Je, hawa wote ni wana CHADEMA?

Jeho

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
5,053
5,503
Habarini wana jukwaa, kwa muda mrefu sijashiriki katika jukwaa hili ingawa mara kadhaa nimekuwa nikiingia kama mgeni, kuna jambo ambalo nahitaji undani wake kama kuna mtu ambaye atakuwa anaelewa kwa undani, kwanza nianze kwa kusema kama mada hii imeshawahi kuwasilishwa humu jukwaani basi sijawahi kuiona kutokana na kutoingia jukwaani mara kwa mara.
Jambo hilo ni kuhusu wanafunzi waliofukuzwa katika chuo cha UDOM, ifahamike kwamba mnamo mwezi wa sita wanafunzi wa college ya social sciences pamoja na college ya natural science and mathematics walifukuzwa chuoni. Mnamo mwezi wa nane wanafunzi wa college ya social sciences walirudishwa kufanya mitihani ya kumaliza semister ya pili, lakini wale wa college ya natural science and mathematics mpaka leo hawajaitwa, wanafunzi hao ni kutoka kozi ya Bsc in Statistics mwaka wa kwanza wakati huo pamoja na kozi ya Bsc in Mathematics mwaka wa kwanza vilevile na hawa sio kozi nzima bali ni takribani wanafunzi arobaini na mbili. Au ndo kusema hao wote ni wanachama wa Chadema?
 
Chadema inahusika vipi na ule mgomo. Ni kwamba waliotimuliwa ni wanafunzi wa Udom waliochochea mgomo usio na tija not otherwise.
 
Hata kama hawakuwa full CDM serikali ya leo tayari imewaandaa wawe full CDM makamandas...mkuu CCM ya leo ni anti-vijana wasomi,haulijui hilo??
 
Mliorudishwa pigeni shule mkimaliza kaanzisheni matawi ya CDM kwa wingi, Nyinyi mnashindwa kula na vipofu waacheni wawasomeshe then njooni kwa wingi CDM
 
Back
Top Bottom