Je, GEORGE KAHAMA na ANDY YOUNG wamegombana?.. Will IKULU Intervene?!

Haya cheki watu walivyokuwa wana-network! Hiyo Pangea nayo si iliuzwa to Barrick Gold? Maana naona wanaruka hapa,lakini imekuwaje?
The Tanzanian Royalty Management group combines technical, financial and administrative expertise to create shareholder value in the resource sector. We have extensive experience in Africa . Our Chairman and CEO is Jim Sinclair, founder and Chairman of Tanzania American Development Corporation 2000 Limited ("Tanzam2000"), now a wholly owned subsidiary of Tanzanian Royalty. Anton Esterhuizen is a Managing Director of Pangea Exploration (Pty.), a South African company (not related to Pangea Goldfields Inc.) with exploration interests in Africa . Marek Kreczmer is the Company's original founder and has many years of exploration experience in Africa . John Deane has 21 years experience in mining and exploration in Africa.
 
Mzee Game na wengine,

Mmeshawahi kusoma kitabu kinachoitwa Confessions of an Economic Hit Mankilichoandikwa na John Perkins? I can what this chap wrote happening in Tanzania right now. Nchi imekwisha na tunazidi kudidimia kwenye lindi la umaskini isipokuwa "wateule" wachache ambao ni sehemu ya syndicate.
 
Mzee Game na wengine,

Mmeshawahi kusoma kitabu kinachoitwa Confessions of an Economic Hit Mankilichoandikwa na John Perkins? I can what this chap wrote happening in Tanzania right now. Nchi imekwisha na tunazidi kudidimia kwenye lindi la umaskini isipokuwa "wateule" wachache ambao ni sehemu ya syndicate.

Ninacho hicho kitabu na mwanzo nilifikiri kuwa Perkins anaongopa mpaka nilipomuuliza profesa wangu wa economics ambaye alikuwa yuko na jamaa wa WB akaniambia kuwa mengine tusiyoyajua tukijayajua kutatokea WW3

Ndio maana naona watu saa zingine wanapongangania tufafuta mstakabali wa nchi kupitia JF naona duh mbona kazi tunayo?

Hivi unajua kama Muungwana alikuwa halali bila kucheki kinachoendelea humu lakini guess what? washamwambia hakuna kitu atazame MTV CRIBS kisha akalale tuu


Sasa hebu soma hiki kipya cha Naomi Klein,in short kinachoendelea Bongo sasa hivi na jana kule kwenye ule mkutano wa New Orleans vyote vilishatabiriwa na huyu mwanamama



397px-Shock_doctrine_cover.jpg
 
Mzee Game na wengine,

Mmeshawahi kusoma kitabu kinachoitwa Confessions of an Economic Hit Mankilichoandikwa na John Perkins? I can what this chap wrote happening in Tanzania right now. Nchi imekwisha na tunazidi kudidimia kwenye lindi la umaskini isipokuwa "wateule" wachache ambao ni sehemu ya syndicate.

Nimeisoma ndugu yangu! Na kwa kweli inatisha! Lakini mimi nimeamua kuendelea na reasearch yangu nione itatufikisha wapi. Hivi mnajua pia kuwa Balali used to be WB? Sasa mi naona picha imeanza kuja na kukamilika. Kuna watu nchi hii akina Sinclair, Tudor na AY ambao ni hatari kwa nchi yetu, lakini hata hao akina Kahama na Rupia et al! Mi naona tuendelee tu kuweka vituz kuna siku ukweli utaibuka!
 

Ninacho hicho kitabu na mwanzo nilifikiri kuwa Perkins anaongopa mpaka nilipomuuliza profesa wangu wa economics ambaye alikuwa yuko na jamaa wa WB akaniambia kuwa mengine tusiyoyajua tukijayajua kutatokea WW3

Ndio maana naona watu saa zingine wanapongangania tufafuta mstakabali wa nchi kupitia JF naona duh mbona kazi tunayo?

Hivi unajua kama Muungwana alikuwa halali bila kucheki kinachoendelea humu lakini guess what? washamwambia hakuna kitu atazame MTV CRIBS kisha akalale tuu


Sasa hebu soma hiki kipya cha Naomi Klein,in short kinachoendelea Bongo sasa hivi na jana kule kwenye ule mkutano wa New Orleans vyote vilishatabiriwa na huyu mwanamama

Muungwana alikuwa kweli anacheki hapa? Mbona namwona kama he's not tech savvy. Anyway, amekuwa 'weaned off' JF siku za hivi karibuni?

About Naomi Klein kwa kweli dada huyu ninamw-admire sana! Kitabu chake cha No logo nilikisoma 10 years ago ilipotoka and I became a believer. Hiki kitabu kipya nitakitafuta! Thanks for the tip
 

Ninacho hicho kitabu na mwanzo nilifikiri kuwa Perkins anaongopa mpaka nilipomuuliza profesa wangu wa economics ambaye alikuwa yuko na jamaa wa WB akaniambia kuwa mengine tusiyoyajua tukijayajua kutatokea WW3

Ndio maana naona watu saa zingine wanapongangania tufafuta mstakabali wa nchi kupitia JF naona duh mbona kazi tunayo?

Hivi unajua kama Muungwana alikuwa halali bila kucheki kinachoendelea humu lakini guess what? washamwambia hakuna kitu atazame MTV CRIBS kisha akalale tuu


Sasa hebu soma hiki kipya cha Naomi Klein,in short kinachoendelea Bongo sasa hivi na jana kule kwenye ule mkutano wa New Orleans vyote vilishatabiriwa na huyu mwanamama



397px-Shock_doctrine_cover.jpg

Game na wengine, ahsanteni kwa tafiti zenu.

Sasa Game, unaposema kuwa mustakabali wa Taifa hauwezi kupatikana thru JF, jambo ambalo linaukweli ndani lakini sijui ni kwa asilimia ngapi. Hivyo kuna alternative gani unayotupatia sisi iwapo maelezo yako yanayofuatia ni yakutia tamaa na kutufanya tujione mabwege jinsi tunavyozidiwa kete na ma-conspirator kutoka nje, iwapo wewe na wengineo wenye knowledge na exposure kubwa katika mambo haya hamjihimu kutueleza sisi Watanzania, au mtaandika vitabu ku counter conspiracies zao?... Tuelimishane ndugu zangu. Hata kama hakuna linalotendeka hivi sasa, walau tu mambo fulani yatakuwa yamewekwa hapa na kusemeka kwa wengi.

SteveD.
 
Mvua hunyesha tone mojamoja, kamwe hainyeshi kwa kumiminika kama maji ya bomba.
Nguvu ya kunywesha ardhi na nguvu ya uharibifu ya naji ya mvua imo kwenye kila tone lidondokalo.
Tone moja ni hafifu mno kuleta mafuriko au kunywesha mmea mmoja ukastawi.
Tone moja ni kilo ngapi?
Tone likutana na tone ninihutokea?
Matone yote kwa pamoja ndo mvua yenyewe na ndo ubichi wa ardhi ,mtirirko wa mito na hata mafuriko.
Hakuna ajuaaye mnazi mmoja huhitaji matone mangapi ya mvua na ya ujazo gani katika maisha yake yote ili kuzaa nazi bora, wala hakuna ajueaye matone mangapi ya mvua na ya ukubwa gani yatajaza na kuufurusha mto Rufiji.

Kudharau tone moja la mvua na kuyaenzi matone hamsini ni Busara?

Cha ajabu kuhusu matone yatengenezayo mvua ni upana wa madhara yake.

Si ajabu kusikia matone ya Mvua yalodondoka Kilimanjaro yakileta madhara ya mafuriko makubwa huko Tanga au Matone ya mvua ya Iringa na Morogoro yakiwaliza Warufiji.

Mtu mwenye hekima kule Rufiji au Tanga huchukua hatua ya kujihami mara asikiapo kwamba kulikuwa na uwingi wa matone ya mvua huko Iringa au Kilimanjaro.

Matone kidogo ya viwanja vya JF huenda si kitu si chochote kwani mkondo wake haulengi Ikulu.
Kumbuka Tabia moja muhimu ya maji;
Maji huzama ardhini na kusambaa chini kwa chini kisha kuibuka pale penye udhaifu, ni vema kwa mdharau matone kujua hilo.
 
Confessions of an Economic hitman indeed. A book and a half.
GT, nitakitafuta hicho kingine asap. Asante for recommendation.
 
Madela wa Madilu, very poetic! BUt excellent point you make! Mimi sikati tamaa hata kidogo! Naona JF imewezakufanya contribution kubwa sana na mtakuja kuona wote matunda yake in 10 years, when we reflect that the real political reforms in Tanzania started on a virtual forum. For your information many ex-Soviet bloc countries walikuwa na forums za wasomi and that is where the real opposition was born, sasa here we have a virtual forum but serves the same purpose!
JF imetufungua wengi macho, it has made us think, prod and push and question and it has served a noble cause!
 
Capitalism at its best, sorry Imperialism! Sisi bado tupo kwenye Ujamaa jamani, it will take blood to convert into neo capitalism!
 
Kuna wakati flani hivi..mwaka '97 nadhani...Nyerere alikuwa kwenye kipindi cha Q&A cha CNN alichokuwa aki-host Riz Khan. Andy Young naye alikuwa mgeni siku hiyo. Andy aliukandia kishenzi ujamaa mbele ya Nyerere. Siku hiyo Nyerere hakuwa na mengi ya kusema zaidi ya kutolea mifano ya Ukristo na Ujamaa....overall it was a good show. I enjoyed it and felt proud to be a Tanzanian
 
Mimi sipingi Capitalism ila naiogopa Imperialism, ambayo ni hatua ya juu kabisa ya ubepari.
Hata wenzetu hapa Marekani wanaiogopa Imperialism kama Miwaya. Sasa hivi kuna Muswada unapingwa vikali na Baraza la Congress kuhusu kuruhusu TV kubwa kumili Radio na Mgazeti kila State kama MH Mengi wa IPP afanyavyo hapo Tanzania.
Wenzetu wanachoogopa ni kile kile tuogopacho sisi huku dunia ya 3Watu wachache kumiliki Habari na kuwa na uwezo mkubwa wa Kusema watakacho na kupotosha ukweli kwa faida yao kama kundi la wachache.

Ujamaa ulituviza akili, tukabweteka tukadumaa na kuenzi watu kuliko mawazo yao na vitendo vyao.
Leo hii bado tunaongozwa na kundi lile lile la watu wale wale waliodai kwamba
"Ujamaa ndiyo njia pekee ya kutufikisha katika kilele cha Maendeleo"

Sasa hivi wanajifanya ni magwiji wa kujenga siasa ya ubeparina hawataki kusahihishwa, ya kweli hayo?

Au walitudnanganya zamani au wanatudanganya sasa, hakuna zaidi.

Ujamaa ulitufanya tujenge utamaduni wa kuwaamini na kuwaabudu viongozi wa serikali.
Ujamaa ulitujengea nidhamu ya woga ya kukaa kimya hadharani na kuuliza maswali mengi mafichoni au tukiwa vyumbani na wake zetu.
Ujamaa ulitufanya tuelekeze macho yetu na mategemeo yetu serikalini, tulijenga matumaini makubwa na kudhani maendeleo yatapatikana kupitia serikali kuu au kupitia mashirika yake.

Serikali wakati ule ilitufunga macho na masikio tusione kiendeleacho nje ya nchi.
Hata kusafiri kwenda nje mtu alihitaji Satate House Clearance.

Kumwita mwanamuziki toka nje aje atumbuize lilikuwa jambo la Kiitifaki.
Mwaka 1987/88 SISIEMU walimwalika Tabulei wa Afrisa Internasional aje apige Muziki hapo Dar, wakati sasa hivi kila mdongi aweza fanya hivyo, kweli ujinga ulituvaa na sisi tukauvaa.

Sasa milango imefunguliwa, jukumu la serikali ni kusimamia utaratibu kwa misingi ya sheria. Kazi kuu ya serikali si kufanya biashara.

Sielewi kwa nini tumeshindwa kutunga sheria ili kila muwekezaji aingie ubia na mwenyeji?

Mtaji mkubwa wa mwenyeji ungekuwa ardhi.

kwa mfano Kule Buzwagi Barick wangelazimika kuingia ubia na wananchi wote walio hama kuwapisha watajirike. Kazi ya serikali ingekuwa ni kuhakikisha zoezi hilo linafana.

Maana ya ubepari si kuwapa wageni kila kitu, kwani mwishowe watatamani wake na waume zetu tutawapa kwa kusingia Ubepari.

" Du Mtasha alikuja na mshiko wa nguvu kweli! Nikamwazima mke wangu kwa muda wa wiki mbili akalale naye"

UJINGA

Awe Sir GEORGE KAHAMA au mkulima kule kwa Wahangaza wenzie ndiye anafanya shughuli ya kuuza nchi aliyopewa na Mwenyezi Mungu bado ni ujinga tu, hamna akili yeyote katika hilo.

Ujinga ambao tangu tupate Uhuru tumedai kupambana nao vikali sana,lakini inaelekea vita imetushinda.

Kwa wepesi wa tafsiri ya Viongozi wa Tanzania, kufuta ujinga ni kujua kusoma na kuandika, wasitambue kwamba kuna kundi kubwa la watu wasio jua kusoma na kuandika lakini hawamo kwenye kundi la wajinga.
Maana hii nyepesi ililenga zaidi kuwawezesha wao kujiengua katika kundi la wajinga na kupata uwezo wa kunyoshea vidole watu wengine.
Leo hapa JF nawaambia kufuta ujinga ni kujitambua wewe ni nani na jamii yako ambayo ndiyo chimbuko lako ni ipi. Mjinga ni yule asiyeweza kutambua kwao na kuthamini kilicho chake.

Wengine Tumekaa marekani kwa zaidi ya Muongo mmoja na pengine kuiga tabia za kizungu za hapa na pale, hii hatufanyi tujione si miongoni mwa wana jamii tuliyo toka ya Imalinyi na Madilu. Binafsi nitakuwa nimerukwa na akili, kuwekwa msukule na wazungu au nimeolewa kabisa kuwapa kisogo watu wa Imalinyi na Madilu kwa kuwauza kwa namna yeyote ile kwa akina Andrew Young na Mob yake.

Kitendo hicho pekee yake, cha kuuza wana jamii wangu, kitanifanya niwe mjinga hadi siku yangu ya kuonja mauti.

Mtu yeyeote asisingizie ubepari wakati wa jitihada zake chafu za kuweka rehani nchi yetu mikononi mwa Wakoloni mamboleo, ni ujinga wake ndio ufanyao auze wana jamii wenzie.
Mtu huyu ni mjinga na yu kinyume na vita ya kufuta Ujinga bila kujari Elimu yake na heshima aliyojijengea.
Si tatizo la ukoloni mamboleo tuonapo nchi yetu ikinadiwa sokoni, bali ni tatizo la viongozi wetu kushindwa kufuta Ujinga wao katika kipindi chao chote walicho ongoza Taifa.

Wajinga ndio waliwao kila siku.
 
By the way Kahama alipewa huo u knighthood na nani na lini na lipi alilolifanya mpaka apewe huo uknighthood?

Vile vile kisheria huwezi kuitwa sir mpaka uwe raia wa UK sasa madilu hebu tuweke sawa hapa
 
Game Theory,
nakubaliana sana na mchango wako ambao umeenda deep ktk kujaribu kuwaangalia hawa jamaa.
Kifupi nitasema kwamba Andrew Young anaweza kuwa tapeli kama madai ya wengi hasa ambao wanategemea saana huruma na kazi za kanisa wakati dunia ya leo misaada haiwezi kwenda hivyo.
Pamoja na mengi yaliyokwisha semwa mimi naamini kuwa ni watu wachache sana huko je wanao amini kuwa Uchumi wa nchi zetu utapatikana tu ikiwa kuna ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi za nje na sisi badala ya sisi kuwa watumwa ndani ya biashara hizo. Ni Andrew Young na Bill Clinton pekee kati ya hawa wageni wengi wamekuwa na msimamo huo na hasa kauli na mifano kama hii:-

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]"The Third World has paid more money back than they got and in a sense the interest that they've paid is more than the principal they borrowed. And it really is morally unjust," Young said.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]He and Clinton suggested that, once relieved from their heavy debt burden, developing countries should invest in public services such as roads, schools and hospitals. Clinton cited Honduras, where debt relief has enabled the government to increase the number of children's school years from six to nine, and Uganda, where primary school enrollment has doubled, as examples.[/SIZE][/FONT]

Sasa basi pamoja na kwamba Tanzania itajengwa na sisi wenyewe watanzania ni muhimu tukumbuke kuwa maendeleo ya nchi hayatoki ndani peke yake. Dunia ya leo huwezi kufanya kitu bila kushirikiana na serikali ama Taasisi za nje ambazo zinaweza kuku jerk ulipokwama. Hata tukitazama hao Tigers na Malyesia wameweza kufanikiwa kwa sababu ya uchaguzi mzuri wa partner wakaachana na kutegemea sana IMF na World bank. Kuuundwa kwa mfuko wa Asia ambao walitanguliza kwanza imani kuwa nchi hizo haziwezi kuendelea ikiwa zitazidi kujilimbikiza madeni na mikopo yenye riba kubwa, wakajenga chombo kinachowazesha nchi changa kujenga miundombinu, vitu muhimu kama mashule, hospital na barabara, changes ziliweza kuonekana mapema na leo hii hawashikiki tena.
Tanzania tunatakiwa kuchagua rafiki na kama nilivyokwisha sema hata siku moja bepari hawezi kuwa rafiki yako ila anaweza kuwa very friendly nasi kiasi kwamba tukafikiria ndiye mtu bora. Huyo Clinton ndoto za usawa wa kiuchumi hakuzianza jana toka akiwa shule alikuwa akikerwa sana na umaskini wa nchi zetu. Alipopata wadhifa, Clinton he managed kukuza uchumi wa Amerika na Dunia nzima sote tulikuwa tukipeta na hakika ndoto yake iliweza kuonekana dunia nzima pamoja na kwamba haikupendwa na mabepari wengi. Akazushiwa fitna na ndio tukauona mwisho wake, lakini matunda yalikwisha onekana kote.
Hata ukitazama September 11, ni ugonvi kati ya familia ya Bush na Ossama kiuchumi, Huko Iraq ni ugonvi kati ya Bush na Saadam kugombea mafuta. Afghanstan ni ugonvi wa Bush na taliban kuweka bomba la mafuta kwani 100% ya washiriki wa sept 11 walikuwa WaSaudia, how can Afghanstan did became a victim - Yote ilikuwa kazi ya CIA na huyo Bent Scowcroft ni mhusika mkubwa sana.
Nilijua toka mwanzo kuwa hapa kuna jambo na harufu ya mzungu kupindisha uwezo wa Sullivan foundation kwa kutumia jina la Andrew Young hali nia na malengo yao sio mabaya maadam sisi tuko macho na makini.
Kwa hiyo ni muhimu sana kwetu kuchunguza nani rafiki na nani adui yetu.
 
Ndugu yangu,
Mambo ya flani alisema hivi siku ile yashapitwa na wakati, watu wanaangalia matendo na sio "ku-dance kwa lips," maneno aliyosema na ume-quote hapo juu ilikuwa ni "lip service" kwa audiance husika...kuyaamini maneno hayo ni sawa na kujipiga gumba kwenye washeli!!. Huyo mzee ni nishai na chimbuko lake ni civil rights mvt, kwani alikuwa mpambe wa MLK (sasa ana capitalize na ku-abuse legacy ya Dr. King) ....huyu ni sawa na uncle jesse au "makalikiti" sharpton, ambao usema chochote ili waonekane lakini matendo yao ni kinyume kabisa.
Achana na tabia ya kuamini maneno ya flani.......kumbuka senators craig na vitter!!!.
 
YuornameisMINE,
Sawa mkuu ujumbe wako umefika naheshimu mawazo yako na ndio maana wewe una dini yako na mimi yangu vilevile pamoja na kwamba sote ni wamoja....
Tukianza kuchambua imani ya kila mmoja wetu sidhani kama tunaweza pata suluhu.

Pili, nadhani hii ni mada na kila mmoja wetu anayo haki yake kimsingi kueleza yale anayoyafahamu ama kuyaamini nje ya hapo pinga kwa hoja. wapi nimesema uongo ama kupotosha ama anzisha hoja fulani inayopingana na hoja yangu.
 
YuornameisMINE,
Sawa mkuu ujumbe wako umefika naheshimu mawazo yako na ndio maana wewe una dini yako na mimi yangu vilevile pamoja na kwamba sote ni wamoja....
Tukianza kuchambua imani ya kila mmoja wetu sidhani kama tunaweza pata suluhu.

Pili, nadhani hii ni mada na kila mmoja wetu anayo haki yake kimsingi kueleza yale anayoyafahamu ama kuyaamini nje ya hapo pinga kwa hoja. wapi nimesema uongo ama kupotosha ama anzisha hoja fulani inayopingana na hoja yangu.

kama huchaelewa kitu usikurupuke kujibu......sijazungumzia dini mahali popote na kwa taarifa yako nimeshaachana na mambo hayo zamani nimebaki mwislamu jina tu!!!.....ujumbe pale juu upo wazi, kama una muda soma tena, inshallah utaelewa.
 
Actually sikuwa na haja ya marumbano kwa wakti huu wa mwisho wa mwaka na holidayz na ndio maana kwenye ile post sikutaja hata jina lako. Ilikuwa ni kwa kila mtu........message sent!!!!.

Happy Holidayz!!.
 
YournameisMine,
Nimekuelewa vizuri isipokuwa wewe ndio hukunielewa. na wala usije pindisha maneno kuwa hukumaanisha mimi kwani neno -Usiamini kila kitu - mlengwa ni mimi. Na haya sio malumbano isipokuwa ni kufahamishana juu ya personal beliefs...
YournameisMine, Dini imetumika kama mfano kuonyesha kuwa binadmu sisi huamini kile tunachopenda kuamini na wakati mwingi hupenda kutoa makosa upande wa pili hali sisi wenyewe imani yetu ina mapungufu mengi sana.

Kitu muhimu nachojaribu kujenga hapa ni kwamba mimi natetea sana ushirikiano kati yetu na weusi wa Marekani nikizingatia kuwa Ubepari hauwezi kuepukwa kwa njia yeyote ile. Unatisha sana lakini ndio reality, lazima tuu -face ...
Wenzetu wote amefanya hivyo na tumeona mafnikio yao.
Hakuna watu matapeli kama Wayahudi lakini pindi walipoweza kuunda muungano kati yao kwa malengo ya kibiashara (mafia) kwa faida yao leo hii dunia nzima inawaogopa hali wapo kina Andrew Young kibao wala sii mmoja. Na hawa kina Andrew Young wao (watu wenye contact) wameweza kuingia hadi nchi za kiarabu kwa faida ya Myahudi. Kwa muda mrefu sasa wamekuwa tishio kubwa la uchumi za nchi nyingi hadi pale Wachina, Wahindi na mataifa mengine walipojifunza wao kuwa na ushirikiano. Wakaunda mafia zao vilevile kwa faida ya nchi zao, leo hii hawakamatiki.
Haya, ndio maisha ya Ubepari, ni vitendo vinavyotisha lakini havina mwepuko na ndio maana kila mji utakao kwenda leo hii utakuta mafia za kila jamii hata hao wahindi koko (Sri Lanka) ambao mnashangaa kuwaona wanaanza kupiga hatua kubwa ktk maendeleo ya jamii yao.
Hapa Tanzania leo hii mafia zetu zimejengwa dhidi ya wananchi wake wenyewe na kusema kweli hawana nguvu hata kidogo isipokuwa wakiwa madarakani. Hofu kubwa ya Mtanzania ni Mtanzania mwenzake na pengine somo langu kubwa ni kwamba Andrew Young na kundi lake sio tishio hata kidogo isipokuwa tishio kubwa ni sisi wenyewe kwa kutokuwa na msimamo mmoja na kuwa adui wa mwafrika kiuchumi bado tunamtazama toka nje hali wapo ndani mwetu kama kunguni. Hii haina maana kuwa huko nje hakuna maadui No wapo...lakini sio hawa jamaa hata kidogo na Andrew Young mtu mmoja hawezi kabisa ktuumiza vichwa ikiwa tutaweza kuondokana na makunguni...
JK ni mtu wa misifa, amedhihirisha wazi kuwa ana mapungufu mengi tu lakini sio hili la kushirikiana na weusi wenzetu. Nitaendelea kukataa kuwa sio Ubaguzi wa rangi ama kabila Mtanzania anapoamua kufunga ndoa na Mtanzania mwenzake hata kama Mtanzania ni binadamu mwenye mapungufu sawa na watu wengine toka nje, still kuna unafuu mkubwa ktk kuijenga nyumba kutokana na tamaduni na mila zenu kuwa sawa.
Mwisho ya yote haya ujumbe wangu ni ni kwamba haina maana support yangu inabainisha kuwa Weusi ama Watanzania pekee wote ni safi na watu wengine wote ni wabaya, laa wapo weusi na wapo wazuri pia , huko nje ya weusi pia wapo wazuri na wabaya isipokuwa nachoomba tutazame nje ya kabati la ufungwa wa akili na kujiuliza inakuwaje watu wengi wote wa mataifa hupenda kufunga ndoa na watu wa makabila yao hata wakiwa nje ya nchi zao?...
Hii ndio message yangu na kama wewe huchagui mchumba kutokana na vigezo hivyo hiyo ni imani yako wewe na itakuwa bora kama utanieleza mimi mazuri ya ndoa za aina hiyo. Na tofauti kubwa ya maelezo yangu na yako ni kwamba wewe hapa unamtazama mtu mmoja Andrew Young huyu mshenga ambaye siye tutakaye funga ndoa naye isipokuwa yule ataye mpendekeza. We still have the choice ya kusema huyo hafai, sasa ubaya wa huyu mshenga mbambe ni kitu gani haswa ikiwa sote tutaweza kugain at the end.. Hizo bia na chakula cha mchana pale Chef Pride?..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom