Je Dr Lucy Nkya yuko sahihi juu ya hili?

Kichankuli

JF-Expert Member
Dec 18, 2008
887
189
Habari hii hapo chini ilichapishwa katika gazeti la Nipashe; je ni kweli kwamba Mafisadi wote ni Wanaume tu?, kwani yule Waziri wa Utalii kilichomliza pale Bungeni kilikuwa ni kitu gani?

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Lucy Nkya, amesema wanawake wamethibitika kutokujihusisha na ufisadi kwani katika kundi kubwa la watu wanaotuhumiwa kwa vitendo hivyo nchini kwa sasa limejaa wanaume, kwa hali hiyo ili kuvikomesha ni vema kuwachagua wanawake zaidi katika nafasi za uongozi.

Dk. Nkya alisema hayo alipokuwa akifungua warsha kuhusu ``Nafasi ya mwanamke na jinsia katika kuimarisha siasa na demokrasia,`` iliyoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), jijini Dar es Salaam jana.

``Katika haya masuala ya ufisadi yanayoendelea, nadhani mtakuwa mmeona kwamba hakuna mwanamke anayetajwa kuhusika. Hii inaonyesha kwamba namna nyingine ya kupambana na ufisadi ni kuchagua viongozi wengi zaidi wanawake katika nafasi za kisiasa,`` alisema Dk. Nkya.

Alisema baadhi ya mila na desturi zimekuwa zikikinzana na jitihada za kuleta usawa wa jinsia, hali ambayo imewafanya wanawake kuendelea kuelemewa na majukumu na mzigo mkubwa wa kazi, hata pale ambapo mabadiliko madogo tu ya kiteknolojia yangewapunguzia uzito huo.

Aliishukuru TCD kwa kutambua umuhimu wa kuwashirikisha wadau mbalimbali katika mijadala inayolenga kutoa elimu, hamasa, ikiwa ni pamoja na kuendeleza na kuimarisha jitihada zinazolenga kufikia lengo la asilimia 50 kwa 50 katika ngazi za uongozi na maamuzi katika siasa na utendaji.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba akiwasilisha mada katika warasha hiyo, aliwataka wadau kujadili nafasi ya wanawake kwa mapana wakati wanapotafuta Katiba mpya ya nchi.

Waziri Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Gharib Bilal, ambaye alikiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika warsha hiyo, alisisitiza mapendekezo ya CCM ya kutaka kila wilaya iwe na majimbo mawili ya uchaguzi ili kutoa fursa kwa wanawake wengi zaidi kuingia bungeni na kufikia idadi ya 50 kwa 50 iliyomo kwenye azimio la Umoja wa Afrika (AU).

Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama (CCM), alisema suala la usawa wa kijinsia, ni haki ya binadamu na si upendeleo kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Hata hivyo, Mbunge Viti Maalum, Halima Mdee (Chadema), alisema haina mantiki kuwa na wanawake wengi katika vyombo vya maamuzi, kama vile Bunge, huku mchango wao ukiwa ni mdogo katika chombo hicho.

Ingawa Dk. Nkya hakutaja ufisadi alioulenga, miongioni mwa kashfa za ufisadi zinazovuma nchini kwa sasa ni pamoja na wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jumla ya watu 21 wakiwa wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi huo.

Jumla ya Sh bilioni 133 zilichotwa EPA kifisadi na makampuni 22 yakiwa yamesajiliwa kijanjajanga. Miongoni mwa walioshitakiwa kwa tuhuma hizo ni wanaume 18 na wanawake watatu.

Kesi nyingine ambayo inahusu ufisadi ni ya kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond Development Corporation (LLC) ambayo mmiliki wake mwanaume, Naeem Gire, amefikishwa mahakamani.

Pia kuna kashfa ya Kamapuni ya Kagoda ASgriculture inayodaiwa kuchota Sh bilioni 40 za EPA, hata hivyo hakuna aliyeshitakiwa kwa sakata hili. Kashfa nyingine ni ya kamapuni ya kukagua tahamani ya uchimbaji madini ya Alex Stewart ambayo mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona wameshitakiwa kwayo, wakituhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Pia katika Alex Stewart aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Grey Mgonja, naye ameunganishwa katika kesi hiyo.

SOURCE: Nipashe
 
Behind every successful man there is a woman... behind wevery successful fisadi there is a woman. Does it make sense?
 
Dr Lucy alishinda kifisadi kwenye huo ubunge wake kwa tiketi ya wanawake kule moro.
Alihonga kanga na shilingi kati ya elfu kumi mpaka hamsini. jiulizeni hizi fedha alipata wapi na atarudisha vipi???
 
Zakia Meghji alikuwa waziri wa fedha wakati madudu mengi ya EPA yanafanywa na hata akajaribu kufichaficha mambo paka pale yalipomchachia; pia kuna wakinamama katika kundi la washitakiwa wa ukwapuaji wa EPA pale BOT ,kwahiyo ni dhahili kuwa ufisadi si swala la wanaume peke yao!!
 
Back
Top Bottom