Je hii kauli ya "2015 ni zamu ya Wazanzibar" ina mkono wa JK?

Yaani tupoteze miaka kumi kwa sababu hiyo hapo juu? Ze last taim tulipotumia vigezo vya ajabu ajabu kama hicho ulichotaja kilichotokea wote ni mashahidi. Mimi sitampigia mtu kura eti kwasababu anatoka sijui wapi, oh kwasababu huko sijui wapi hawajakalia kiti muda mrefu, NO! Na kama CCM watamsimamisha mtu kwa kigezo hicho, mbona oltenativu zipo nyingi?

Hata wao wazenj wanajuta this time kujaribu kuwaachia jk kwa kutumia kigezo cha kutopeana zamu,lakini nchi tumeiharibu sisi wabara kupitia mkapa wetu na jk wetu ndio kaja kuua kabisa,ngoja wao wakae wajaribu kurekebisha,unajua wazenj na matatizo yao yote la ufisadi tunawafunika,sisi wabara tukipata nafasi huwa tunakula kupita kiasi,wao hawana sana tatizo la ufisadi,ili tupone mgombea wa ccm atoke kwao..!
 
Basi ikiwa hivyo safari hii rais wa Zanzibar atoke Tanganyika. Kulingana na katiba ya Zanzibar "Zanzibar ni nchi. Iweje raia wa nyingine akalie kiti nchi nyingine? We need Tanganyika government back kabla hatujafikiria kupokezana uraisi wa muungano. After all hatutakiwi kumchagua mtu kwa utanganyika au uzanzibar wake ila kwa kuwa anafaa kutuongoza regardless anatoka zanzibar au tanganyika. Ni mtazamo wangu.

upotoshaji jazz band..........
 
Mbona kihoro. 2015 ni mbali sana kuweni na subra.

Ndio mimi nawashangaa hawa wabara wenzangu,wanagombania ndizi wakati mgomba sio wao safari hii,wenye mgomba wametulia tuli...wao tu ndio kutwaa kupita pita na kujaribu kupindisha ukweli ama kwa hakika hiki ni kihoro na kihoja pia!
 
Kama ni hivyo na sie wabara zamu yetu kuwa rais wa zanzibar,huyu rais wa huku ni wa JMT(si tunamchukulia kama Rais wa Tanganyika aka Tanzania Bara)

tatizo letu sisi hatujitambui,tunachotakiwa kuandamana na kukidai ni serikali yetu ya tanzania bara,lakini tumelala usingizi,tunadhani eti serikali ya muungano ndio yetu,hapana tunakosea,hii ni ya wote ndio maana na wao wamo,ile ya kule ni yao ndio mana sisi hatumo,mbona hii ni rahisi sana kwa great thinker kuielewa tusiwe kama wasomi wa darasa la elimu ya watu wazima,hili liko wazi
 
kuna mkrsito mwanasiasa wa kuwa rais znz? maana sasa ni zamu ya mkristo hakuna cha zamu ya zanzibar wala nini condition ya kwanza awe mkristo aliyempokea yesu kama mwokozi wa maisha yake!

mnataka mkatoliki mwingine tena?wakatoliki na waislam inatosha sasa,this time ni mzanzibari hata awe hana dini,yupo salimm A salim,yeye si muislam wala mkristo ni mjamaa kama kingunge na jenerali ulimwengu,huyu anafaa kama issue ni uislam!
 
Mara kadhaa nimekuwa nikipata kushawishika kwamba kutokana na kelele za wazanzibari na hasa hawa wanaotukana viongozi wetu wa upande wa Tanganyika, ni muda muafaka kuuvunjilia mbali huu muungano ili kila mmoja achukue hamsini zake. Naamini kwamba Tanganyika itakuwa nchi bora sana bila wazanzibari.

Lakini kwa upande mwingine nikijaribu kuwatazama wazanzibari, jinsi wanavyobaguana wenyewe kwa wenyewe, waunguja kujiona superior kwa wapemba, na nikikumbuka fukuto la wapemba kudai nchi yao ya pemba, ninapata shaka juu ya mustakabali wa uwepo na umoja wa wazanzibari nje ya muungano, nakubaliana na maneno ya baba wa taifa kwamba nje ya muungano hakuna wazanzibari, kuna wapemba na waunguja!!

Na nikijaribu kuwatazama hawa wazanzibari waliojazana huku Tanganyika nashindwa kufahamu hatma yao kama muungano ukivunjika. Ni heri tuendelee na huu muungano ili kulinda ustawi wa wazanzibari kwa pamoja, ingawa watanganyika tutaendelea kuwabeba na kuwavumilia na matusi wanayotutukana.

Back to the topic, uraisi wa Tanzania hauwezi kuzungushwa toka bara kwenda zanzibar. Kama kuna mzanzibari anajiona ana uwezo wakuiongoza JMT anaruhusiwa kuingia kwenye mchakato, si suala la kuachiana ama huruma. Hatuwezi kuiweka nchi rehani ili tu kuwafurahisha watu fulani fulani.

Kuna kitu kimoja wabara tunachanganya,nani kakwambia kwamba muungano ukivunjika wazenj watapakiwa kwenye meli kubwa kurudishwa kwao,hapa wapo wakenya,wachina,waarab n.k. mbona hatuna muungano nao na wanaendelea kuishi hapa,hii iondoe akilini mwako kwanza,duniani unaweza kuishi popote pale mradi unafuata sheria za hapo ulipo ikiwemo kulipa kodi mbalimbali n.k.we need tax payer and investors here mzee na wafanyakazi pia ndio mana kuna wakenya n.k wanafanya kazi hapa.

N a pili kwa nini kila tu jamaa wanapokumbushia umuhimu wa wao pia kufaidi matunda ya muungano ikiwemo kukikalia iko kiti ndio mapenzi yenu kwa tanganyika yanazidi,kuna nini hapa kimejificha?
 
Haina mkono wa mtu bali ndio hali halisi wabara tuache kujipenda kupita kiasi,huu ni muungano wa nchi mbili wenzetu wametuvumilia mara mbili,kwa mkapa na kwa huyu kikwete tuwe waungwana this time na wao wakikalie iko kiti then kitarudi bara tena tatizo liko wapi...

Tatizo ni kuwa mzanzibari sasa hivi sio raia wa Tanzania, mtu wa bara sio mzanzibari. Kama mzanzibari akiwa rais, basi hata mwethiopia ruksa kuwa rais Tanzania!
 
Jamani mbona mzee wetu na baba wa taifa letu alishatufundisha jinsi ya kumchagua rais wetu wa jamuhuri ya muungano wa tanzania. Nawakumbusha hapa "tusimchague mtu kwa uzanzibari wake au utanganyika wake. Tukifanya hivyo basi tutakuwa tumekiuka miiko na tumekaribisha dhambi ya ubaguzi" hapa yatupasa tumchague mtu kwa uwezo wa kiuongozi na si sifa nyingine.

Hivi hawa viongozi wetu huwa wanamuenzi mwalimu jk kwa lipi? Mboona kwa hili mwalimu alishatupa muongozo? Tuache ubaguzi jamani, hapa tuangalie sifa tu na wala si uzanzibar au utanganyika. Mbona tunapenda sana kujadili vitu visiokuwa na maslahi kwa taifa letu? Mnataka kuniambia matatizo tulionao sasa kama taifa dawayake ni kuwa na rais mzanzibar? Jamani tubadilike kifikra na kiakili pia. Tuache kuwa na fikra chakavu na hulka ya kibaguzi.

Hamna kitu sipendi kama mtu anapoongelea mambo ya hii Nchi na kuchukua quotes of Dead one. Hivi Watanzania uwezo wetu wa kufikiri na kuamua mambo ukomo wake ni kwa The late JK Nyerere?

Hivi hatuwezi kufikiri na kuamua mambo kwa uwezo wa zaidi ya the Late JK?
 
Tatizo ni kuwa mzanzibari sasa hivi sio raia wa Tanzania, mtu wa bara sio mzanzibari. Kama mzanzibari akiwa rais, basi hata mwethiopia ruksa kuwa rais Tanzania!

Nani kawavua huo uraia,au ni serikali ya halmashauri ya kichwa chako ndio imeamua hivyo?mbona tuna makamu wa rais mzenj kwanini isiwe kwa rais?fikiria mara mbili.
 
Hakika wachangiaji wanapochangia jambo lolote la Kiislam wamekua mara zote wakiwatukana Waislam.Wanawatukana Waislam,wanachoma Qur'an Tukufu wakati Waislam hawajawahi kuchoma Biblia,wanamtukana Mtukufu Mtume(amani iwe juu yake na aali zake watoharifu) wakati Waislam wanamheshimu Yesu(amani iwe juu yake).Kwann Wakristu wanawachukia Waislam kiasi hiki.Lakini Watukanaji wanaufahamu Uislam?Wamesoma chochote kuhusu Uislam?Na kama wamesoma, wamesoma toka kwa watu sahihi au kutoka kwa maadui wa Uislam?.Mmoja kawanasibisha Waislam na uchawi,majini,ushoga,madawa ya kulevya.Je anajua anachokiandika?.Uchawi ulikuwepo tangu enzi za Nabii Musa (amani iwe juu yake) haelewi?Majini yametajwa ktk Biblia na kipo kisa cha Yesu(amani iwe juu yake) cha kutoa mapepo na kuamuru wawaingie nguruwe.Hujui hili au Waislam walikuwepo enzi za Yesu(amani iwe juu yake)?Na kuhusu ushoga wangewauliza Waanglikana labda chuki zenu zitapungua.Ni Obama na Cameroon wanaotaka 'tuoane'(Mwenyezi Apishie mbali) kwa jina la haki za binadamu.Je Watukanaji hawatumii akili?Ama madawa ya kulevya wazalishaji wakuu Mexico.Kauze madawa China,Iran au Hijaz uone cha mtema kuni.Eti utambulisho wa Waislam ni ufukara !!Ni nani amewaloga Watukanaji? Hivi wamekwenda Indonesia,Malasia.Jamhuri ya Kiislam ya Iran,Hijaz Libya Oman kwa kutaja chache sana wakauona huo ufukara?Huu wa hapa una historia yake.Nyie mnaojiita wasomi,sifa ya msomi ni kukataa ukweli?Hawaisomi historia?Na matusi ni dhihirisho la kuishiwa hoja.Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Zaidi

hakuna mkristu anayewatukana waislam ila nyie ndo chanzo cha choko zote duniani.wapi mkristu anajitoa mhanga,mkristu yupi ni gaidi,pirates?mko kama mapepo hamna haya
 
2015 zamu ya wakristo membe sio mkristo tunaujua huo mkakati wa majina na wale wanafunzi mlio wasomesha chuo kikuu tunajua yote! Muda ukifika tunalipua. Awamu ya zanzibar walimpigia zengwe salim. Jk akachukua. Mmekwisha kama muungano utavunjwa kwa urais na uvunjwe tu
 
hakuna mkristu anayewatukana waislam ila nyie ndo chanzo cha choko zote duniani.wapi mkristu anajitoa mhanga,mkristu yupi ni gaidi,pirates?mko kama mapepo hamna haya
Una hakika na unachokiandika?.Chuki uliyo nayo haikupi hata nafasi ya kufikiri kidogo.Sikushangai maana imesemwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.Pia mjinga huamini kila kitu.Hongera zako ww uliye kama malaika.
 
Kuna kitu kimoja wabara tunachanganya,nani kakwambia kwamba muungano ukivunjika wazenj watapakiwa kwenye meli kubwa kurudishwa kwao,hapa wapo wakenya,wachina,waarab n.k. mbona hatuna muungano nao na wanaendelea kuishi hapa,hii iondoe akilini mwako kwanza,duniani unaweza kuishi popote pale mradi unafuata sheria za hapo ulipo ikiwemo kulipa kodi mbalimbali n.k.we need tax payer and investors here mzee na wafanyakazi pia ndio mana kuna wakenya n.k wanafanya kazi hapa.

N a pili kwa nini kila tu jamaa wanapokumbushia umuhimu wa wao pia kufaidi matunda ya muungano ikiwemo kukikalia iko kiti ndio mapenzi yenu kwa tanganyika yanazidi,kuna nini hapa kimejificha?
Mkuu, naomba wewe kama ni mwanachama wa chama cha siasa, pigania chama chako kiweke mgombea toka Zanzibar.

Wapiga kura wa Jamhuri ya Muungano wataamua kumchagua huyo au mgombea mwingine watakayempenda aliyesimamishwa na vyama vingine period.
 
Zanzibar haitusadii chochote sisi Watanganyika,waacheni wajitenge then tuanze kukata huduma zinazoenda huko toka Tanganyika moja baada ya nyingine,vijana wa Tanganyika wana mahitaji makubwa ya mikopo ya elimu ya juu wakati pesa zao zinapelekwa Zanzibar,umeme unatoka Tanganyika,Elimu wana tegemea Tanganyika, wanaleta wabunge wao kwenye bunge letu kushiriki kutunga sheria hata zile zisizoihusu Zanzibar, wakati hakuna mbunge hata mmoja toka Tanganyika anayeingia baraza la wawakilishi. Kuna mambo mengi ambayo tumewavumilia sana ambayo yanavunja katiba ya inayoitwa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Zanzibar wana katiba yao inayotamka wazi kuwa ni nchi. Kwa hiyo ni kitu cha ajabu kwa watu wa nchi nyingine kuanza kuota ndoto za kwenda kutawala nchi nyingine! Chama cha Mafisadi (CCM) wakijaribu hilo wajiandae kuangushwa na kubeba fedha zao walizokusanya toka EPA,KAGODA,MEREMETA,IPTL RICHMOND,BUZWAGI NK mbali kabisa na IKULU YETU.
 
Haina mkono wa mtu bali ndio hali halisi wabara tuache kujipenda kupita kiasi,huu ni muungano wa nchi mbili wenzetu wametuvumilia mara mbili,kwa mkapa na kwa huyu kikwete tuwe waungwana this time na wao wakikalie iko kiti then kitarudi bara tena tatizo liko wapi...
acha kauli za ajabu wewe.nani kakuambia urais wa hii nchi ni wa kupeana kama pipi?
mikoa ya kaskazini ya tanganyika yenye watu wengi washatoa rais?au kanda ya kati yenye watu wengi zaid ya hao wazenj washatoa rais?
ACHA KUSHABIKIA NCHI JIRAN YA ZENJI,MAMBO YA TANGANYIKA TUACHIE WATANGANYIKA
 
Back
Top Bottom