Je China ni rafiki wa Nchi zinazoendelea au ni mnyonyaji mpya?

Iron Lady

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
4,071
1,363
tumeshuhudia jinsi ukoloni mambo leo unavyotutafuna na kutumaliza kidogo kidogo, baadhi ya nchi kama marekani na mataifa fulanifulani ya ulaya yamekuwa yakishinikiza sera mbalimbali za kutumalizia mali zetu na kuuzorotesha uchumi wetu.baadhi yetu tumekuwa tukiwaelewa kuwa ni wanyonyaji wakubwa na baadhi wamekuwa wakiendelea kuamini kuwa ni wasaidizi wa maendeleo ya nchi zetu masikini.sasa hivi sisi ni dampo la bidhaa feki na original za nchi za watu,sisi ndio eneo la kujaribia biashara na kujizolea mali na kuondoka haya yanafanywa na nchi nyingi za kigeni.

china inakuja kwa kasi katika uchumi wa dunia,imekuwa ikizitumia ipasavyo sera za soko huria bila kutumia nguvu za mapigano ikiwa inaendeleza urafiki wa kihistoria kwa baadhi ya nchi kama tanzania na kuujenga mpya katika mataifa mengine ya kiafrika kiasi cha kuonekana mwema na rafiki mzuri, lengo je ni kusaidia nchi za kiafrica au ni mnyonyaji yule yule wa lengo lilelile isipokuwa style tu?
 
Hakuna urafiki kati ya mtu aliyenacho na asiyekuwanacho na once urafiki huo unapokuwepo upo tu kwa sababu....
Marekani ni rafiki sana na watawala wa mataifa ya dunia ya tatu yenye rasilimali ghafi na lengo la urafiki huu ni kuondoka na raw materials kwa ajili ya viwanda vyao kwao..China as well! In short ukoloni upo, ila kwa njia ya kisasa!
 
Wajamaa hao ni zaman lkn wote ni mabepar tu kwa sasa! Wameshika kila sehemu kiurafiki na ni hatar Sana kwetu
 
Wajamaa hao ni zaman lkn wote ni mabepar tu kwa sasa! Wameshika kila sehemu kiurafiki na ni hatar Sana kwetu

Enzi za kina Mau ujamaa uliwezekana, Nyerere alijaribu ila alishuhudia kufail kwa ujamaa kabla kazi yake chini ya jua haijakamilika...Ujamaa upo sikatai ila ni ama ujamaa wa kibwanyenye ama ujamaa wa mafukara!
 
Back
Top Bottom