Kuna Mjasiriamali mmoja wa biashara ndogo ndogo (Small Scale Enterpreneur) alikopa toka Benki moja hapa nchini kwa makubaliano ya kurejesha mkopo kwa kiasi cha shs.289,000.00 kila mwezi. Biashara yake ikaenda mrama kwani aliyemkabidhi kuendesha biashara yake ametoroka na mtaji pamoja na faida kabla mkopo haujamalizika kulipwa wote. Naye sasa anarejesha mkopo huo kutokana na mshahara wake ambao kwa nafasi ya kazi yake haufikii kiwango cha marejesho ya mkopo alichokubaliana na Benki hapo awali. Ati Benki hiyo inataka kumfilisi kwa kukamata mali zake na kuziuza ikiwamo nyumba yake ya familia ili kufidia deni lililobaki. Je hatua hiyo ya Benki ni sahihi na halali katika macho ya sheria za Tanzania? Huyu Mjasiriamali maskini anaweza kusaidiwa vipi?
imwan
imwan