa kuuliza "umenipa kiasi gani"?
 
Kama nitakuwa nimekuelewa vizuri si sahihi wanavyotumia hilo neno "ga" mfano..nakulaga, naendaga,napendaga, nakunywaga, hii "ga" inatumika mahali si pake japokuwa inaeleweka lakin sio kiswahili sanifu

Kwa muda mrefu tangu nakua nimekuwa niksikia watu wengi wanapozungumza kiswahili hupenda kuweka neno "ga" mwisho wa neno..mfano Alikwenda wao husema "Alikwendaga" sasa hapo nimekuwa nikijiuliza je ni kiswahili sahihi au la? na swali langu lingine ni hili.. hivi nikifika dukani na ninapotaka kuulizia kitu ipi ni lugha sahihi kati ya hizi, mfano 1. bei gani?? au 2. kiasi gani? naomba msaada jamani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom