Je hii kauli ya "2015 ni zamu ya Wazanzibar" ina mkono wa JK?

Kwa mtazamo wangu kama hizi hisia zipo basi zitakuwa zinasukumwa na siasa uchwala za makundi na uwoga wakufanya maamuzi magumu kama ilivyotokea kwenye uteuzi wa spika,si mliona mizengwe iliyofanyika dakika za mwisho kutoka hata kusikojulikana ilikuja formula mpyaaaaa ya kupokezana zamu kwa jinsia katika mihimili mitatau ya dola sijui ilitoka wapi?. sasaili kuepuka haya makundi yaliyoanza kujianisha katika kuelekea 2015, kwa kifupi linatafutwa jibu jepesi kwa maswali magumu ili kuahairisha tatizo(mpambano) na kuondoa lawama kwa wanamitandao wote. But time will tell.
 
Tuache huu ujinga. Hatuwezi kufanya kama Tanzania Visiwani kwamba wamewapa wapemba! Tanzania ni bora sana kuliko ujinga huu wa kizazi hiki. Naona sasa nchi inahitaji dikteta ili urudi kwenye mstari.
 
Hapana;tumewatawala lini?Wao mara zote wamekuwa na raisi wao;lakini wao ndio wametawala Tanganyika mara moja;mzanzibar Mwinyi akatawala Tanganyika!Hatutaki utapeli huu utokee tena!!!

Samahani kidogo,na wewe ni great thinker?hivi bado mpaka leo kuna watu hawaelewi Tanzania ni muungano wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar?kweli elimu ya uraia imepwaya sana basi!Kijana sikiliza kulikua na nchi kama nilivyozitaja hapo juu,nchi hizo wakuu wake (sio) wananchi wakaamua kuziunganisha na kuunda serikali moja ikiitwa Tanzania,ila bahati mbaya kwetu wa bara na nzuri kwa wazenj rais wao kidogo alikua na fikra pana akasisitiza yeye serikali yake itabaki,akamshauri na mwenzake wa bara asiivunje serikali yake,wabara akawa mbishi akasema hawa watu wangu hawahitaji serikali,tutashare hii ya muungano,hivyo ndivyo ilivyokuwa,sisi kiongozi wetu hakuyasimamia maslahi yetu kwenye muungano ipasavyo,kwa hiyo hapa cha kufanya ni kuidai kwa nguvu zote serikali yetu ya Tanganyika sio kutaka kujifanya eti hatujui kwamba hii ya muungano ni ya kushare kwa kuwa ni ya wote!huo ndio ukweli najua mengi huyajui wakubwa zako wanakuficha waulize eti kwanini rais wetu aliivunja serikali ya tanganyika wakati rais wa zanzibar hakuivunja serikali ya yake licha kuingia kwenye muungano?
 
CCM ikiamua kwamba ni zamu ya mgombea wao atoke Znz basi itambue kwamba imeshindwa hata kabla ya kuanza kampeni. Maana uchakachuaji na wizi wa kura bado kura hazitatosha!
 
acha upuuzi wako watanganyika zami yetu lini kukalia ikulu ya zanziabar hivi watanganiyka mnaelewa maana ya zamu
 
hivi kuna kikundi cha watu wanoamua Raisi wa nchi hii. kama wapo hii ni hatari kubwa. hebu tuamke ikulu isiwe na mwenyewe tena pawe ni mahali pa viongozi waadilifu tu.
 
hivi kuna kikundi cha watu wanoamua Raisi wa nchi hii. kama wapo hii ni hatari kubwa. hebu tuamke ikulu isiwe na mwenyewe tena pawe ni mahali pa viongozi waadilifu tu.
 
hao ni ccm wanatafuta mgombea wao. Nchi hii tuna vyama vingi vya siasa, wao ccm wakiweka mgombea wao kwa ubara na uzanzibar sisi watanganyika tutampigia kura mgombea anayefaa toka vyama vingine. Hakuna haja kuumiza vichwa na hii ccm.
 
hao ni ccm wanatafuta mgombea wao. Nchi hii tuna vyama vingi vya siasa, wao ccm wakiweka mgombea wao kwa ubara na uzanzibar sisi watanganyika tutampigia kura mgombea anayefaa toka vyama vingine. Hakuna haja kuumiza vichwa na hii ccm.

hicho ndio tunapaswa kukizungumza pamoja na kudai serikali yetu ya tanganyika irejeshewe,sio kudandia serikali ya muungano na kutaka kuifanya eti ndio ya tanganyika,huo ni uongo wa kitoto!
 
Watu wanao tetea siasa za Zanzibar na Tanganyika, wengi ni Wazanzibari - wenye uroho wa madaraka wanahisi serikari ya muungano inawafunga speed governor.
Njaa ya madaraka hata kama inawa cost kizazi na vizazi itakusadia nini? wakati kata miaka ya kuishi uliyo bakisha kama unayo mingi ni 30??

1. Ki msingi Tanzania tunaendela vizuri katika ku-integrate uislam wala u-kristo, na ukabila in 20 years to come utakuwa umeisha!! - hizi ni dini za kuletwa tuu, babu zetu wahakuwa nazo!! [Big up Nyerere kwa hili linalo wasumbua hata Kenya, laiti ungalikuwepo maneno yako ya 1995 yange-dhihirika] - Mtu anayetaka tumia hizi silaha tatu ni **** sana na hatufai!!

2. Tunatakiwa kutumia fursa ya katiba mpya kufuta traces za Zanzibar na Tanganyika ndo tutaendelea! Nchi nzima igawanywe katika majimbo na Zanzibar iwe jimbo! kama USA [inakuwaje mie niko Mbeya, au mtwara kuhu, mkuu eti mtu mmoja huko Dar ananiteulia Mkuu wa mkoa, Wilaya, RDD, etc] na tuwe na serikali ya shirikisho, Wazanzibar watagombea kama wengine na watachaguliwa kwa uwezo wao tuu.

3. Scenario ndogo tu! Hivi hasa hao Wanzanzibari wenye kidomo domo, kama huu muungano ukivunjika kwa chochoko zao, hao Wanzanibar woote wanao ishi bara na mali zao tukiwatimua huko Zanzibar bado kutawatosha???

If you think big you will see how this thing is irreversible! even if forefathers erred in the terms on the Union!! karibu April 26th
 
Hivi ni nani wanaoonekana waroho wa madaraka tukiutizama mfano mdogo tu wa hizi harakati za wanaotajwa tajwa kuusogelea urais wa Tanzania kati ya ndugu zetu wazanzibari na sisi ambao tayari tumekikalia kiti mara 2 mfululizo kupitia mkapa na kikwete huku tukikikalia pia kiti cha uwaziri mkuu kwa miaka mingi wakati wenzetu walikaa mara moja tu tena kwa muda mfupi kwenye kiti hicho kupitia Salim A.Salim aliemrithi sokoine?tafakari vizuri hapa.

Na ndugu zangu sisi watanzania bara kwanini tunapenda sana kupotosha mambo kwa kujaribu kutishia eti kama muungano unavunjika leo(mungu apishie mbali) eti wazanzibari tutawapakiza kwenye meli na kuwarudisha kwao?!!hii inashangaza sana kuona inazungumzwa na great thinker!!!hivi mmewahi kujiuliza kwanini kuna wachina,wahindi,wakenya.waganda,wanyarwanda n.k. wanaishi na kumiliki mali hapa Tanzania?je mnadhani labda nchi hizo nilizozitaja tuna muungano nazo ndio maana raia wake wako hapa na wanamiliki mali?
 
Tatizo hapa ni katiba. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio huyo huyo anakuwa rais wa Tanganyika.
Kwa kuwa Zanzibar ina rais wake na kwa sasa ni nchi hivo kuwa na rais toka Zanzibar kuwa rais wa Jamhuri itakuwaje?
Katiba mpya ni lazima irekebishe hili........
TAFAKARI EE MTANGANYIKA.
 
... Scenario ndogo tu! Hivi hasa hao Wanzanzibari wenye kidomo domo, kama huu muungano ukivunjika kwa chochoko zao, hao Wanzanibar woote wanao ishi bara na mali zao tukiwatimua huko Zanzibar bado kutawatosha???
Mbona wabara mnawalazimisha Wazanzibar kuwasaidia? Ni sawa na mke anaomba talaka unamwambia sitaki, nikikuacha utapata tabu, nooo, toa hiyo talaka tuone kama hata survive kivyake.

Hii hoja ya Watanzania bara kuwatisha Wazanzubar inanishangaza sana. Ina maana sisi tuko kuwabeba Wazanzibar tu? Hakuna faida tunayopata, ni sisi kuwasaidia Wazanzibar? Well, hawataki, Wazanzibar wenyewe wanasema kama tunawaona ni mzigo basi tuwatue! Kwa nini mnawalazimisha Wazanzibari Muungano? Kwa Wazanzibar Muungano sio lazima.


CUF2.jpg
 
Hili la kuchoma Qur'ani Takatifu kwa kweli si jambo jema lakini naomba niwatetee hawa jamaa wa Mwanza. Hawa watu walipinga bet katika ubishi, Waislam wakadai ukichoma Qur'ani haishiki moto na ikiungua unakufa hapo hapo. Jamaa akabisha akasema mi naiwasha na inaungua na sifi. Wakamwambia choma.

Jamaa akawasha kiberiti, Qur'ani kama tunavyojua kama Biblia imetengenezwa kwa makaratasi ya miti hii hii ya kawaida ya mpapule, ikaanza kushika moto, mara Qur'ani nyakanyaka. Waislam kusubiri jamaa a drop dead, wanaona jamaa hafi, ikabidi jamaa awaulize, bado muda gani umebaki wa kusubiri nianguke, naweza kuondoka? Si ndo Waislam wakaita Takbir! wengine wakaitikia Alahu Akbar! wakaanza kumchapa Mkristo, Mkristo akawachomoka, na anapumua mpaka leo. Sasa kwa kweli hapo sijui tuseme mkosi nani.

basi ni balaaa!!!!!
 
Si kupeana... Hata Kama hauna ushindani upate tu??
Ni muda wao kupigania, unadhani why watakosa wakati muda bado......!!!!!
Alf kupata wao ni kwamba hakuna mgombea wa bara wanastopishwa?
Ingia ktk ushindani na ushinde hii si nchi ya vijiti Bali abayeshinda ataongoza hata kwao angekuwepo mwenye ubavu aaaaah anapata hata wakitokea Mara 3..
 
Mnaona wenzetu wanajitambua na kuzidai haki zao (Taifa lao litambulike zaidi ndani ya muungano),wanatumia kila mbinu kufikisha ujumbe kwa wakubwa ikiwemo kutumia mabango,vipeperushi n.k. lakini sisi bado tumelala usingizi,hatuwahoji viongozi wetu kuhusu Tanganyika yetu walikoipeleka,kwanini lakini hatufanyi hivyo nani katuloga?Je ni Julius Nyerere?lakini kama ni yeye huo uchawi gani aliotumia usioisha au kupungua nguvu?mnaona wenzetu kwa mapenzi waliyonayo kwa taifa lao wako tayari hata muungano ufe zanzibar ibaki lakini sisi ni kinyume,tunaipenda Tanzania(muungano) kuliko Tanganyika...!!!Jamano wabara wenzangu hakuna Tanzania(muungano) bila tanganyika na zanzibar!tusitafute pa kutokea pengine njia iliyopo ni kuing'ang'ania serikali ya Muungano iturejeshee Tanganyika yetu kama ilivyowapa wazanzibari zanzibar yao,twende zanzibar ikiwezekana tukajifunze wenzetu wanatumia mbinu gani mpaka wanafanikiwa kwenye mambo yao ya kudai haki za taifa lao katika serikali ya muungano?Kama muungano ni wa kuua taifa letu la Tanganyika na sisi tuseme ni bora usiwepo yaani sio lazima kama Tanganyika haipo,kujivunia serikali ya mungano wa tanganyika na zanzibar bila ya kuwa na Taifa letu ni unyonge,tuililie Tanganyika kuliko urais wa serikali ya muungano ambao wazanzibar nao wana haki sawa na sisi!
 
wana jf ukweli ni kwamba hakuna zamu, urais wa tanzania sio zawadi na hajazuiwa mtu kutoka znz au bara kugombea, we mwaga longolongo tunakuchagua na angalizo kama znz watataka kupewa bure tutamaliza karne hajatokea huko......
 
we mwenyewe hujitambui si unaona ulivyojichanganya hapo kwenye maandishi yako,unasema mikoa ya kaskazini haijatoa rais kwa nini iwe zenj,lakini hapo hapo unajisahau na kurudi kusema niache kushabikia "nchi" (sio mkoa)jirani.....zanzibar ni nchi jirani tuliyoungana nayo mzee sio mkoa kama mikoa ya kaskazini,jitambue kwanza kabla ya kuleta hoja,ukweli uko pale pale hamna jinsi tunaweza kuukwepa,zanzibar wanastahili na wao kuenjoy matunda ya muungano wetu ikiwemo kukalia kiti cha urais wa serikali ya muungano wa Tanganyika na ZANZIBAR!

ni zamu ya tanga,kilmanjaro manyara na arusha
 
Back
Top Bottom