Je hii kauli ya "2015 ni zamu ya Wazanzibar" ina mkono wa JK?

wanachoma Qur'an Tukufu wakati Waislam hawajawahi kuchoma Biblia
Hili la kuchoma Qur'ani Takatifu kwa kweli si jambo jema lakini naomba niwatetee hawa jamaa wa Mwanza. Hawa watu walipinga bet katika ubishi, Waislam wakadai ukichoma Qur'ani haishiki moto na ikiungua unakufa hapo hapo. Jamaa akabisha akasema mi naiwasha na inaungua na sifi. Wakamwambia choma.

Jamaa akawasha kiberiti, Qur'ani kama tunavyojua kama Biblia imetengenezwa kwa makaratasi ya miti hii hii ya kawaida ya mpapule, ikaanza kushika moto, mara Qur'ani nyakanyaka. Waislam kusubiri jamaa a drop dead, wanaona jamaa hafi, ikabidi jamaa awaulize, bado muda gani umebaki wa kusubiri nianguke, naweza kuondoka? Si ndo Waislam wakaita Takbir! wengine wakaitikia Alahu Akbar! wakaanza kumchapa Mkristo, Mkristo akawachomoka, na anapumua mpaka leo. Sasa kwa kweli hapo sijui tuseme mkosi nani.
 
Hata wao wazenj wanajuta this time kujaribu kuwaachia jk kwa kutumia kigezo cha kutopeana zamu,lakini nchi tumeiharibu sisi wabara kupitia mkapa wetu na jk wetu ndio kaja kuua kabisa,ngoja wao wakae wajaribu kurekebisha,unajua wazenj na matatizo yao yote la ufisadi tunawafunika,sisi wabara tukipata nafasi huwa tunakula kupita kiasi,wao hawana sana tatizo la ufisadi,ili tupone mgombea wa ccm atoke kwao..!

Kim Kardash,

Inaonekana wewe umetumwa na Wazanzibara.
Kwenye Katiba hichi kitu hakipo. Si Katiba ya Serikali ya Baraza la Mapinduzi wala Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Angalia Katiba zinasemaje kuhusu Rais wa JMT anachaguliwa vipi. Siyo mtu unakuja kubwabwaja hapa kama vile umetumwa kupiga debe kwa ajili ya Wapemba na Waunguja kuhusu Urahisi wa Muungano.

Rais wa JMT atachaguliwa kulingana na Katiba ya JMT na si vinginevo.
 
Kama ni hivyo na sie wabara zamu yetu kuwa rais wa zanzibar,huyu rais wa huku ni wa JMT(si tunamchukulia kama Rais wa Tanganyika aka Tanzania Bara)

sasakwa nini Sisi Wa Tanganyika tumeishika Zanzibar hatutaki kuwachia nchi yao wawe kivyao...kwa sababu sheria inasema Muungano wa nchi mbili lazima iwe equality kwa kila upande....
nitarudi baadae:A S 465:
 
Basi ikiwa hivyo safari hii rais wa Zanzibar atoke Tanganyika. Kulingana na katiba ya Zanzibar "Zanzibar ni nchi. Iweje raia wa nyingine akalie kiti nchi nyingine? We need Tanganyika government back kabla hatujafikiria kupokezana uraisi wa muungano. After all hatutakiwi kumchagua mtu kwa utanganyika au uzanzibar wake ila kwa kuwa anafaa kutuongoza regardless anatoka zanzibar au tanganyika. Ni mtazamo wangu.

Nani atadai Tanganyika back? Wazanzibari? au wabara(watanganyika)?

Tanganyika gvt, tutaidai kutoka kwa nani? anothe G55? Au wananchi wa BARA(Tanganyika) tunapaswa kuidai kupitia katika kutoa maoni ya kuandika Katiba Mpya?

Hata hivyo, Muungano wa Tanzania si muungano wenye muundo uliozoeleka katika aina ya miundo ya muungano duniani.
Lililo wazi ni kuwa hatukuunganisha kila kitu. Tuliunganisha baadhi ya mambo. Leo yanaitwa mambo ya Muungano.

Cooper hoja yako hapa ina udhaifu mmoja tu. Unasahau kuwa Wazanzibari wanadai kukalia kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano na sio Urais wa Tanganyika.

Kauli ya "we need Tanganyika gvt back" ni hoja ya msingi na kwa kila mtanganyika anayetaka kuona utata wa Muungano unaondolewa na kuweka mipaka inayojulikana baina ya serikali ya Tanganyika, serikali ya zanzibar na serikali ya muungano.

Yes, we need Tanganyika gvt back!

Mwalimu Nyerere alishasema-

"Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika ..." Uk 11

Link utaipata hapa https://www.jamiiforums.com/interna...a-maendeleo-afrika-mashariki.html#post1941107
 
jamani mbona mzee wetu na baba wa taifa letu alishatufundisha jinsi ya kumchagua rais wetu wa jamuhuri ya muungano wa tanzania. Nawakumbusha hapa "tusimchague mtu kwa uzanzibari wake au utanganyika wake. Tukifanya hivyo basi tutakuwa tumekiuka miiko na tumekaribisha dhambi ya ubaguzi" hapa yatupasa tumchague mtu kwa uwezo wa kiuongozi na si sifa nyingine.

Hivi hawa viongozi wetu huwa wanamuenzi mwalimu jk kwa lipi? Mboona kwa hili mwalimu alishatupa muongozo? Tuache ubaguzi jamani, hapa tuangalie sifa tu na wala si uzanzibar au utanganyika. Mbona tunapenda sana kujadili vitu visiokuwa na maslahi kwa taifa letu? Mnataka kuniambia matatizo tulionao sasa kama taifa dawayake ni kuwa na rais mzanzibar? Jamani tubadilike kifikra na kiakili pia. Tuache kuwa na fikra chakavu na hulka ya kibaguzi.

tatizo yanayosemwa ni ya mdomoni tu. Mioyoni hao viongozi wana yao.
 
Huu mjadala inabidi usubiri kukamilika kwa katiba mpya na muundo wa muungano utakaoafikiwa. Hata hivyo, harakati za Zanzibar kujidhihirisha kama nchi ilhali hatma ya Tanganyika (Tanzania bara) ikiendelea kuwa gizani ndani ya muungano huu inaondoa uwezekano wa Rais wa JMT kutoka huko (Znz). Nadhani hata mabosi wa CCM wana akili ya kutosha kuona kwamba mgombea wa Zanzibar ana nafasi finyu sana ya kukubalika katika Tanganyika ya leo.

 
Last edited by a moderator:
musiwe na wasiwasi. Maadamu kuna nchi mbili wenye muungano feki na maraisi pia watakuwa feki. Ali Hassan Mwinyi sio mzanzibari kwa hivo kama munataka ukweli ni kuwa hajatokea Raisi Mzanzibari na kama hamuwezi kukubali ukweli, zanzibar irudi kuwa taifa huru na tanganyika irudishiwe uhai wake.
 
Kim Kardash,

Inaonekana wewe umetumwa na Wazanzibara.
Kwenye Katiba hichi kitu hakipo. Si Katiba ya Serikali ya Baraza la Mapinduzi wala Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Angalia Katiba zinasemaje kuhusu Rais wa JMT anachaguliwa vipi. Siyo mtu unakuja kubwabwaja hapa kama vile umetumwa kupiga debe kwa ajili ya Wapemba na Waunguja kuhusu Urahisi wa Muungano.

Rais wa JMT atachaguliwa kulingana na Katiba ya JMT na si vinginevo.


No sijatumwa na yeyote bali i believe in liberties na pia usawa,haiingilii akili kwamba eti wabara ndio tuna akili nyiiiingi sana za kutawala kama sio kuongoza kuliko wenzetu wa upande wa pili,haya mambo ndio yanawafanya wenzetu kusononeka kila siku na kutuona kama tunawaburuza,hali hii ndio inasababisha kutoaminiana,tensa wenzeti mi nawapongeza wamekuwa wastahamilivu sana kutuvumilia,maana baada ya mkapa kumaliza wangeweza kufanya "fujo" ,lakini kuonyesha wana nia njema na muungano wakaacha tukae sisi kwa mara nyingine tena,sasa kwa nini na sisi tusijifunze hii kutoka kwao,kwani na wao wakikikalia iko kiti safari hii tupungukiwa nini,hebu tuweni fair kidogo jamani,waumini wote wa usawa kutoka huku bara tuungane kuhakikisha dhuluma hii dhidi ya wazanzibari kutokana na uchache wao inakoma mara moja,nyerere angekuwapo hii asingeikubali,kwanini tunajina sisi ndio bora zaidi,kwanini tunakua hivi watu wa bara?haifurahishi hata kidogo.Fikirieni mara mbili ingekua sisi ndio tunafanyiwa hivi na wazanzibari tungekubali?kuna mabo mengi wazanzibar wanalalamika chini chini mfano nafasi ya waziri mkuu nayo pia kwanini toka akalie mzanzibari mmoja bwana salim hajakaa mungine tena?uvccm miaka kibao wazenj walikua hawajakalia kiti cha uenyekiti pale toka akikalie mzee wangu SEIF KHATIB miaka ileeee,juzi ndio akaja kukaa huyu masauni tena baada ya sisi wa bara kupigana vikumbo sana ndio jakaya ili kuepusha balaa la umoja huo kugawanyika akaja na kete hiyo ya basi kiti hiki kiende zanzibar kupesha shari,nini kilitokea,masauni alikikalia kwa mwaka mooja kama sio miwili kutokana na wingi wetu tukamtoa sasa tunakikalia sisi kwa mlango wa nyuma kupitia makamu mwenyekiti BENNO!What is this?
 
acha kauli za ajabu wewe.nani kakuambia urais wa hii nchi ni wa kupeana kama pipi?
mikoa ya kaskazini ya tanganyika yenye watu wengi washatoa rais?au kanda ya kati yenye watu wengi zaid ya hao wazenj washatoa rais?
ACHA KUSHABIKIA NCHI JIRAN YA ZENJI,MAMBO YA TANGANYIKA TUACHIE WATANGANYIKA


we mwenyewe hujitambui si unaona ulivyojichanganya hapo kwenye maandishi yako,unasema mikoa ya kaskazini haijatoa rais kwa nini iwe zenj,lakini hapo hapo unajisahau na kurudi kusema niache kushabikia "nchi" (sio mkoa)jirani.....zanzibar ni nchi jirani tuliyoungana nayo mzee sio mkoa kama mikoa ya kaskazini,jitambue kwanza kabla ya kuleta hoja,ukweli uko pale pale hamna jinsi tunaweza kuukwepa,zanzibar wanastahili na wao kuenjoy matunda ya muungano wetu ikiwemo kukalia kiti cha urais wa serikali ya muungano wa Tanganyika na ZANZIBAR!
 
mkuu, naomba wewe kama ni mwanachama wa chama cha siasa, pigania chama chako kiweke mgombea toka zanzibar.

Wapiga kura wa jamhuri ya muungano wataamua kumchagua huyo au mgombea mwingine watakayempenda aliyesimamishwa na vyama vingine period.

kama unanisoma vizuri utagunduakwamba mimi namzungumzia rais tanzania kupitia ccm kwa kuwa naamini ndio wamiliki wa huu muungano,vyama vingine vingi havina shida na muungano na vingine vimeapa kuuvunjilia mbali,sijishughulishi na hivyo ambavyo kwanza vingine vimekuwa na wagombea wa kudumu wa nafasi ya urais,kila siku ni hao hao,sasa ni ngumu kuwabadilisha watu wa aina hiyo,ndio mana nimejikita kwa mgombea wa ccm,nyie waumini wa tanganyika kuonyesha hasira zenu kama ccm watasikiliza kilio changu na kumsimamisha mzanzibari basi pigieni wagombea wengine ambao wa vyama vingine ambao watakua sio wazanzibari,that's very simple hatuna haja ya kuhitilafiana hapa...liko wazi,ila ccm kuonyesha wana nia njema na ndugu zetu wa upande wa pili,safari asimame mzanzibari!Huo ndio ukweli japo hatupendi kuusikia wabara tulio wengi.
 
Zanzibar haitusadii chochote sisi Watanganyika,waacheni wajitenge then tuanze kukata huduma zinazoenda huko toka Tanganyika moja baada ya nyingine,vijana wa Tanganyika wana mahitaji makubwa ya mikopo ya elimu ya juu wakati pesa zao zinapelekwa Zanzibar,umeme unatoka Tanganyika,Elimu wana tegemea Tanganyika, wanaleta wabunge wao kwenye bunge letu kushiriki kutunga sheria hata zile zisizoihusu Zanzibar, wakati hakuna mbunge hata mmoja toka Tanganyika anayeingia baraza la wawakilishi. Kuna mambo mengi ambayo tumewavumilia sana ambayo yanavunja katiba ya inayoitwa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Zanzibar wana katiba yao inayotamka wazi kuwa ni nchi. Kwa hiyo ni kitu cha ajabu kwa watu wa nchi nyingine kuanza kuota ndoto za kwenda kutawala nchi nyingine! Chama cha Mafisadi (CCM) wakijaribu hilo wajiandae kuangushwa na kubeba fedha zao walizokusanya toka EPA,KAGODA,MEREMETA,IPTL RICHMOND,BUZWAGI NK mbali kabisa na IKULU YETU.

zanzibar ni nchi na ndio mana ikazaliwa Tanzania ambayo ni muungano wa nchi mbili TANGANYIKA NA ZANZIBAR! Sasa unyonge wetu cc wabara kutoidai serikali yetu tusitake kuwaadhibu wao kwanini wana serikali yao,tujihukumu sisi kwa nini hatuna serikali yetu?je ni wao wamekataza sisi tusiwe na serikali yetu kama wao?jibu hapana.Sasa kwanini sisi mpaka leo hatuna serikali halafu tunjaribu kufanya jitihada za makusudi kutaka kuijfanya eti serikali ya muungano iwe ndio serikali ya Tanganyika,huo ni uongo,tuitafute serikali yetu ya tanganyika iliko,wala sio hii ya muungano,hii ni ya wote.
 
Mkuu Kim Kardash, this is becoming boring! Si lazima ujibu kila post hata kama hauna jipya.

1. Wewe si Mtanzania Bara kama unavyodai. Uwe mkweli ujisemee kwa uwazi.
2. Suala unalopigania halina msingi wa katiba.
 
Mkuu Kim Kardash, this is becoming boring! Si lazima ujibu kila post hata kama hauna jipya.

1. Wewe si Mtanzania Bara kama unavyodai. Uwe mkweli ujisemee kwa uwazi.
2. Suala unalopigania halina msingi wa katiba.

No hili lazima tuliseme kwa nguvu ili watu waelewe,sisi waumini wa haki na usawa this i s very disturbing kwetu,unazungumzia katiba,sawa,hata katiba pia haisemi safari hii akiwa rais muislam safari inayofuata awe mkristo(mkatoliki) lakini hiyo ndio hali halisi,sio kila kitu lazima ukione kwenye katiba hasa katika nchi zetu hizi za dunia ya tatu,sometimes ni busara ya kawaida tu hutumika mzee.

Halafu kwa nini wabongo mwanangu mtu akiwa anatetea kitu tofauti tu hata kama kina ukweli mnapenda kusema basi "wewe sio mwenzetu(si mtanzania bara) au wewe unatumika",kwanini hamuamini mtu anaweza kutofautiana na nyie kutokana na reality tu bila kusukumwa na kitu chochote?je ni kwa kuwa mara nyingi watz mawazo yetu huwa ni ya kusukumwa sukumwa tu bila kupima jambo kwa akili zetu au?
 
Je kwanini Wazenji waliisigina nafasi yao 2005 wakamwachia JK?
 
Je kwanini Wazenji waliisigina nafasi yao 2005 wakamwachia JK?
kwa sababu ya hila na ujanja wetu sisi watu wa bara,safari hii tusifanye tena hila,tuwaache na wao wakikalie iko kiti then na sisi tutakaa baadae,hatuwezi kutawala pekeetu lazima tushirikiane tena ikiwezekana safari hii hata cha uwaziri mkuu wakikalie pia,yani wakalie vyote urais na uwaziri mkuu kama ccm itashinda sisi tukalie cha umakamu wa rais maana na sisi hatujakionja hicho toka mfumo wa vyama vingi uanze!
 
Mambo ya urais wa JMT yapo kwenye katiba co ujanja ujanja wa kuachiana kishkaji hakuna zamu ya m2 kwenye katiba bara hata 2kipiga miaka 50 fresh 2 sisi hatuna rais wetu wa Tanganyika huyo wa JMT ndio huyo huyo rais wa Tanganyika 2nawaachiaje wazenj na wao wa2achie urais wao 2015
 
Hebu tujaribu na hili. Ikiwa sisi ni nchi moja basi yafaa sasa tukapata rais wa Zanzibar kutoka Tanganyika. Huu mjadala nao uanze
 
Hebu tujaribu na hili. Ikiwa sisi ni nchi moja basi yafaa sasa tukapata rais wa Zanzibar kutoka Tanganyika. Huu mjadala nao uanze
Hilo tumejaribu ni gumu,tatizo sisi hatujitambui wenzetu ilikuwaje wakawa na serikali na sisi nyerere akatudanganya tuivunje ya kwetu tukakubali?sisi tuandamane kuidai serikali ya tanganyika na wazenj wameahidi kutusupport sisi tu ndio tumelala usingizi kwa ujuaji wetu,wazenj wengi mimi nimesoma nao chuo na wanapenda kweli na sisi tuwe na serikali yetu na huwa wanatushangaa kwa nini hatuidai....
 
hii hali ya watanganyika kutotaka kutawaliwa na wazenj imeanza baada ya sisi wabara kuwatawala jamaa kwa awamu mbili mfululizo au?

Hapana;tumewatawala lini?Wao mara zote wamekuwa na raisi wao;lakini wao ndio wametawala Tanganyika mara moja;mzanzibar Mwinyi akatawala Tanganyika!Hatutaki utapeli huu utokee tena!!!
 
Back
Top Bottom