Je haya MADISH ya "tv'' ni analog au digital ?

Kivia

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
278
32
Ndg zangu naomba kujulishwa je haya madish ya tv yapo ktk mfumo gani ni analog au digital ?. Na je pindi serikali itakapostopisha mitambo ya analog, je na wenye madishi itabidi wanunue vingamuzi au wataendelea kupata channel kama kawaida ? Kwa anayejua naomba msaada.
 
Ni Digital na yataendelea kutumika Daima, tatizo ni vituo vya TV's vitaendelea kurusha matangazo yake "free on air" ili tuendelee na Satelite Dish au watauza matangazo yao kwenye Ving'amuzi...
 
  • Thanks
Reactions: GM7
kwanza ktk nchi za wenzetu wanatumia both ditital na analogue kaka hata ktk cable zao utaona kuna digital na analogue channels. kwa bongo ni blahblhah tu itachukua mda kuingia full digital lkn mitambo hiyo hawatazima mwisho wa mwaka huu kama wanavodai, miundo mbinu ya digital haijakaa vema na wanatakiwa kuwa na service provider walau mmoja ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa garama za vingamuzi,wanapaswa hao wa vingamuzi kuweka channel zote za tanzania na za nje wataamua wenyewe na mwananchi awe na uchaguzi,hili la tbc na clouds afu star na itv wawe na vingamuzi vyao TCRA wamekurupuka waende shule wakasome ICT.
 
Mkuu receiver ndio zinakuo digital au analog lakini kwa siku hizi receiver nyingi ni digital hivyo bado tutahitaji sana madish, ili kupata matangazo ya masafa marefu hata kama provier watakuwa ktk digital na wanatoa vin' gamuzi.
 
kwanza ktk nchi za wenzetu wanatumia both ditital na analogue kaka hata ktk cable zao utaona kuna digital na analogue channels. kwa bongo ni blahblhah tu itachukua mda kuingia full digital lkn mitambo hiyo hawatazima mwisho wa mwaka huu kama wanavodai, miundo mbinu ya digital haijakaa vema na wanatakiwa kuwa na service provider walau mmoja ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa garama za vingamuzi,wanapaswa hao wa vingamuzi kuweka channel zote za tanzania na za nje wataamua wenyewe na mwananchi awe na uchaguzi,hili la tbc na clouds afu star na itv wawe na vingamuzi vyao TCRA wamekurupuka waende shule wakasome ICT.

Hata mimi naona hawa jamaa sijui vipi. Agape Television Network wana king'amuzi chao cha TING, TBC nao wana king'amuzi chao cha Startimes ambapo ndani yake unapata TBC1, TBC2, Ch10, Clouds tv, Haya sasa Na hawa ITV, Star TV wana mpango gani, je na wenyewe wataweka ving'amuzi vya kwao?

Hiii ina maana kama unataka kuangalia chaneli zote za Tanzania uwe na ving'amuzi vingi? na wakati huohuo kila king'amuzi kuna malipo yake ya kila mwezi ili kupata chaneli hizo.

Ningekuwa mimi ndio TCRA ningeamua kuweka TV zote katika king'amuzi kimoja tu. Kwanini wasifanye hivyo? ndio maana tunasema wamekurupuka.
 
kwanza ktk nchi za wenzetu wanatumia both ditital na analogue kaka hata ktk cable zao utaona kuna digital na analogue channels. kwa bongo ni blahblhah tu itachukua mda kuingia full digital lkn mitambo hiyo hawatazima mwisho wa mwaka huu kama wanavodai, miundo mbinu ya digital haijakaa vema na wanatakiwa kuwa na service provider walau mmoja ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa garama za vingamuzi,wanapaswa hao wa vingamuzi kuweka channel zote za tanzania na za nje wataamua wenyewe na mwananchi awe na uchaguzi,hili la tbc na clouds afu star na itv wawe na vingamuzi vyao TCRA wamekurupuka waende shule wakasome ICT.
bnyar mchga

haya maoni ni ya habari mchanganyiko an si ya kitekniki.
 
Serikali wanampango wa kuongeza wigo wa kodi kupitia ving'amuzi. Si vibaya lakini inaonekana kama hawajajipanga. Sasa watu itabidi wanunue ving'amuzi zaidi ya kimoja ili kuweza kuangalia chaneli zote za ndani. Hizi zote ni gharama zinazoweza kuepukwa kama wangekuwa wamepangilia vizuri.
 
Back
Top Bottom