Elections 2010 Je,Dr.W Slaa anaweza kuteuliwa kuwa mbunge kama akikosa nafasi ya urahisi?

mbona mnaleta mijadala ya ajabu?? kwa nini tunajadili jambo ambalo bado muda wake, au mmetumwa?? matokeo bado, mimi naamini Dr Slaa ndo atakuwa rais wetu tuwe wavumilivu kusubili matokeo ya mwisho...
 
Hakuna sababu ya Dr Slaa kuwania kuingia bungeni kwa sasa, bali atumike kujenga msingi imara zaidi wa CHADEMA hasa vijijini, na mitaani kwa wanyonge, ili mwaka 2015 kazi ya ukombozi ikamilike
 
hatutafuti heshima hapa tunataka mabadiliko na yeye ndio muasisi wa yote SAUTI YA WATU NI SAUTI YA MUNGU, anacheleweshwa tu kuingia ikulu lakini 2015 yupo ndani ya nyumba nyeupe nyie vipi hamuoni huu ni muda wa kujiandaa ,haitaji kuingia mjengoni anatakiwa kujiandaa kuingia pale Baba yetu Nyerere alipo paheshimu kama Dk Slaa anavyopaheshimu
 
kinadharia ana nafasi, ingawa katika hali halisi nafasi hiyo ni finyu saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana. kwanini? rais ana mamlaka ya kuteua wabunge kumi, ambao kinadhari si lazima watoke katika chama chake (rais). hivyo kwa msingi huo slaa ana stand chance ya kupata ubunge kwa kupitia nafasi hizo kumi za uteuzi wa rais

lakini swali kubwa ni je rais (awaye yeyote atakaeshinda) atakua na utashi wa kumteua slaa kuwa mbunge? ukizingatia alivowachachafya bunge lililopita?
 
hapo zamani za kale ....palitokea......NCCR-MAGEUZI....ilivuma kuliko upepo wa kimbunga.......!
 
hapo zamani za kale ....palitokea......NCCR-MAGEUZI....ilivuma kuliko upepo wa kimbunga.......!


Safi kwa kulijua hilo " Zamani za kale " Well hapo zamani za kale palikuwapo Rais alieitwa Bokasa, maboutu seseseko unajua wewe utakuwa umeathirika na zile hadithi za zamani sungura na fisi, sizitaki mbichi hizi, adili na nduguze na kusahau kibanga ampiga mkoloni....Sasa hivi nia na kiu ya watanzania ni kumngoa mkoloni mweusi I mean mkoloni wa kijani bila kujali mtu yupo chama gani. Mwaka 1995 watu walijali sana vyama siku hizi hatujali vyama mie mmoja wao naweza nikampa diwani wa TLP, Mbunge CUF, Rais Chadema and vise versa kuzingatia nguvu ya mgombea husika. Kwahiyo kama bado unaota hadithi za kale katangaze kwenye kipindi cha mama na mwana RTD.
 
yes he can get the chance but it must be amongs the 10 reserved chances given to the president to select mp in his willing so if jakaya wishes to include slaaaa then atarudi mjengoniiiiii.viti maalum hawezi kupata sababu majina walishayapendekeza wenyewe chadema na tayari wameshayapeleka

Viti maalumu ni vya wanawake na sio vile 10 vya Rais.
 
members pls i need ur political inteligence......... can he get nominated in the special seats?

Kukubali uteuzi wa JK ni kuua demokrasia na kutusaliti watanzania wazalendo na wenye uchungu na nchi hii.
 
Mhe Godbless ametoa hali halisi. Ni kupitia dirisha dogo tu la viti 10 vya Rais au uchaguzi mdogo kama utatokea. Hata hivyo, nafikiri ni vyema akajikita kukijenga chama zaidi ukizingatia timu ya CHADEMA kubwa imehamia mjengoni akiwemo Mwenyekiti. Tunahitaji chama imara kwa chaguzi zijazo zikiwemo na chaguzi ndogo
 
Kwa mtazamo wangu mimi nadhani ni vizuri Slaa akabaki katibu mkuu wa chama kwa ajili ya kukijenga chama, kuhakikisha chama kinatanuka kufika sehemu nyingi za bara na visiwani, hili ni jambo la muhimu sana na litatusaidia sana kuwa na chama imara.

Kazi hii ni nzito sana, na pia akiwa nje still tuna vichwa vya kutosha sana bungeni sioni kama kutaharibika kitu. We need to build a strong CHADEMA.

umesema kweli kiraka. slaa abakie kuwa katibu mkuu wa chadema. licha ya kupata ushindi mkubwa wa viti vya wabunge ambao wametokana aidha na juhudi za slaa, vita vya panzi ndani ya ccm, kura za chuki etc mshikamano ndani ya chadema bado uko tete sana. tunataka kuona chadema yenye idadi nzuri ya sasa ya wabunge na chadema iliyo stable na yenye solidality ikiwania kupata ushindi mzuri zaidi 2015
 
Back
Top Bottom