Sn2139
JF-Expert Member
- Apr 9, 2010
- 834
- 250
Ndugu wana JF, salaam aleikum ...
Leo nimejiuliza swali nikaona niwashirikishe na wengine ili nipatae msaada. Kuna mfululizo wa matukio yamekuwa yakitokea nchini mwetu na kuzifanya siasa za nchi kuwa mpya, kutisha na kuvunja moyo. Je nani anaweza kutoa forecast ya siasa za Tz miaka miwili ijayo? Tukizingatia matukio yafuatayo.
Leo nimejiuliza swali nikaona niwashirikishe na wengine ili nipatae msaada. Kuna mfululizo wa matukio yamekuwa yakitokea nchini mwetu na kuzifanya siasa za nchi kuwa mpya, kutisha na kuvunja moyo. Je nani anaweza kutoa forecast ya siasa za Tz miaka miwili ijayo? Tukizingatia matukio yafuatayo.
- Nyerere anang'atuka kuongoza nchi
- Alhaji A. H. Mwinyi anakuwa raisi wa JMT
- Katibu Mkuu wa Chama Marehem Kolimba anataka Katiba ya Nchi irekebishwe ili kuruhu rais kutawala zaidi ya vipindi viwili
- Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi anakamata madini ya thamani yakitoroshwa nchini kupitia AirPort
- Mh BW Mkapa anakuwa Rais wa JMT
- Mwl JK Nyerere anafariki dunia katika hospital ya St Thomas huko Uingereza
- NBC inabinafsishwa
- Mashirika ya umma yanauzwa kama ni amri kutoka mbinguni Kiwira,
- Nyumba za serikali zinauzwa kwa namna isiyokubalika....
- Polisi inaua raia 23 huko Pemba
- Tanzania yazalisha wakimbizi kwa mara ya kwanza, wengine Somalia na wengine Mombasa na Uingereza
- Mh JM Kikwete anachaguliwa kuwa rais wa JMT kwa kishindo
- Ufisadi wa kutisha EPA wabainika
- Richmond, Dowans, IPTL
- Idadi ya wapiga kura yashuka kwa mara ya kwanza kutoka wastani wa 78% hadi 42% ?
- Rais wa nchi aanguka hadharani mara tatu !!!!
- NEC yatumika kuchakachua kura
- Nchi nzima yagubikwa na vuguvugu la kulalamikia uhalali wa matokeo ya wabunge, Mwz, Shy, Morogoro, Dsm, Mby nk
- Uchaguzi wa Meya wa Arusha, Mwz, Kigoma nk utata
- TANESCO yaamuriwa na ICC kulipa DOWANS Bilioni 185 na Serikali yasema ni Bilioni 95
- Waziri wa serikali aishauri serikali yake isilipe pesa hizo, Mwanasheria mkuu wa Serikali asema serikali lazima ilipe. Waziri wa nishati anasema serikali inajiandaa kulipa haraka pesa hiyo. Waziri wa Pesa anasema serikali haina pesa.
- Bei ya umeme yapanda huku mgao ukiongezeka....
- Polisi yakataza mikutano ya CDM nchi nzima
- Polisi yaruhusu maandamano na mkutano wa CDM huko Arusha lakini IGP aibuka ghafla na kuzuia maandamano kwa tangazo kupitia TV na Radio
- Polisi yaua raia waliokuwa wakitembea kwa amani kuelekea kwenye mkutano
- Serikali yaomba kukutana na CDM wazungumze, CDM yakataa
- ....